Kibera – Slum survivors

Wiki kama tano zilizopita Kamau alianzisha mjadala motomoto kwenye blog ya Michuzi ambao tunajua jinsi ulivyotokomea. Sijui kama wengi wetu tuliokuwa tunaufuatilia tulijifunza lolote la maana ili kuhakikisha mambo kama yale yanachambuliwa kwa kina; kwasababu labda kuna uwezekano wewe msomaji, kijana, utakuwa mmoja wa viongozi hapo baadae na tusingependa maamuzi kama yale yajirudie!

Kama una kumbukumbu nzuri, nadhani utakiri kwamba neno au jina “Kibera” lilikuwa likitumiwa kama silaha ya kumnyamazisha Kamau (kama una muda, hesabu Kibera ilitajwa mara ngapi kwenye maoni).

Hivi watu wale walikuwa na haki ya kutumia Kibera kumnyamazisha Kamau? Je, wana picha halisi ya mambo yanayotokea Kibera? Wanadhani yanayotokea Kibera hayatokei Tanzania au nchi nyingine yoyote masikini? Ukubwa na idadi ya watu wanaoishi Kibera ndio inatufumba macho; kutufanya tusahau yanayojiri Mbagala, Tandale, Tandika, Unga Limited na vijiji vingi Tanzania?

Swali la msingi ni hili: Matatizo au mambo tunayoyaona Kibera na sehemu nyingine duniani tunadhani sio matatizo yetu?

Sikiliza hekima na busara za mwalimu mmoja anayeishi Kibera (mwishoni mwa filamu):

Warning: Extremely explicit graphic content between 1:00 and 2:00. Onyo: Picha zinazooneshwa kwenye dakika ya 1:00 na 2:00 zinahitaji moyo mgumu kuziangalia.

Previous ArticleNext Article
Steven was born and raised in Dar es Salaam, and moved to Germany for his studies. He graduated with a BSc. in Physics (Jacobs University Bremen), and then a MSc. in Engineering Physics (Technische Universität München). Steven is currently pursuing a PhD in Physics (growth of coatings/multilayers for next generation lithography reflective optics) in the Netherlands. He’s thinking about starting his own business in a few years; something high-tech related. At Vijana FM, Steven discusses issues critical to youths in Tanzania, music, sport and a host of other angles. He’s also helping Vijana FM with a Swahili translation project.

This post has 4 Comments

4
  1. Labda tujiulize kwanza: Kwanini tunaacha hivi vitu vinaendelea? Walioko madarakani na sisi watu wakawaida, tunaweza kufanya lolote?

  2. Hii docu inasikitisha sana. Nimeguswa na ile sehemu wanaposema kuwa ‘if the upper class think the problem is not theirs, then they have to re-think because eventually it will knock at their doors’ or something. Such inequality cannot continue indefinately because sooner or later the slum dwellers will say ‘enough is enough’ and start a soft or even brutal revolution. I mean, Kibera is in Nairobi – wakiamua kuanzisha vagi mji mzima patakalika kweli?

    Dar tuna Tandale, na Manzese ambapo wengi wa wananchi wanaishi katika jiji bila maji safi, sewage system, uwepo wa zahanati nk. Hatuwezi kuruhusu hali hii kuendelea. Wewe kama kijana (wa O’bay, Upanga, Mikocheni) ukidhani tatizo hili sio lako, kijana wa Tandale haoni shida kupiga mguu kutoka Tandale kwenda Sinza-Kijitonyama-Msasani- na kufika Ostabei ili kuanzisha vagi. What does he/she loose anyway?

    La maana ni hawa wanaoishi katika sehemu hizo kutafuta legitimate political representative tu. Handouts kutoka kwa wahisani hazitoshi – since it creates the dependency cycle we are all familiar with. Wakiwa na representative anayeishi humo humo kwenye slum ndipo anaweza wakawa na ‘hope’ fulani.

    Pia, ni juhudi binafsi ya baadhi yetu tuliobahatika kupata ka’elimu kujitolea na kufanya jitihada kama za yule mwalimu wa kujitolea katika clip. Tunaweza kuchangisha na kuanzisha shule kama hizo, au kusaidia katika ‘campaign’ za kuhamasisha watu wasiendekeze kutupa taka hovyo, au kuhamasisha dhidi ya magonjwa ya ukimwi n.k. Hii haihitaji pesa, bali muda wako tu – jiji la Dar au Nairobi lina vijana wasomi wangapi? Wanafunzi wa chuo kikuu je – kwanini hawahusiki?

    Eventually, we will need to improve the conditions of people’s livelihood in such slums so as to start another wave of mass ’emigration’ from such slums. Because, I believe it will be hard to sustain improved living standards in such a crowded setting. Watu wapate nafuu, waondoke, mahala ilipokuwepo slum, pabomolewe itengenezwe public facility – kama park or whatever.

    my Monday rant

  3. hii inasikitisha, halafu Nairobi mnaita half london!!!!!
    hivi hawa viongozi wanatuchukuliaje?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Send this to a friend