Waraka wa wazi kwa Nakaaya

Makao Makuu,

Chama cha Vijana Waliochoka (TZ),

Dar es Salaam.

CCVW-TZ/Tawi Na. 1/WRK – 01/170910                                          Ijumaa, Septemba 17, 2010.

Ni muhimu kuweka picha yako kwenye waraka kama huu ili kuvutia vijana.

Tawi la Arusha Mjini

CCM/CHADEMA (Usisahau kufuta isiyostahili!)

Tanzania

Bi. Nakaaya Sumari,

YAH: CHAMA CHA VIJANA WALIOCHOKA (TZ)

Tumekuwa tukiangalia kwa makini mwelekeo wa Vijana Tanzania kwa kipindi kirefu. Baada ya tathmini ya kina iliyofanywa na Vijana wachache sana walioamka, tumeona ni wajibu wetu kuanzisha Chama cha Vijana Waliochoka (Tanzania) ili kufanya mapinduzi ya kweli nchini. Nia hasa ni kuhamasisha Vijana kufuatilia siasa kwa “makini” na “kushiriki kikamilifu” ili kuleta mabadiliko yatakayodumu kwa zaidi ya vizazi viwili vijavyo.

Ila tumegundua kuwa siasa ya Tanzania — hasa kwa upande wa Vijana — imetawaliwa na ushabiki tu. Madhumuni yetu hasa ni kuwatumia watu maarufu kama nyie kuwasihi Vijana angalau watutegee masikio.

Bahati mbaya au nzuri, hatuwezi kukuahidi kiti maalumu Bungeni kwasababu ndio kwanza Chama chetu kiko kwenye mchakato wa kuandika Katiba. Baada ya hapo tutakuwa tunafanya utafiti wa kina ili kuona sehemu ambazo zinahitaji mabadiliko kwenye utendaji wa Serikali ya Tanzania kwa ujumla. Kisha tutaandika ilani kwa ajili ya ushiriki wetu kwenye Uchaguzi Mkuu mwaka 2020.

Kauli mbiu ya Chama ni hii: Tunaamini walioko juu wananing’inia kama tone la kamasi — kama hawadondoki, sisi tutahakikisha wanapengwa!

Ukiacha “mvuto” wako, tuna uhakika utatuletea mbinu za kuviangusha vyama vinavyotikisa nchi sasa hivi kwasababu unazijua vizuri na kwa kina katiba za CCM na CHADEMA. Pia, tuna matumaini kuwa umezipitia ilani za Uchaguzi za vyama husika (CCM na CHADEMA).

Mimi kama Katibu Mkuu wa Chama cha Vijana Waliochoka nina uhakika utakubali mwaliko wetu kwa moyo mkunjufu. Tafadhali, soma makala ifuatayo (Vijana wa Tanzania Tuamke!) ili kurahisisha shughuli za usahili.

Wako mtiifu,

Toto Tundu.

Katibu Mkuu,

Chama cha Vijana Waliochoka (TZ).

Previous ArticleNext Article
Steven was born and raised in Dar es Salaam, and moved to Germany for his studies. He graduated with a BSc. in Physics (Jacobs University Bremen), and then a MSc. in Engineering Physics (Technische Universität München). Steven is currently pursuing a PhD in Physics (growth of coatings/multilayers for next generation lithography reflective optics) in the Netherlands. He’s thinking about starting his own business in a few years; something high-tech related. At Vijana FM, Steven discusses issues critical to youths in Tanzania, music, sport and a host of other angles. He’s also helping Vijana FM with a Swahili translation project.

This post has 9 Comments

9
  1. safi sana, ila Nakaaya ni mfano wa watu wanaotafuta madaraka na sifa kwa gharama za siasa. Hata hivyo huyu ni mtu mdogo sana kumjadili… tuangalie ya maana

  2. vijana wengi tumekuwa si watendaji wa yale tunayoyasema.

    Wengi ni wakosoaji wazuri wa mifumo iliyopo lakini baadae tunaendelea kuikumbatia mifumo hiyo hiyo sijui ni kwa ukosefu wa ujasiri au ukosefu wa mbadala.

    vijana hasa maarufu wako katika nafasi nzuri ya kutetea kile mnyonge anashindwa kukiwakilisha kwa jamii lakini inasikitisha kuona ni vijana wachache mno wanaoweza kusimamia uetetezi au misimamo yao kwa muda mrefu.

    kubadili vyama sio kitu kigeni duniani, lakini angetutendea haki vijana kwa kutuambia kwa vielelezo vya ushahidi kilichomfanya kuhama chama kimoja kuingia chengine kwenye wakati huu wa kampeni.

    nataraji amejiandaa kufanya hivyo

  3. hatuwezi kupoteza muda mwingi kumpa sifa Nakaaya, ni mtu wa kawaida tu kama vile ambavyo watu wengi wamehama vyama. itakuwa yeye tu, mbona mpendazoe freddy aliacha ubunge na kuingia chama ambacho hata hakijasajiliwa thoo kwa sasa yupo Chadema

  4. Kwanza nianze kwa kurekebisha jina la chama,kukiita chama cha vijana waliochoka ni kutuzalilisha sisi vijana,sasa kama tumeshachoka that means hatuwezi tena kuleta mabadiliko,hilo jina hatutaki hata kulisikia,tuitwe chama cha vijana wanaotaka mabadiliko.Huyo nakaaya sio lolote wala chochote anatafuta umaarufu kupitia siasa,uwezo hana wala nini namshauri akae hukohuko kwenye mziki siasa haziwezi.Hao ndio wale kama popo sio ndege wala mnyama leo chadema kesho anadanganyika ccm,huyo hafai kuwa mpigania haki.

  5. Sikutegemea barua kama hii itahitaji “kutafsiriwa”… Hata ile hadithi ya mbayuwayu nayo ilitafsiriwa?

    Nitaishia hapa… Walioilewa barua fikisheni ujumbe. Hii sio kwa Nakaaya tu (ingawa yeye ni easy target sasa hivi), lakini hii siasa ya Tanzania imekuwa kama mchezo wa kuigiza na kuna baadhi ya watu ‘wamechoka’.

  6. @Toto Tundu, hahahah, kweli wewe ni mtundu….Ooh Nakaaya, sijui nianze wapi. Sasa sijui alikuwa anasoma ilani/ sera za CCM kisirisiri alipokuwa Chadema, au kahamia tu CCM bila kujua itikadi zao, ilimradi tu siku imepita.

    Mimi nasema hivi, dada Nakaaya kama utasoma huu mchango wangu, ni hivi. Kuhama chama ni haki ya kila Mtanzania, wewe ukiwa mmoja wapo. Hata ukitaka uanzishe chama chako, na ukasema akina baba na akina kaka marufuku, sidhani kama kutakua na pingamizi kubwa, si kuna shule za jinsia moja tu, hivyo uamuzi huo hautakuwa kitu kipya wala wa ajabu. Lakini utata au uchokaji wa wengi ni hapa..

    (hii ni kama ulihamia bila kusoma sera/ ilani za CCM, lakini kama ulisoma na kuzielewa na kukubaliana nazo na kuridhishwa na utekelezwaji wa sera hizo, basi tupilia mbali yafuatuayo, lakini kama hukusoma basi naomba niendelee…)

    Wengi tulikuona kama mtu mwenye msimamo, na mwenye dira fulani, hivyo kuwa kama mboni ya jicho letu sisi vijana, au tunaweza kusema, “idol” wetu. Lakini nadhani kuna wengi wetu ambao hatukuegemea na wewe ungehama tu chama ghafla, na kuhamia chama kile ambacho umekuwa ukikisema siku si nyingi zilizopita. Kwa kuwa sisi wengi tulikuweka kwenye fungu tofauti na wanasiasa wengine ambao hupenda madaraka, wabinafsi, bendera fuata upepo “opportunist”, wasio na msimamo, au wasio kuwa tayari kusimama na kupigania msimamo wao. Hivyo kitendo chako cha kuhama, kimetuacha wengi na kiulizo cha, je, tulikosea kukuweka wewe kwenye fungu lile tofauti na hao nilio wataja hapo juu, na kama ni hivyo, wengi tunajiona wajinga kwa kudanganyika kama watoto wadogo, tukifikiria wewe si kama akina wale.

    Lakini hata hivyo, unaweza kuleta maendeleo kwa wananchi kupitia CCM, huo ni ukweli usiopingika, na labda utafanya hivyo. Utapigana mpaka zahanati zijengwe, na akina mama wajawazito wajifungue salama na kila mmoja kulala katika kitanda chake peke yake.

    Lakini pamoja na hilo linawezekana, nadhani credibility yako kwetu sisi umeyumba, imani yetu kwako imepata nyufa. Kumbuka, Gandhi alilala chini na kupigwa na wenzake akigombania uhuru. MLK na wenzake walipigwa na kung’atwa na mbwa wa polisi wabaguzi, leo hii watu weusi waishi kwa haki na usawa, list ni ndefu. Je, watu wote hao wangekimbia na kusema, if you cant beat them join them, tena kumbuka kuwa, wao walikuwa na kazi kubwa kuzidi matatizo ambayo tunapambana nayo sisi. Kwani wewe hujawahi kupigwa ukitetea imani yako. Hivyo kukimbia tu CCM, imetushangaza wengi, ni kama ume-bail out wakati ndio kwanza safari imeanza.

    Hauwezi kufika, kama kila gari linapojiandaa kuanza safari basi tairi linachomoka, halafu kesho tunalalamika, jamani gari hili halitufikishi popote. Sasa kama matariri nyie ndio mnafanya mambo ya “Uyuda”, sasa mnategemea nini, kama sio kufanya safari iwe ndefu zaidi na hata kuonekana kuwa haiwezekana. Jamani, acheni ujinga, kama watu walikuwa walinyongwa kwenye miti (slavery/ lynched) na leo ndio hao wameshika nchi, tushindwe sisi ambao kazi kubwa tuliyonayo siyo kupambana na mtu mwingine, bali ujinga wetu sisi wenyewe.

    Kama nilivyosema, nasubiri remix ya Mr. Politician, iitwe Ms. Politician, manake sasa hivi taswira ninayopata nikisikiliza Mr. Politician ni tofauti kabisa, I guess kweli tungo ile ilikuwa ni fasihi haswaa. Manake, ulitubwaga tukifikiria ni hadithi kuhusu wengine, hivyo tutupie macho wengine, kumbe kikulacho ukingoni mwako…hahah…

    Remember, “That who dont stand for something, will fall for anyhting”

  7. I thought this lady was somebody but now akili yangu inaniambia she is nothing.. Lets just dont waste our time. Tuendelee tusikatishwe tamaa na hawa popo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Send this to a friend