Ukubwa wa Pua Ndio Wingi Wa Kamasi..??

Mkutano wa Kili Music Awards uliofanyika majuma kadhaa yaliyopita ulitoa nafasi nzuri kwa wasanii kutoa maoni na madukuduku yao juu ya tuzo hizo. Wasanii wa bongo flava walikuwa na mengi ya kuchangia, wengi walijaribu kuweka bayana mapungufu ya tuzo hizo, na kutoa ushauri wa nini kifanyike kuboresha tuzo hizo. Mimi binafsi nilichukua nafasi hiyo kuangalia upeo wa wasanii wa bongoflava, kwani ukitaka kujua mdogo wa mtu unanuka sharti usubiri azungumze. Mambo mengi yaliyojadiliwa lakini kuna baadhi yalinikaa akilini. Baadhi ya mambo hayo yalikuwa ni swala zima la Tanzania kuwa na tuzo chache za kutunza wasanii wetu, pili, utaratibu wa top ten za radio station nyingi kutokueleweka zinapatikanaje, tatu, swala la radio DJ kuwa mameneja wa wanamziki kwani kuna hatari ya hao ma-Dj’s kuleta upendeleo kwa wasanii wao n.k.

T.I.D alikuwa msanii miongoni mwa wengi waliotoa dukuduku lao na tuzo hizo za Kili Music Awards. Mwamziki huyo wa Top Band alionyesha wazi kutoridhishwa kwa kutopewa tuzo ukilinganisha na ukongwe wake katika mziki wa bongo flava na vibao vyake vingi vilivyowahi kushika chati, kwa mfano nyimbo yake ya zeze. Maneno ya T.I.D hayakuwa ya mzaha, kwani majuzi alitangaza na kusema “siwezi shiriki”, akiwa anamaanisha amejitoa kwenye kinyang’anyiro cha tuzo hizo za Kili. Mimi binafsi nilishtushwa na uwamuzi huo wa T.I.D kwani sikuelewa kama kuzigomea tuzo hizo ndio njia ya kuzisukuma kumpatia tuzo au alikuwa na nia gani hasa hasa na maamuzi hayo. Baada ya wiki kadhaa toka T.I.D alipotangaza kujitoa, msanii Dully Sykes na yeye alitangaza kujitoa kwenye tuzo hizo, na yeye akiwa na sababu zinazofanana na sababu za T.I.D.

T.I.D na Dully Sykes ni wasanii wawili wakongwe katika mziki wa bongo flava, hivyo kujitoa kwao kunaacha viulizo. Mimi nimeachwa nikijiuliza, inawezekana maamuzi yao yamekuwa ya kukurupuka zaidi au kweli kuna matatizo ya kimsingi katika tuzo hizo za Kili. Je kujitoa kwao kutasaidia kukuza mziki wa bongo flava au utayumbisha mtazamo juu ya mziki huu na wasanii wahusika katika sanaa hii.

Mtazamo wangu katika swala hili ni huu, kama akina T.I.D na Dully Sykes wana hoja dhabiti ya kujitoa kwakuwa kuna tatizo la kupendelewa kwa wasanii katika tuzo hizo, basi tutarudi kwenye hoja ile ya umoja miongoni mwa wasanii wa bongo flava kupigania haki zao. Kuna umuhimi wasanii kujiunga dhidi ya kunyonywa haki zao.

Ningependa kuwaacha wapendi wa bongo flava na swali, je maamuzi ya TID na Dully Sykes ni sahihi? na je ni mafundisho gani wanawaachia wasanii wanaochipukia?. Safari ni ndefu katika mziki huu wa bongo flava, na ninadhani kama kuna maonevu kwenye hizi tuzo, basi nafurahi kuona kuwa watu wanaweza kusimama na kuzisusia katika kutafuta haki zao, lakini kama ni kwasababu za kibinafsi kwakuwa fulani ni mwananziki mkubwa na mkongwe hivyo anastahili tuzo, mimi ninahili lakuwaambia, ukubwa wa pua siyo wingi wa kamasi.

Previous ArticleNext Article
Bahati was born and raised in Tanzania, and then moved to California to pursue his college education. He graduated in 2008 with a Bachelor’s Degree in Political Science and a minor in Sociology. Bahati expects to be doing his Masters in African Studies in the near future. He is currently working on starting a t-shirt business and a possible publication of some of his writings. One thing that Bahati cannot live without is music, specifically Hip Hop & Bongoflava which he argues are both the voice of the youth today, and is excited to look into how Bongoflava can be a source of further entrepreneurship among the youth in Tanzania. Bahati believes that Bongoflava can help to reduce poverty in Tanzania, as can a more collective effort among key players.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Send this to a friend