Kimya chenye mshindo mkuu

Hatimaye kile kimya cha muda mrefu cha Nakaaya Sumari kimeisha. Baada ya da’ Nakaaya kuanzisha blog yake na kutangaza kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo aliingia chimboni.

Wachache wetu tulisikia tetesi juu juu tu mwanzoni mwa wiki hii kuwa Nakaaya anapanga kugombea ubunge kwa tiketi ya CHADEMA. Na mchana wa leo Nakaaya amevunja ukimya kwa kutangaza nia yake ya kugombea ubunge wa viti maalumu Arusha.

Binafsi, napenda kuchukua fursa hii – kama Kijana – kumpongeza kwa kujishughulisha na Siasa na kuamua kupigania anachoamini. Wale wenzangu ambao bado wanadhani kujitosa kwenye Siasa ni kupoteza muda, labda matukio kama haya yatawafanya mfikirie upya.

Lakini, kama nilivyosema siku chache zilizopita, kwa kuwa hawa Vijana wenzetu wana mvuto kwa watu wa rika letu, ningependa kuwasikia wakitueleza mambo ya msingi. Nini kinawasukuma kujiunga na chama fulani? Sera gani hasa za vyama wanazoziangalia?

Kwahiyo mimi kama mshabiki wa baadhi ya hawa Vijana waliojiteza na kujitosa kwenye Siasa, nitaiminya kura yangu mpaka nitakapopata majibu!

Picha kwa hisani ya Nakaaya blog
.

Previous ArticleNext Article
Steven was born and raised in Dar es Salaam, and moved to Germany for his studies. He graduated with a BSc. in Physics (Jacobs University Bremen), and then a MSc. in Engineering Physics (Technische Universität München). Steven is currently pursuing a PhD in Physics (growth of coatings/multilayers for next generation lithography reflective optics) in the Netherlands. He’s thinking about starting his own business in a few years; something high-tech related. At Vijana FM, Steven discusses issues critical to youths in Tanzania, music, sport and a host of other angles. He’s also helping Vijana FM with a Swahili translation project.

This post has 1 Comment

1
  1. Hongera sana dada Nakaaya kwa kujikita katika Siasa ila mziki ndio kwaheri tena au utakuwa 'maltipapasi'?? natumaini tutaona mabadiliko katika Inchi yetu ukizingatia wewe ni kijana na wafahamu nini kifanyike ili tuweze kuitoa inchi yetu katika janga tuliokuwa nalo kwa sasa.

    nafikiri huu ni mwendelezo mzuri kwa vijana kujikita katika vyama fulani kutoka na sera zao kwa maendeleo ya inchi kwa ujumla na sio kwa manufaa yao kama viongozi wengi.

    Naamini vijana wengine watajitokeza na kujikita katika siasa maana tunahitaji vijana ambao wataleta maendeleo katika inchi na sio kukaa/kuendelea na wazee tu, sio kama wagombea wazee siwataki la hasha busara zao,ukongwe na ushauri utaitajika kwa wagombea vijana ili ''libeneke'' liweze kwenda sawa.

    Nakutakia safari njema katika uwanja wa siasa dada Nakaaya na Mungu akubariki.

    Asante.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Send this to a friend