Nelson R. Mandela – 46664

Tarehe 18 Julai ni Siku ya Mandela. Ili kusheherekea siku hii, nimeamua kuwakumbusha historia ya Mzee Madiba.
Nelson Mandela; na Sue Dickinson

Filamu ifuatayo ni ya historia ya Nelson Rolihlahla Mandela, kwa maneno yake mwenyewe — kwa kifupi. Angalia jinsi wazee wetu walivyotaabika, wakajitoa mhanga ili mimi na wewe leo tuweze kusimama bila uwoga na kutembea mitaani na vifua vyetu mbele.

Sijui unapata hisia za aina gani unapoona na kusikia hadithi kama hizi. Binafsi, napata motisha isiyo kifani na sichoki kuwashukuru wanaharakati kwa mambo waliyofanya. Leo hii naweza kuandika chochote ninachotaka kwenye blogs na vyombo vingine vya habari; sauti yangu inasikika. Sitetereki pale mtu anapoanza kunirushia maneno ya kibaguzi. Naamini kuwa sehemu kubwa ya mafanikio kwenye maisha yangu itatokana na juhudi zangu mwenyewe.

Bahati mbaya watu wengine wanatumia uhuru huu huu kujinufaisha wenyewe na familia zao; wamesahau machozi, jasho na damu ya wanaharakati kama Madiba. Wamewahi kujiuliza: Tungekuwa wapi kama watu na viongozi kama hawa wangeamua kupigana kwa ajili yao na familia zao tu?

Previous ArticleNext Article
Steven was born and raised in Dar es Salaam, and moved to Germany for his studies. He graduated with a BSc. in Physics (Jacobs University Bremen), and then a MSc. in Engineering Physics (Technische Universität München). Steven is currently pursuing a PhD in Physics (growth of coatings/multilayers for next generation lithography reflective optics) in the Netherlands. He’s thinking about starting his own business in a few years; something high-tech related. At Vijana FM, Steven discusses issues critical to youths in Tanzania, music, sport and a host of other angles. He’s also helping Vijana FM with a Swahili translation project.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Send this to a friend