Dhuluma za Kimapenzi, Migori, Kenya

[audio:http://www.vijana.fm/wp-content/uploads/2013/02/Jinamizi-Migori-Arnold-Ageta.mp3|titles=Arnold Ageta – Jinamizi Migori]

Dhuluma za kimapenzi kwa wasichana limekuwa ni jambo la kushughulikiwa kwa dharura humu nchini. Kaunti ya Migori ni moja ya maeneo ya humu nchini ambamo visa hivyo vimekuwa vikirekodiwa kwa idadi kubwa.

INSERT 1: Girl on how she was defiled.

Huyo mtu alinipata karibu na njia akaniuliza hiyo maneno nikamwambia sitaki hiyo maneno akaniambia nitakupiga mpaka utafanya…akanibeba kwa mahindi akaniambia nikipiga nduru atanipiga…akishafanya hivyo halafu akaenda.

Msichana huyu wa miaka kumi na tatu ni mwathiriwa wa ubakaji. Kwa sababu hizo, nitabana jina lake. Nitamwita Mary ambalo si jina lake halisi.

SFX: Fade up sound of wheel chair squeaking and screeching then fade under to introduce presenter.

Maisha ya Mary yamekuwa yakizunguka juu au karibu na kiti chake cha magurudumu ambacho kimezeeka na kuchakaa.

SFX: Fade up sound of wheel chair squeaking and screeching then fade under to introduce presenter.

Mary hana miguu, hana mikono. Mama yake ni mjane na tena ni mgonjwa. La kushangaza ni kwamba mwanaume aliyembaka bado hajakamatwa.

INSERT 2: Mary’s mom on report to administration.

Chifu aliniita akaniambia tufanye namna hii twende Migori tuandikishe statement lakini hiyo siku alinijifichia, sikumwona, wakati ngine akarudi akachukua picha ya mototo akaenda tu pole akanyamaza tu. Ndio mzee mwingine akachukua hatua akanileta hapa Migori tukaandikisha statement… nimefuatilia lakini chifu alimficha…sasa ningekuwa na uwezo…ningee.

SFX: Sound to mark tension.

Miezi minne baada ya kitendo hicho cha ubakaji.

INSERT 3: Mom on the defilement and pregnancy.

Ilikuwa naona iko na uchokezi mingi anachoka tu mara kwa mara analala nikampima tu polepole nikamwangalia nikamwuliza mbona unachokanga tu namna hiyo? Hata sura naona imegeuka?

Mary ni mjamzito.

SFX: Sound of news over the radio on Mary’s pregnancy.

Msichana wa miaka kumi na mitatu asiye na mikono wala miguu aliyepachikwa mimba baada ya kubakwa wilayani Migori ameshangaza wengi baada ya kujifungua motto wa kiume usiku wa kuamkia leo. Hata hivyo msichana huyo angali anangojea mkono wa sheria kumtia mbaroni mwanume aliyemfanyia unyama huo.

Bwana Fredrick Lai ni afisa mkuu wa polisi wilayani Migori. Nilimwuliza ni kwa nini mshukiwa wa kesi hiyo hajashikwa?

INSERT 5: OCPD Migori on the case. Voice over.

It came to us immediately after it was reported in the media. We took action, we went to the scene and unfortunately the suspect had already got information about the issue before the police. And in that situation, the suspect disappeared.

Voice over: (Tulipata habari hizo kwa vyombo vya habari kabla ya taarifa kufikia polisi. Tulichukua hatua na kufika kwenye eneo latukio. Katika hali hiyo, mshukiwa alitoroka kabla yetu kumfikia.)

Ni kweli kesi hiyo iliripotiwa mapema?

I have gone through all our records. I have confirmed that that incident was not actually reported to our station

Voice over: (Nimepitia rekodi zetu zote na nimebainisha kuwa ripoti hiyo haikurekodiwa kwetu)

Je mkuu wa wilaya ya Migori bwana Julius Mutula anajua ukweli?

INSERT 6: DC Migori on report of the case to police. Voice over.

It was only reported to the police and it was recorded in OB. It’s a defilement case but it has not gone to court because initially the mother went to the home of the boy’s, they wanted to reach some kind of an agreement.

Voice over: (Hiyo kesi iliripotiwa na kurekodiwa kwa polisikama kesi ya ubakaji lakini haijaenda kortini kwa sababu hapo mwanzoni kulikuwa na jaribio la mama ya msichana kumaliza hii kesi nje ya korti pamoja na wazazi wa mshukiwa).

Mama ya Mary pia atalaumiwa kwa kujaribu kuharibu kesi hiyo?

INSERT 7: Mom on effort to reach the man.

Huyo mtu hatukuelewana na yeye…kwa sababu nilienda nyumbani kwake nikadhani atakuja kwangu sikuona yeye mpaka wakati huu…tuongee na yeye aone vile atanifanya.

SOUND TO MARK TRANSITION.

SFX: Children singing song on prayer to God to help them defeat the devil.

Mungu nisaidie na uwezo wa kupigana na shetani…hayo ndiyo maneno ya wimbo wa watoto hawa kutoka shule anakosomea Mary.

SFX: Children singing song on prayer to God to help them defeat the devil…
Unyanyasaji wa wasichana wa umri mdogo kimapenzi pamoja na ndoa za mapema umekuwa ni shetani la majinamizi katika maeneo haya ya Nyanza kusini.

Msichana huyu yatima naye ni mwathiriwa wa ndoa ya mapema.

INSERT 8: Girl 2 and mother 2 on her story on early marriage.

Yeye akanipatia one hundred akaniambia nimtafutie change nimpelekee. Akaniambia niko na brother yangu nataka kukupatia. Nikamwambia mimi sitaki mtu mimi bado naenda shuleni. Akaniambia shule haina maana. Kuna wenye wamesoma hata college hawajafaidika… yeye akaniambia utakuja tu jioni akaniambia utakuja kama umefunga shuka hivi ndiyo mtu asikujue.

Tulikuwa jioni kitu saa moja na nusu sasa tulikuwa tumekaa tu hapo nje na tukapata ametoka nikaenda kwa huyo mama umesikia anakuambia alitokea kwake. Nikamwuliza huyo mama,ni jirani tu, akaniambia huyo mtoto sijamwona. Huyo motto ni mdogo, siwezi kumwongoza mtoto mdogo. Si anazaliwa kama tunaona.

Bado hakuna hatua yoyote ambayo imechukuliwa baada ya msichana huyo kuokolewa kutoka kwa ndoa ya mapema.

SFX: Children singing a song. Play under then out.

Visa kumi tu Kati ya visa mia moja vya unyanyasaji wa kimapenzi kwa wasichana ndivyo huripotiwa humu nchini kwa mujibu wa shirika la kimataifa linaloshughulikia watoto la Unicef. Ni jambo linalohitaji kushughulikiwa kwa dharura. Bi Cecilia Okoth ni afisa wa kujitolea wa watoto Katika eneo la Migori.

INSERT 9: Cecilia Okoth on problems. Voice over.

We have a lot of problems with children especially the girl child…because of the negative practices of our culture. We have advocacy but we are handicapped. We don’t have means to reach out immediately for cases.

(Tuna shida nyingi za watoto haswa kwa mtoto msichana. Ni sababu ya mila duni. Tunawajibika lakini uwezo wetu ni mdogo wa kufikia kwa haraka visa vinavyoripotiwa)

SFX: Man singing in village then fade under presenter.

Wanaume ndio wamehusishwa pakubwa na visa vya ubakaji na unyanyasaji wa watoto kimapenzi.

SFX: Man singing in village then fade under presenter then out.

Kesi nyingi zinazohusu watoto hufutiliwa mbali kwa sababu ya kukosekana kwa mashahidi.
Nilifuatilia kesi nambari mia tatu na nane ya mwaka elfu mbili na tisa katika mahakama ya migori, korti nambari moja kwenye kaunti ya migori.

Wanaume wawili walikuwa wameshtakiwa kwa kosa la kumweka msichana wa miaka kumi na miwili katika hali ya ndoa na vilevile kumnyanyasa kimapenzi. Kesi hiyo ilichukua takribani mwaka mmoja na nusu kukamilika. Washukiwa hao wawili waliachiliwa huru. Kesi yenyewe ilitupiliwa mbali. Kulingana na hakimu Kibet Sambu ailiyeamua kesi hiyo, mashahidi wa upande wa mashtaka walikosa kuhudhuria vikao vya korti ili kutoa ushahidi kuhusu kesi hiyo. Shida iko wapi?

INSERT 10: DC Migori on defilement cases. Voice over.

The problem we are having you find a child has been defiled and the parents entered into some funny arrangements with the culprits and then they end up defeating justice in court. People are prevailed upon to desist from going to give evidence in court. Several cases have been concluded in a very funny way because of the collusion of the parents and the culprits.

Voice over: (Shida ni kwamba msichana akibakwa, wazazi huanza kufanya mpango wa maelewano ya nje ya korti na washukiwa. Mashahidi hufisidiwa wasiende kutoa ushahidi kwa kesi kama hizo. Hii hukatiza mkondo wa sheria na haki. Ni kesi nyingi zimefutiliwa mbali kwa njia kama hizo.)

Huyo ni bwana Julius Mutula ambaye ni mtawala wa kimkoa. Viongozi kama yeye wamewajibikaje kwa tatizo hili?

INSERT 11: DC Migori on strategy. Voice over.

We are approaching the issue through public barazas public forums, we have been talking with our people and we have been also encouraging our people to desist from the practice of defiling ,raping young children and we have also been cautioning parents from the habit of you know entering into some kind of arrangements after a child has been defiled or raped.

Voice over: (Tumekuwa tukihamasisha wananchi kupitia kwa baraza za vijijini na makongamano ya umma kuhusu haja ya kupiga vita ubakaji na dhuluma nyingine kwa watoto. Pia tunaonya wazazi wasijaribu kutatua kesi hizo nje ya korti watoto wakibakwa)
Kwa Mary, maisha yanaendelea japo kwa shida. Nilikutana naye akiruhusiwa katika chumba cha kina mama wanaokaribia kujifungua katika hospitali ya wilaya ya Migori.

Nimekuja ku… ku… kujifungulia hapa… nimekuja hapa wanipime.

SFX: Children reciting a poem on neglect.

INSERT 12: Mom on desperation.

Mtoto yangu nilikuwa nataka asome. Kwa maana mi sina uwezo sina uwezo wowote hata mimi ni mgonjwa nilikumbuka alikuwa atasoma halafu akuje kunisaidia baadaye kwa maana yake baba yake amekufa sasa naona mtu amemtenda kitendo kama hicho nimesikia huzuni sana.

SFX: Sound of newborn child crying.

Wiki mbili baadaye, Mary alijifungua.

Nilijifungua jana saa kumi na mbili…nimezaa, ni kijana, ni kilema…mguu.

SFX: Sound of newborn child crying.

Insert 13: Mary and her mum on delivery.

Mimi huyu mtoto wangu wakati alikuwa mjamzito nilikuwa na huzuni nilikuwa ninafikiria huyu mtoto tajifunguaje,alikuwa hata hawezi kutembea, amechoka tu shida iko nayo ananiambia mama mimi nasikia uzito sasa nitajifanyaje sasa wanansema watanipeleka kwa kisu. Nita…sasa si nitakufa? Nikamwambia huwezi kufa, utakuwa tu mzima. Lakini mabo ya Mungu ni mengi Mungu amemsaidia amejifungua kwa sasa mimi niko na furaha.

Nilikuwa nimeogopa tu kidogo.

Ombi kuu la Mary kwa serikai ni moja.

INSERT 14: Inisomezee watoto wetu, hata mimi pia nisome.

SFX: Children reciting poem.

Ni mwezi mmoja sasa tangu ajifungue. Mama na mtoto wote wangali buheri wa afya. Mama yake anazidi kushughulika angalau mwana na mjukuu wale, walale kwa hali ngumu aliyo nayo.

INSERT 15: Mary’s mom on daughter’s motherhood.

Vile mtoto kama atanyonya inatakiwa mtu awe karibu. akiwa peke yake hawezi. Nafanya kazi kidogokidogo ya kulima hii na kushughulikia watoto vile watakula.

Mary angali amezama katika lindi la unyanyaswaji wa kimapenzi. Je atauona mkono wa haki?

Insert 16: OCPD Migori on follow ups. Voice over.

We may not have circumstantial evidence to prove this case for now. But now that we have a by-product of what is alleged to have happened, with the advance in technology, if the suspect is arrested, we can be able to link the suspect with the child who has been borne through DNA testing and things like that.

Voice over: (Kwa sasa hatuna ushahidi wa kutosha. Lakini kwa sababu tuna motto ambaye amezaliwa kutokana na kitendo kinachodaiwa kutokea, tutatumia teknolojia ya DNAau mbinu nyinginezo kumhusisha mshukiwa na kitendo hicho).

SFX: Children singing song on prayer to God to help them defeat the devil.

Ni miezi kumi na moja sasa. Mary bado anangojea haki kutendeka. Atasubiri hadi lini?

SFX: Children reciting poem.

Visa vingine vingi vya dhuluma za kimapenzi kwa wasichana wa umri mdogo vinaendelea kuripotiwa. Je katiba mpya itaongeza makali kwa vita dhidi ya jinamizi hili?

Nikiripotia Radio Kisima kutoka katika kaunti ya Migori, mimi ni Arnold Ageta.

Previous ArticleNext Article
Born and raised in Western Kenya, Arnold studied Journalism and Public Relations. He has worked in both radio and TV and is a CBA-One World Media 2011 award winner for the best program produced in a developing country. Arnold has excellent audio visual production skills; he worked for Hope Channel TV and now works for Radio Kisima FM as Head of Programs. He also owns a TV production house, Argertta Communications. Arnold seeks to write and produce youth-related stories on various issues for Vijana FM. Radio/TV features are his specialization.

This post has 1 Comment

1

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Send this to a friend