Langa na Kala Pina katika Njia Panda

Wiki chache zilizopita, kupitia CheusiDawaTV, tulipata fursa ya kumsikia Langa akiongelea kipindi kigumu alichopitia — kwa takribani miaka 5, alikuwa anatumia madawa ya kulevya.

Langa ni msanii wa Hip Hop, hivyo sauti yake na ujumbe inaobeba hutua kwenye masikio ya vijana kwa urahisi zaidi. Hivyo, inatia moyo kumsikia akiongelea kwa kina kuhusu “drug addiction”. Wengi wetu hatukujua mtu mwenye “arosto” anakuwa kwenye hali gani — mpaka inafikia hatua ya mtu kufanya mambo ambayo jamii haikutegemea kabisa.

Jumapili ya tarehe 14 Agosti, 2011, Langa na Kala Pina walialikwa kwenye kipindi cha Njia Panda na Dk. Isaac Maro, kujadili matumizi ya madawa ya kulevya na mapambano yaliyomo katika kuyaacha. Pia, waligusia mipango ya baadaye ya kupambana na matumizi ya madawa ya kulevya katika harakati za kuiokoa jamii ya Tanzania.

Sikiliza kilichojadiliwa — mahojiano kwa hisani ya wavuti.com:

Previous ArticleNext Article
Steven was born and raised in Dar es Salaam, and moved to Germany for his studies. He graduated with a BSc. in Physics (Jacobs University Bremen), and then a MSc. in Engineering Physics (Technische Universität München). Steven is currently pursuing a PhD in Physics (growth of coatings/multilayers for next generation lithography reflective optics) in the Netherlands. He’s thinking about starting his own business in a few years; something high-tech related. At Vijana FM, Steven discusses issues critical to youths in Tanzania, music, sport and a host of other angles. He’s also helping Vijana FM with a Swahili translation project.

This post has 1 Comment

1

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Send this to a friend