Sikiliza hoja za aliyeandika mistari ya ‘Bongo Flava’ kwenye mtihani

Kitu ambacho kilibaki kwenye fikra zetu baada ya matokeo ya kidato cha nne kutangazwa mwaka jana, kilikuwa ni kisa cha mwanafunzi ambaye aliandika mistari ya “Bongo Flava” kwenye mtihani. Wengi tulitingisha vichwa, tulisikitika. Wengine tuliamua kujiuliza kwanini taarifa mbaya zinazoashiria sekta ya elimu nchini kuendelea kumomonyoka hazikupewa kipaumbele, badala yake watu waliamua kukebehi kitendo kilichofanywa na mwanafunzi mmoja.

Bahati mbaya au nzuri, Julius Dawson — kijana aliyeandika mistari ya Bongo Flava — alipewa nafasi ya kuongea na umma na kuelezea nini hasa kilimsukuma kufanya kile kitendo. Pia, amejadili kwa kina kuhusu suala la kulea vipaji nchini na mitaala kwenye shule zetu.

Msikilize kwa makini kisha tupe maoni yako:

[audio:http://www.vijana.fm/wp-content/uploads/2012/07/PB.mp3|titles=Julius Dawson akihojiwa katika kipindi cha Power Breakfast (Clouds FM)]

Chanzo na makala nyingine:

Previous ArticleNext Article
Steven was born and raised in Dar es Salaam, and moved to Germany for his studies. He graduated with a BSc. in Physics (Jacobs University Bremen), and then a MSc. in Engineering Physics (Technische Universität München). Steven is currently pursuing a PhD in Physics (growth of coatings/multilayers for next generation lithography reflective optics) in the Netherlands. He’s thinking about starting his own business in a few years; something high-tech related. At Vijana FM, Steven discusses issues critical to youths in Tanzania, music, sport and a host of other angles. He’s also helping Vijana FM with a Swahili translation project.

This post has 10 Comments

10
  1. Wahusika wangekuwa makini wangejiuliza kwa nini aliamua kuandika hiyo mistari ya Bongo Fleva. Badala yake, they made fun of it. They thought it was so funny.

  2. Clouds ruined a perfect opportunity. When does someone like Julius come by radio studios with the guts to say this stuff out loud? Sorry to say but it could have drastically upped their programming if Julius ran some of their shows, especially those shows that are targetting young people. Radio stations should be seeking out youth like Julius and giving them as much time as they need to speak on the mic, not the other way around. Guess this is wishful thinking… for now.

  3. I agree with Jack D. Opportunity wasted. These are the people (Julius) that need to be listened to. Politicians are not experts, but poeple like Julius are in their own right.

    Experts in education need to be involved together with people like Julius, to find solutions to our education system. We pay too much attention to politicians who know very little to nothing ( not all of course)

  4. Wabongo sijui tutaamka lini? Kweli kijana ni jasiri. Wengi wapo kwenye changamoto kama zake lakini hawawezi kuyaongelea mambo yao kwa uwazi kama huyu dogo. Nadhani ameshangaza wengi kwa jinsi alivyoweza kujielezea vizuri mno, kitu ambacho hata viongozi wetu wanashindwa kufanya.

    Hivi zile ripoti za Twaweza na Tamasha Vijana zinafanyiwa kazi kweli… sio kwa upande wa serikali tu, bali hata majumbani mwetu??

  5. Wabongo tuacheni longolongo ……huyu ana miaka 23, ni mtu mzima ambae kwa hali ya kawaida alitakiwa awe anamaliza chuo kikuu, kwa hiyo kumchukulia kama mtoto asiyekuwa na responsibilities sivyo.

    Yeye anasema alitaka asome sanaa au muziki tu, hivi anakusudia kusema hayo masomo mengine huko kwenye shule ya sanaa asisomeshwe au?

    Ningemuelewa zaidi iwapo kwenye somo la Kiswahili kwa mfano, badala ya kuandika mashairi yanayolazimishwa kwenye mtaala, yeye angeandika mashairi ya Bongo Fleva, na sehemu ya insha angeandika historia yake na vitu kama hivyo.

    Lakini kumuendekeza ni kuendekeza kila atakaekataa kusoma shule, akajitia ana kipaji.

  6. Jack D

    Ni kweli hatuna hata moja, lakini kimsingi hatuna hata hizo zinazosomesha masomo ya kawaida…..hazitoshi, na zinapokuwepo hazikidhi haja hata ya elimu ya kawaida tu.

    Katika nchi za nje, wanaosoma masomo ya arts au shule zinazojikita kwenye sports sio kama hawa wanafunzi hawajifunzi na masomo mengine ya kawaida kama hisabati na mengine ya kijamii.

    Kupigania kuanzishwe shule za sanaa hata za baada ya saa za masomo ya kawaida ni jambo la msingi, lakini pia tukemee kwa kijana huyu na wengineo watakaojitokeza baada ya huyu (amini wapo) kwa kutojishughulisha na masomo ya msingi kama hesabati na mengine ya jamii kwa kusema kuwa anakipaji cha muziki.

    Hivi ukiwa mwanasanaa au mwanamichezo huhitaji kujua masomo mengine?

    Nidhamu na good grades zinaweza kukupeleka a long way katika kupata wafadhili hata nje ya nchi maadamu kipaji unacho ukenda kujiendeleza.

    Lazima ujipange kupambana na mazingira yako, ewe kijana. Alivyofanya huyu is not the business

  7. @Hyperkei, nakubaliana na maada unazozitoa hapo juu! Ukweli ni kwamba Elimu yetu ina matatizo mengi na itatuchukua muda si mfupi kuweza kuiweka mahali ambapo itaweza kujenga kipaji cha kila mtoto na kumpa nafasi ya kujishughulisha na kufanya ambayo yana mvuto wa asili kwake.

    Lakini kabla hatujafika hapo, nafikiri waliopo mashuleni inabidi wachukue hicho kidogo kinachotolewa na mfumo wa sasa na kuangalia namna ya kuweza kukitumia kwa manufaa yao katika jamii! Nimesikia huo wimbo wa kijana Julius na nafikiri ana kipaji kinachoweza kumpa kipato kama kikiendelezwa na jamii kukubali sanaa yake. Lakini imani yake na vijana wengi nchini kwamba elimu na sanaa ni vitu viwili tofauti ni potovu na inabidi watu waache kuiendeleza. Kama unataka kuwa msaani tuseme wa Bongo Flava ama kuigiza, ningetegemea kwamba utakuwa na udadisi fulani juu ya lugha iwe kiswahili ama kingereza na kwamba hilo litaonekana katika matokeo yako ya mithihani katika fani hizi.

    Pia nakumbuka tulifundishwa kwamba sanaa ni kioo ya cha jamii, na unapozungumzia jamii, kielimu moja kwa moja unagusia mambo kama historia, elimu ya siasa, uchumi na mengine mengi na kama msanii anayetafuta mali ghafi ya sanaa yake, nigependa kuonga una uelevu wa kutosha wa mambo haya.

    Kwa hiyo suala la kusema kwamba elimu yetu ni mbovu kwa hiyo hamna haja ya kuitilia maanani na kwamba ukombozi upo kwenye sanaa ya Bongo Flava, halina msingi na lisiwe sababu ya watu kutosoma! Matokeo ya mawazo kama haya ni kwamba jamii huona sanaa kama fani ya walioshindwa na elimu na hii si ukweli lakini maadam jamii inaliona hivi kutaendelea kuwa na vikwazo na ushawishi finyu wa sanaa hii katika jamii kwa ujumla!

  8. tunahitaji kuwa wanafilosofia katika kulijadili hili jambo la huyu kijana..tunahitaji kufikiri kwa kina juu ya kilichotokea japo najua kutaibua mkanganyiko zaidi kwa utofauti wa malezi na mazingira ambayo tumekulia na kusomea. je mazingira yanampatia fursa gani kijana wa leo anaekulia kwenye lundo la changamoto.?swala hapa si elimu pekee.labda wewe umebahatika kuwa na jirani aliyesoma na akapata nafasi ya kufanya atakalo lakini kuna maelfu ya waliosoma na bado wanahangaikia ajira na walikuwa na vipaji ambavyo havikupewa fursa ya kuchanua..kwa nini havikupewa fursa? jibu kila mmoja wetu analo..lakini labda kubwa kuliko hayo majibu ni kukosa kujitambua wewe ni mtu wa aina gani..unakipaji gani. Tunahitaji busara sana kuchambua swala hili..mim naliona kama kisa mkasa kinachohitaji upembuzi yakinifu juu ya mfumo mzima wa elimu yetu..
    Mimi si mpi hongera kwa alichokifanya, ila nampa hongera kwa kujitambua kuwa yeye anaweza kufanya nini. kwani kuna wengi ambao kamaliza nao na walifanya mitihani yao kwa nidhamu kuu na hadi sasa hawajijui wao ni kina nani..Lazima tukubali hii leo ya kuwa, makubwa na yakushangaza duniani yamefanywa na watu wa aina ya kijana huyu..hawa wao wanakaa katika kundi la wabunifu na utekelezaji halafu wengine wanachukua kutoka kwao na kukiendeleza.Sifurahishwi na alichokifanya ila ameibua mgongano wa kina wa mawazo na changamoto kwa kila mhusika..mwananchi na serikali yake.Tunahitaji kujitazama upya.

  9. utaalamu mwingine sio lazima watoke nje!! Unaweza tukaanzisha taaluma hizo kwa kubuni au kuiga au kuboresha…!!

    wataalamu wa music wanasemaje kuhusu huyo kijana!!
    waalimu,police,wanasiasa, jamii kwa ujumla…Mwisho tutajua plani ilikua ni nini!!…
    je future yake ikoje!!….
    Lakini kua Msanii sio kwamba una haki zaidi ya watu wengine…!!?

    alifanya hivyo kuonyesha kipaji chake?
    ipo siku vijana wata toa taarifa muhimu kwa serikali kupitia mitihani!!…

    Taarifa za mauaji…!! kwa upelelezi!!

    kabla hamja wa anika adhalani…ongeeni nao mtambue matatizo yao!! baada ya hapo wapewe mtiani mingine!!

Leave a Reply to Anonymous Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Send this to a friend