Sweet dreams

Steven was born and raised in Dar es Salaam, and moved to Germany for his studies. He graduated with a BSc. in Physics (Jacobs University Bremen), and then a MSc. in Engineering Physics (Technische Universität München). Steven is currently pursuing a PhD in Physics (growth of coatings/multilayers for next generation lithography reflective optics) in the Netherlands. He’s thinking about starting his own business in a few years; something high-tech related. At Vijana FM, Steven discusses issues critical to youths in Tanzania, music, sport and a host of other angles. He’s also helping Vijana FM with a Swahili translation project.

This post has 8 Comments

8
  1. an inspiring story indeed! A similar dream should be taken to the Tuareg of Niger, a country most of whose land, unlike Rwanda, is a desert…per capita GDP is 400 USD. Sad is they have recently discovered Uranium but with this discovery comes the radiation that the locals are victims of…!

    Gone are the days when one wishes to make a change only in their own countries, Now is the time when it is important to work for a global community…!

  2. Hii documentary kwa upande mwengine inatoa changamoto kwa Watanzania.
    Wengi wetu tunatenda tunayotenda kwa ajili ya personal gains tu na wala huwa hatuna malengo ya kusaidia jamii. Kwa Watanzania wengi nafsi kwanza, jamii na taifa baadae hata kwa wale walio katika nyadhifa za juu za uongozi.

    Tunasahau kuwa hata ukiwa wewe umeelimika na kuwa na mafanikio kedekede hutaweza kuishi kwa furaha katika jamii yenye tofauti kubwa na wewe.

  3. @hyperkei

    Jambo la kwamba bongo watu wengi wanaangalia nafsi zao kwanza kwa kiasi fulani mi naweza kuwaelewa. Maana wao wenyewe ndo kwanza matatizo ni kibao, sasa wasaidieje jamii wakati wao wenyewe bado wanamatatizo kibao? Mi nadhani wanachofanya ni kwamba “wanasaidia jamii wakati wao pia wakijisaidia.” Hii ni tofauti sana na yule anayesaidia nafsi yake peke yake na pengine ndugu zake wachache. Ndo maana pia hata hawa matajiri wakubwa wa Kimarekani huanza kusaidia jamii baada ya kuzeeka, ama baada ya kuwa wametimiza mahitaji yao. “This is normal.” Mi naweza kuwaelewa kabisa. Sema ni jambo tofauti kwa yule anayetanguliza jamii kwanza kabla ya kujisaidia yeye mwenyewe. Hii inaweza pia kufananishwa na yule ambaye alimsaidia ombaomba barabarani hadi na yeye akawa ombaomba.

    Ila kama utamaanisha “civil servants”, kweli hapo kunakuwa na tatizo kama watajali nafsi zao kwanza, maana hawa wamepewa dhamana ya kuhudumia jamii, na mafanikio yao yanapimwa kwa ubora wa maisha/huduma wanazotoa kwa jamii!

  4. Bihemo, umeshawahi kusikia huu msemo: “Bihemo, usitunyime harusi bwana! Hiyo ni ‘haki’ yetu. Bila sherehe kubwa hatutamtambua shemeji!”

    Halafu, mtu — ndugu wa karibu kabisa — akihitaji hela za kwenda chuo (Bongo au nje ya nchi), kajaribu kuwaomba msaada wa fedha watu hao hao wanaosema harusi kubwa ni ‘haki’ yao.

    Au wangapi hupenda kwenda kuwaona hata ndugu zao wagonjwa wanapolazwa hospitalini? Hudhani labda zile gharama zoooote wakati wa mazishi labda zingeweza kurefusha maisha ya mgonjwa kwa kipindi fulani kwa kumpatia mahitaji muhimu? “Kazi yake Mola haina makosa.”

    Nawaambia hivi, nipe jukumu lolote unalofikiria sasa hivi, mimi nitaandika kitabu kizima cha vizingizio (vya Watanzania).

    Nafahamu kuwa natengeneza maadui; lakini ukweli hauna uchi.

    Fikiria… “Leaders are reflection of their (respective) society/societies.” Uwiano uliopo huko juu (Bungeni) hauko tofauti sana na wengi wetu ”wazalendo”. Nani hapa hajawahi kutoa ‘hela ya soda’, au kutumia mtu unayemjua ili ishu zako ziende fasta?

    Nitaweka documentary nyingine baadae kidogo inayohusu vijana na watoto kutoka Kongo (Kinshasa). Hiyo ilinigusa kuliko hii ya ashkilimu.

  5. SN, hahaha…! “Kutoa soda bongo ndo mwendo mdundo..” Ngoja kwanza nisome, naona kuna quiz hapa inasumbua akili yangu…nitakujibu kwa kirefu zaidi, baadaye!

  6. @SN

    Nilitaka kuongezea kuhusu hilo la “soda ndogo…” Miaka miwili iliyopita, naamini hali bado iko hivyo hivyo, ulikuwa ukienda idara ya Uhamiaji pale Dar kutafuta Passport utaambiwa “Passport yako itatoka baada ya mwezi mmoja….”! Lakini ukweli wa mambo ulikuwa, ukitaka uipate siku hiyo hiyo passport hiyo utaipata…kama kuna ndugu yako atakufanyia labda bure, ila wengine watakufanyia kwa pesa. Ni kwamba watakujazia hadi mtaa unakoishi, na mihuri (wenyeviti wa mitaa/wajumbe wa nyumba kumi) pia wanayo !

    Sasa nikaenda ofisi moja pale Dar siku moja katika mihangaiko fulani fulani ya kimaisha….nikataka kuonana na bwana mmoja…mbunge fulani hivi na anashughuli nyingine nzuri nzuri! Nilikuwa na vimawazo vyangu na niliomba nionane nae. Kuna hawa dada zetu tunaowaita “secretary” unaowakuta reception. Hawa kazi yao ni kuwarudisha nyumbani wanaoonekana hawana kama “hohehahe”. Wanachofanya ni kujaribu kutatua shida zako pale pale, wao ndo wanakuwa huyo “mbunge” unayetaka kuongea naye. Appointment hupati ng’o. Utamaliza soli ya viatu ukirudi kufuatilia kama appointment yako imefanyiwa kazi..!

    Kuna mambo mengi nyumbani…mengi yanaudhi! Lakini pengine viongozi wetu kama wangeamua kuongoza mifano, kama unavyosema, mambo mengine yangefanyika kirahisi bila milolongo!

  7. Bihemo

    Tanzania inaendekeza rushwa mpaka imejijengea mazingira ya kulazimisha mtu kutoa rushwa.

    Chukua mfano wa airport. Wameweka scale za kupimia mizigo ndani (watu wako wanakuwa weshaondoka), kisha mzigo ukizidi hata chini ya 5kg (ambazo zinaruhusika katika mashirika ya kimataifa) wanakuambia ulipie au uwape rushwa. Bahati mbaya wengi wanaangukia kwenye kutoa rushwa.

    Tuende hospitali, ma nurse hawakupi huduma mpaka uwape rushwa na madaktari vile vile.

    Waliofungua huduma za kutoa elimu, hawatutozi rushwa lakini wanatuuzia hizo elimu kwa bei ambayo hailingani na thamani ya huduma yenyewe.

    Ukienda bungeni inabidi ujiulize wangapi wameenda pale kwa ajili ya wito wa kusaidia jamii na wangapi wameenda pale kwa sababu ndio njia rahisi ya kupata utajiri.

    Tatizo la ubinafsi liko kuanzia ngazi ya chini kabisa hadi juu.

    Hakuna anaejali iwapo Mkoani Mara kuna wasichana watafanyiwa ukeketaji au Geita kuna zahanati ukienda hutibiwi mpaka wende na maji yako.Kila mtu ni ‘rabbi rabbi nafsi’ tu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Send this to a friend