Backyard Studio na Uchaguzi Mkuu

Studio ya Backyard ya jijini Dar es Salaam inatoka na changamoto kabambe kwa wasanii wa muziki wa aina yote. Backyard Studio inatoa offer ya kurekodi bure kwa msanii yeyote mwenye nyimbo ambayo inahusiana na uchaguzi mkuu ujao.

Samuel Andrew Mbwana a.ka Braton anaelezea nia na madhumuni ya offer hii kwa kusema, “nimeona nitoe offer hii ili mradi wasanii wapate nafasi ya kutosha katika kuelimisha jamii kuhusu uchaguzi wa amani, faida kupiga kura na kuelimisha jamii kuhusu viongozi wanao tufaa katika jamii”.

Hii ni changamoto tosha kwa wasanii, hivyo mjitokeze na kuelimisha jamii. Tunatarajia kuona wengi wenu mkijitokeza na kuchangamkia fursa hii ambayo ni adimu. Tukiwa bado tunasononeka na wengi wenu kutojitokeza na kutunga nyimbo kuhusiana na kombe la dunia, basi tunategemea mtatumia hii nafasi vyema kutunga nyimbo kuhusu uchaguzi mkuu.

Habari kwa hisani ya Issa Michuzi

Previous ArticleNext Article
Bahati was born and raised in Tanzania, and then moved to California to pursue his college education. He graduated in 2008 with a Bachelor’s Degree in Political Science and a minor in Sociology. Bahati expects to be doing his Masters in African Studies in the near future. He is currently working on starting a t-shirt business and a possible publication of some of his writings. One thing that Bahati cannot live without is music, specifically Hip Hop & Bongoflava which he argues are both the voice of the youth today, and is excited to look into how Bongoflava can be a source of further entrepreneurship among the youth in Tanzania. Bahati believes that Bongoflava can help to reduce poverty in Tanzania, as can a more collective effort among key players.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Send this to a friend