Study abroad – Tanzanian students’ perspectives

Name: Patrick
Institution of study: Osmania University – Hyderabad, India
University study program: Computer Applications
High School: Mzumbe Secondary School – Morogoro

Kwanini ulichagua kusoma nje ya nchi? Program hii haipo vyuoni Tanzania?

Ni baada ya kupata usumbufu mkubwa toka Bodi ya mikopo ya elimu ya juu. Hii program ipo nchini Tanzania.

Ni masuala yapi muhimu ya ulizingatia wakati unatuma maombi katika chuo unachosoma sasa au pengine ulipotuma maombi?

Nilizingatia hasa uwepo wa udhamini wa masomo yaani Scholarship.

Vipi masuala ya gharama ya elimu na maisha – scholarship zipo?

Scholarship zinatolewa na Ubalozi wa India nchini Tanzania uliopo katika barabara ya Kinondoni, Plot # 82.

Ni changamoto gani ulikumbana nazo kuhusu transition kutoka maisha ya masomo Tanzania na hapo ulipo?

Mazingira mapya, tofauti ya tamaduni na jamii mpya ilinichukua muda kuyazoea mazingira.


Je, mtaala wa elimu yetu ya Tanzania ulikusaidia vipi katika mwaka wako wa mwanzo wa masomo hapo? Au ni juhudi zako binafsi?

Masomo kama Mathematics kwa Tanzania ni mazuri na yalinisaidia nilivyojinga hapa hasa mwaka wangu wa kwanza.

Utamshauri nini mwanafunzi aliyesoma A-level na kutahiniwa na NECTA kuhusu kutuma maombi katika chuo chako?

Kama anapata nafasi katika vyuo vya Tanzania ni bora tu kusoma nyumbani.

Kuna watanzania wangapi chuoni kwako?

Kama mia moja hivi.

Swali la kizushi: Una mpango wa kurudi Tanzania?

Ndiyo, nikimaliza Elimu yangu nitarudi Tanzania

*  *  *  *

Name: Steven
Institution of study: Harvard University – MA, USA
University study program: Electrical Engineering and Computer Science
School: Ilboru Sec. School – Arusha (O’ level) & International School Moshi (ISM)

Kwanini ulichagua kusoma nje ya nchi? Program hii haipo vyuoni Tanzania?

Gharama: Nilibahatika kupata ufadhili kutoka chuoni Harvard na hivyo kwangu ikawa gharama nafuu zaidi kwenda kusoma huko kuliko kusoma nyumbani Tanzania.

Program: Mpaka namaliza International Baccalaureate (IB) diploma pale ISM, sikuwa na uhakika kuwa nisome nini. Vyuo vya Marekani vinaruhusu kujiunga hata kama hujaamua nini cha kusoma (undecided).

Ni masuala yepi muhimu ya ulizingatia wakati unatuma maombi katika chuo unachosoma sasa au pengine ulipotuma maombi?

Aina ya chuo: Kuna aina nyingi za vyuo. Mimi nilikuwa natafuta chuo ambacho kinatoa degree ya kwanza (Bachelors) katika sayansi au sanaa, na kinachotambulika kimataifa (accredited).

Ufadhili: Nilitafuta vyuo ambavyo vilikuwa na program za ufadhili. Kuna vyuo ambayo vina program mbalimbali za scholarship pamoja na financial Aid. Vyuo hivyo huwa vinaitwa Need Blind (Yaani admission haitegemei uwezo wa mtu kifedha. Wana-admit waombaji kwanza halafu wanaangalia kama wana uwezo wa kulipia au hawana. Kwa wasiokuwa na uwezo wa kulipia, wanawapa Scholarship). Scholarship hizi zinaweza kuwa 100% au chini ya hapo, ambapo muombaji kuhitajika kuchangia kiasi kinachobakia.

Ni muda gani mzuri wa kuanza na maandalizi ya kutuma maombi ya chuo huko ulipo?

Nilianza maandalizi miaka miwili kabla ya kutuma maombi. Kumbuka applications inajumuisha vitu vingi sio matokeo tu ya darasani. Kuna personal statement, recommendations, extracurriculars activities n.k. Nilipata bahati ya kuwa na mwalimu aliyenidokeza haya tangu mwanzoni. Nilijua uwezo wangu wa kuandika insha ulikuwa wa wastani kwahivyo ilibidi niongeze bidii na kufanya mazoezi. Pia nilijenga uhusiano mzuri na walimu waliokuwa wananifundisha maana baadaye niliwaomba waniandikie recommendation letter. Nilijitahidi kufanya vizuri darasani wakati wote, hata assignments ndogondogo maana hizi pia zinatumwa kama sehemu ya application yako.

Utamshauri nini mwanafunzi aliyesoma A level na kutahiniwa na NECTA kuhusu kutuma maombi katika chuo chako?

Ofisi za admission katika vyuo vya huku marekani hawaangalii grade zako peke yake, wanathamini sana pia jinsi gani unajihusisha na shughuli za nje ya darasani kama vile uongozi, michezo n.k. Ili uwe na application nzuri, anza maandalizi mapema. Tangu unapoanza form five, hakikisha unafanya vizuri darasani na nje pia. Kama shule yenu haina extracurriculars zaidi ya michezo fikiria jinsi gani mnaweza kuanzisha vyama vingine na wenzako. Tafuta washauri wazuri kama vile walimu au watu wengine waliotuma maombi miaka iliyotangulia n.k. Jenga/tafuta namna ya kujiandaa kufanya mitihani ya SAT na TOEFL. Jifunze kuandika insha vizuri maana utahitaji kuandika personal statement kwenye maombi ya chuo.

Ni ushauri gani utampatia mwanafunzi wa A level kuhusu namna ya kujitayarisha na mtihani wa Standardized Assessment Test (SAT)?

SAT: Practice, practice, practice and when you’re done, practice some more! Sehemu ya hesabu most likely itakuwa sio ngumu sana lakini practice anyways.

Sehemu ya Critical Thinking and Writing: Hii section kwa kweli ni ngumu! Hata wenyewe wa huku zinakotungwa wanaona ngumu. Kwahiyo nadhani ushauri ni kupractice tu. Kuna vitabu mbalimbali (najua pale ubalozi wa Marekani wanavyo kwenye Library yao) pamoja na resources nyingine kwenye mtandao ambazo zinasaidia katika maandalizi ya hii kitu!

Ni changamoto gani ulikumbana nazo kuhusu transition kutoka maisha ya masomo Tanzania na hapo ulipo?

Writing: Kuandika Insha (papers) ni sehemu kubwa sana ya maisha ya kimasomo katika vyuo vya Marekani. Niliposoma IB pale ISM sikuwa nimesoma masomo ambayo yalihitaji kuandika intensively isipokuwa Kiswahili na hii ilifanya transition ya kuandika papers kuwa ngumu. Hata hivyo chuo kilikuwa na resources mbalimbali za kusaidia wanafunzi waliokuwa na changamoto kama hii.

Kasi: Kila kitu kilikuwa kinafanyika au kwenda kwa kasi sana nikilinganisha na nilivyokuwa nimezoea kabla ya hapo. Lakini baada ya muda nilizoea kasi hii mpya.

Jambo lingine kubwa lililokuwa changamoto ni kujijengea tabia, yaani utamaduni wa kujifunza jinsi kujifunza (learning how to learn). Ufundishaji wa chuoni (nafikiri ni vyuo vingi ulimwenguni) ni tofauti sana na wa elimu ya kabla ya chuo. Chuoni, mara nyingi niliona kuwa maprofesa wanatumia mbinu.

Ni yapi yanayohimizwa zaidi huko kuliko Tanzania, na ni yapi unadhani Tanzania tunahimiza na hauyaoni huko?

Kwa uzoefu wangu katika shule za nyumbani, kuna utamaduni wa kusomea mitihani. Mtihani wa mwisho unapewa kipaumbele sana kiasi kwamba mandeleo ya kila siku darasani yanaonekana kutokuwa na uzito wowote. Hii ilikuwa tofauti na pale ISM ambapo maendeleo ya kila siku darasani kuanzia kwenye homework, tests na assignment nyingine yanapewa uzito katika matokeo yako ya mwisho. Kwa kifupi mtu unakuwa unaandaa matokeo yako tangu siku ya kwanza unapoanza shule. Mfumo huu pia ndio nilioukuta hata huku chuoni. Assignments zote zina nafasi yake katika matokeo yako mwisho wa muhula.

Kuna Watanzania wangapi chuoni kwako? Kama hawapo wa kutosha unadhani tatizo ni lipi, kama wanaotoka nchi jirani ya Tanzania ni wengi zaidi?

Nilipokuwa nahitimu, tulikuwa Watanzania wawili (mimi na mwingine yuko mwaka wa tatu). Nimepata fununu kuwa wanakuja wengine wawili Septemba. Nafikiri kutokuwepo kwa Watanzania wengi hapa chuoni inatokana na watu kutotuma maombi, na pia kukosa maandalizi thabiti. Watanzania wote ninaowajua ambao wamekuja kusoma hapa walisoma katika mtaala wa IB. Kuna haja ya kujenga mfumo utakaowawezesha wanaofanya mtaala wa NECTA kuweza kutuma maombi na kufanikiwa kuja.

*  *  *  *

Much thanks to Pat and Steve for your insightful information!

If you are an East African student studying abroad and would like to take part in this project, drop a line at: joji (at) vijana (dot) fm.

Previous ArticleNext Article
Joji was born and grew up in Dar es Salaam, Tanzania. He graduated with a B.Sc in Biochemistry in Germany, and is now pursuing a Masters degree in Microbiology & Immunology at the Swiss Federal Institute of Technology (ETH) in Zurich, Switzerland . Joji is particularly interested in matters related to global health, and basic science research that tackles public health challenges. He is engaged in mentoring Tanzanian students in higher education issues, most notably at the Kibaha High School. In this capacity, Joji blogs with Vijana FM about scientific research and development, and how youth can gain greater access to higher learning.

This post has 16 Comments

16
  1. Patrick ukipata muda itakuwa sio vibaya ukatueleza kwa kifupi kuhusu hili jibu lako:

    Utamshauri nini mwanafunzi aliyesoma A-level na kutahiniwa na NECTA kuhusu kutuma maombi katika chuo chako?
    Kama anapata nafasi katika vyuo vya Tanzania ni bora tu kusoma nyumbani.

    Steven amegusia tena jambo ambalo tulijadili kwa kifupi kwenye makala iliyopita, na nadhani wahusika hawana budi kufungua macho. Hakuna haja ya kuanza kutupia lawama wizara husika (najua hiyo ndio itakuwa njia rahisi).

    Lakini mimi na wewe tunajua kwamba kuwa kwenye timu ya shule (ya kikapu au boli), kufanya midahalo (enzi zile nilikuwa nadhani ni ubishoo tu; kwasababu washkaji zangu walikuwa na slang nyiiiingi!), kutembelea na kusaidia vituo vya watoto yatima (huu ni wajibu, sio lazima iwe kwenye mtaala wa elimu) na mambo mengine kama hayo ni mapenzi ya mtu binafsi na ni rahisi kutekeleza. Wanaohitaji msaada tunaweza tukawasaidia kwa kuwapa majina ya vituo mbalimbali.

  2. nitapataje uthamini wakusoma nje ya nchi?ni mtanzania nilie malizia olevel uganda na jibu yalikua mazuri tu.natafuta uthamini wa masomo nje

    1. Salamu kwa Watanzania wenzangu.
      Naitwa Norbert na ni specialist katika sayansi kuhusu maisha maarufu kama Science of Creative Intelligence taaluma muhimu iliyoasisiwa duniani na mwanasayansi mkongwe Maharishi.

      Kama unatafuta mahala pa kusoma tunaweza kukusaidia kupata nafasi ya kusoma bachelor na masters pamoja na kupata financial aid chuoni hapo.
      Ni chuo cha Maharishi University of Management angalia http://www.mum.edu
      MUM wanachukua wale wa masters hasa wa accounting na computer science.
      Kama ni mtanzania unaweza kujaza fomu online na unapojaza kuna mahala utaulizwa agent namba ya Tanzania weka TZA-001

      Naomba uwajulishe wengine wenye shida ya kupata ufadhili na nafasi ya admission katika vyuo mbali mbali.
      Ukiwa na swali piga simu 0755 29 66 74
      Au andika chuoni kwa Craig
      Mungu akubariki.

  3. Am real impressed by your effo about srt toward making Tanzanian’s youth dream come true.Am soory ,how about master’s sponsorship.

  4. @Marro, of course, we look forward to hearing from Masters students as well, and we continue to maintain a list of resources for education. Let us know if you’re looking for something particular, or if you would like to contribute something! Cheers.

  5. hi,I am dani a form five student at ndanda high school.I wish to have a chance of getting a scholership because my future is now getting a hole between since the lost of my lovely dad.what should I do please help me

  6. kaka Mimi yatima napataje hiyo chance ,nilifanikiwa kumaliza o-level , nikakosa msaada wakuendelea mbele.Nimezipenda sana post zako.

  7. Hi guys..
    mimi ni mtanzania nina miaka 23 vilevile nina diploma ya law with shariah niloichukuwa pale muslim university of morogoro. swali langu kwa wadau wa hapa ni kuwa nitawezaje kupata nafas ya kusoma nje ya tanzania ngazi ya bachelor hasahasa nchi ya UK au US plerase naombeni msaada wa kuelezwa procedures

  8. ok sawa , mnawasaidiaje vijana wenzenu wanaotaka kwenda kusoma nje lakini hawajui pa kupata msaada?

  9. Will I get a scholarship to study abroad for my diploma regardless am not a degree scholar? Where to go? What to do?

  10. namaliza advance mwakani nahitaj kusoma nje ya nchi lkn cna uwezo nahtaj msaada wenu watanzania kitaaluma nipo vzr

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Send this to a friend