Ijumaa moja nilikuwa nimetulia tu nyumbani kama kawaida nikisoma Robbo blog, kufuatilia matukio mbalimbali na kujiandaa na mechi zilizokuwa zinafuata kwenye Ligi Kuu ya Uingereza. Kwangu hiyo ni burudani tosha baada ya pilika pilika za wiki nzima kwenye maabara.
Rafiki yangu akanitumia ‘link’ ya website ambayo ilikuwa ina film ‘Shuga’, iliyotengenezwa Kenya kwa hisani ya kampeni ya MTV’s Staying Alive. Aliniambia tu, ‘Hii ni kali!’ Kama kawaida yangu nilisita kidogo; yaani niache kusoma Robbo blog halafu niangalie kitu ambacho nimekuwa nikikisikia tokea 1996 (elimu kuhusu Virusi vya Ukimwi/Ukimwi)?
Kabla ya kulala nikaamua kubofya ile ‘link’, kuangalia kilichopo huku nikiuvuta usingizi taratibu. Nilikuwa nimechoka lakini baada ya kuangalia film kwa dakika kadhaa usingizi ulitokomea. Nikaiangalia kwa makini film nzima na ujumbe nikaupata. Ni film ya zamani kidogo lakini ujumbe wake unamgusa kila kijana, hasa wale ambao wako vyuoni.
Ukiacha ujumbe uliokusudiwa kuna mambo mengine mengi ambayo yatakufumbua macho. Wale ambao wana ndoto au mipango ya kuingia kwenye fani ya utengenezaji, uongozaji wa kurekodi, uigizaji na pia utangazaji wa film nadhani watajifunza vitu viwili vitatu.
Ni film ya zamani kidogo na watu wengi labda wameshaiona, lakini nimeona sio vibaya kuianika tena na kuwapa ukumbi Vijana kuijadili.
Shuga Episode 1 from mtv staying alive on Vimeo.
Shuga Episode 2 from mtv staying alive on Vimeo.
Shuga Episode 3 from mtv staying alive on Vimeo.