Outliers: the Story of Success

Hivi punde tu nimemaliza kukisoma kitabu cha Malcolm Gladwell kiitwacho Outliers: the story of success. Nimeona ni vyema kuwasilisha hapa machache kuhusu kitabu hiki ili nawe ukinunue na kukisoma. Kabla sijaendelea, ningependa kuweka bayana kuwa kitabu hiki sio ‘self help book’ – yaani vile tabu vinavyotoa listi ya ni yepi ya kufanya ili ufanikiwe kimaisha.

Katika makala iliyopita, SN alitupatia maswali na hoja muhimu kuhusu suala la motisha na mafanikio kiujumla kimaisha. Ndani ya Outliers, Gladwell anatupatia mwanga kuhusu sifa zinazowaunganisha watu kadhaa wenye ‘mafanikio’ katika nyanja mbali mbali. Anaeleza kuwa ‘mafanikio’ hayatokani na kipaji pekee yaani talent au genius, bali ni mjumuiko wa sifa ambazo mara nyingi hatuzifikirii kama bahati, malezi, mila, historia ya familia/uzawa n.k. Ni muhimu pia kuweka bayana kuwa hapa haongelei ile bahati kama ya kushinda bahati nasibu, bali aina ya bahati ya kuwa ‘at the right place at the right time’ na kuwa na uwezo wa kuitumia nafasi hiyo kwa manufaa yako kiufanisi.

Malcolm Gladwell ana kipaji cha kuchambua tafiti mbalimbali za sociology na kuzielezea kwa ufanisi kwa mtu wa kawaida (layman). Kwenye Outliers, anaelezea thesis yake kwa kutumia mifano ya maisha ya akina Bill Gates, Mozart, kundi maarufu la muziki the Beatles n.k. Anatuelezea kuwa Gates, ukiachilia mbali uwezo wake kielimu, mafanikio yake katika software industry yalitokana na kuwa na ‘bahati’ ya kusoma katika shule ya sekondari iliyokuwa na computer maalum isiyotumia punch-cards (pekee nchini US kwa wakati huo) iliyomwezesha kufanya mazoezi kwenye fani hiyo kuzidi wenzake. Nafasi hii na nyinginezo zilimwezesha ku’accumulate zaidi ya masaa 10,000 ya programming kabla hata hajaanza chuo, na hivyo kumfanya awe mtaalam kwenye fani. Anatueleza pia kwamba wale Beatles, chimbuko la umahiri wao katika muziki ulianza tu baada ya kupata ‘bahati’ ya kualikwa mara kwa mara jijini Hamburg kwenye shoo ndogo-ndogo zisizofahamika, na hivyo kuweza ku’accumulate masaa yao 10,000 ya mazoezi kabla hata ya kuanza kutumbuiza katika shoo kubwa.

Ndani ya Outliers, Gladwell anaeleza mifano ya umuhimu wa uzawa katika mafanikio, anatoa maelezo kwanini wayahudi wengi wanaendesha uchumi wa miji kama New York. Ohh, na pia hujawahi kujiuliza kwanini Wachina/Wakorea/Wajapani wengi ni wakali katika hisabati? Hasa hasa Wachina tunaokumbana nao vyuoni huku ulaya na marekani? Gladwell anaelezea kuwa chimbuko ni kutokana na lugha zao kuwapa advantage fulani katika kuhesabu, yaani zipo very concise kuzidi lugha kama kiingereza au nyingine nyingi. Sijui kiswahili kikoje katika fikra hii, ila hii ni mada nyingine ukizingatia kuwa nchini TZ hisabati bado ni gonjwa sugu.

mwandishi Malcolm Gladwell
Kitabu hiki kinachochea fikra, na ni aina ya vitabu ambavyo kijana wapaswa kusoma. Binafsi nimevutiwa na insights hizo mbalimbali, ingawa katika baadhi ya ‘stori’ kunakuwa na oversimplification fulani katika kutafuta chanzo – masuala ya causality na correlation. Ila utaweza kupata mwanga kuhusu ni yepi yanawafanya baadhi ya watu kuwa wa pekee. Are YOU an outlier? Je, tayari umeshakusanya masaa 10,000 katika fani uliyopo sasa?

Waweza kukinunua Outliers hapa: http://www.amazon.com/dp/0316017922
Soma kazi zake nyingine hapa: http://www.gladwell.com/

Previous ArticleNext Article
Joji was born and grew up in Dar es Salaam, Tanzania. He graduated with a B.Sc in Biochemistry in Germany, and is now pursuing a Masters degree in Microbiology & Immunology at the Swiss Federal Institute of Technology (ETH) in Zurich, Switzerland . Joji is particularly interested in matters related to global health, and basic science research that tackles public health challenges. He is engaged in mentoring Tanzanian students in higher education issues, most notably at the Kibaha High School. In this capacity, Joji blogs with Vijana FM about scientific research and development, and how youth can gain greater access to higher learning.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Send this to a friend