Tanzania na tatizo la umeme

Na Sakura

Katika kuumiza kichwa kutafakari suala la umeme nimekumbana na takwimu zilizonifanya nione maruweruwe!

Load profile inaonesha kuwa matumizi makubwa ya umeme — yaani, peak demand — ni wakati wa kuanzia saa kumi na mbili jioni hadi saa tano usiku, ambayo kimsingi ni matumizi ya majumbani na biashara ndogo ndogo. TANESCO inasema kuwa inahitaji kutumia nishati kama mitambo ya SONGAS na mengineyo (IPTL, DOWANS) ili kukidhi hitaji hilo hususan wakati wa msimu wa kiangazi, na hivyo kupandisha gharama za uzalishaji umeme kwa kila unit moja.

Daily Load Shape - 2008. Source: Long Run Marginal Cost of Service Tariff Study-Report (May 2010).

Mbaya inakuja wateja wa wakati huo wa peak si kama wanatumia umeme mwingi kila mmoja, ni ile wapo wengi mno na wanahitaji kutumia umeme kwa wakati mmoja. Na hata ukiwaambia wabane matumizi labda wakae gizani kwa hiari badala ya kwa lazima kama ilivyo sasa kwa vile umeme majumbani hautumiwi zaidi ya matumizi ya lazima, na kila chumba kimoja cha kupanga si kama kina zaidi ya taa mbili!

Peak Day Operation by Plant - Oct, 2008. Source: Long Run Marginal Cost of Service Tariff Study-Report (May 2010).

Linapokuja suala la ruzuku ili kufidia matumizi ya hao wateja wadogo-wadogo, serikali isharuka kimanga, TANESCO imeambiwa ibebe msalaba wake mwenyewe.

Wakati TANESCO iking’ang’ania kuwa bei ya sasa haikhalis, je, TANESCO ina haki ya kupandisha bei hata kwa wateja wake wadogo ili kujiendesha?

Je, ni haki kwa serikali kuingilia maamuzi ya TANESCO iwapo tayari imeshajivua lawama?

Je, kuna njia mbadala ya kukabiliana na suala hili?

Vyanzo, taarifa zaidi na makala nyingine:

Previous ArticleNext Article
Steven was born and raised in Dar es Salaam, and moved to Germany for his studies. He graduated with a BSc. in Physics (Jacobs University Bremen), and then a MSc. in Engineering Physics (Technische Universität München). Steven is currently pursuing a PhD in Physics (growth of coatings/multilayers for next generation lithography reflective optics) in the Netherlands. He’s thinking about starting his own business in a few years; something high-tech related. At Vijana FM, Steven discusses issues critical to youths in Tanzania, music, sport and a host of other angles. He’s also helping Vijana FM with a Swahili translation project.

This post has 4 Comments

4
  1. Nice to finally see some data coming from TANESCO. Any chance of these graphs being issued on a monthly basis so that Tanzanians know how much they consume on an aggregate scale?

  2. Data zipo kibao ni suala la kusearch kidogo tu kwenye internet.

    Ewura wamekuwa wakitoa ripoti zote za TANESCO za maombi yao ya kuongeza bei ya umeme. Kwenye ripoti hizo kuna data zote hadi za kifedha pamoja na vielelezo vyake (hadi wanabodi wamelipwa milioni mia ngapi kwa mwaka!). Si rahisi tu kwa waaandishi wetu kukubali kusoma kurasa 400 au 500 kupata habari. Wao wanasubiri kupewa taarifa zilizokwisha fanyiwa digestion ndo wazitoe. (I don’t remember the last time I saw a graph of any kind in a Tanzanian Swahili newspaper )

    Tukiacha hilo upande; serikali inatakiwa kutoa ruzuku kwa TANESCO ili kukidhi tofauti ya bei ya uzalishaji na ile wanaouziwa wateja maskini (life-line tarrif customers-D1) kwa sababu inavyoonekana sasa ni kuwa TANESCO inajilipa fedha zake kwa kutoza bei ya juu kwa wateja wake wa T1 (Domestic) na kuanzia T2 na kuendelea (commercial customers) na bado haitoshi.

    Na hapa TANESCO inapolipisha bei ya juu kwa wateja wa T1 ni tayari adhabu inarudi kwa wale wale wanaotakiwa kupewa huduma ya D1 kwa sababu kwa kila nyumba moja ya kupanga inatozwa bei ta T1 haijalishi kama kila chumba kimepangwa na mteja wa D1.

    Juu ya hivyo TANESCO ilivyosasa haiwezi kujiendesha maisha, kwa sababu hakuna uwekezaji wowote unaofanywa kwenye production. Malipo wanayouza umeme yote yanageuka malipo kwa mitambo ya kukodi kama IPTL, DOWANS,SONGAS na kwengine.

    Nahisi bora hata TANESCO wangetukatia umeme miezi mitatu mfululizo (kama walivyokaa Zanzibar) iwapo watatuaminisha kuwa baada ya hapo tatizo la umeme litakuwa limeisha kabisa kwa TANESCO kununua mitambo yake wenyewe badala ya kulipa kila siku mamilioni kwa mitambo ya kukodi.

  3. Solution for “TATIZO LA UMEME TANZANIA”. competition, competion, competion!! We need another company to compete with Tanesco. Take example of mobile phone; even my grandma in the village out there has a cell phone. Who could have dreamed of that? and the service is great and she can afford it. Think about that.

  4. Naomba kumuuliza Ngeleja a.k.a mzee gizan kweus kwamba’anajua maana ya mega watt na kilo watt kitaalam? Hizo mitambo mara DOWANS na mengineyo yanahusu Tz??? kwel ninauhakika leo Tz tukiamua kuzaliza umeme tunaweza na pesa zipo mifukon mwa viongoz wachache. KWANATUZINGUA

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Send this to a friend