Hadithi fupi

Kwa wale ambao walikuwa wanafuatilia hadithi fupi hapa Vijana FM (unaweza ukazipata hadithi za awali hapa), nataka kuwataarifu kuwa zoezi la kuzipost hapa litasitishwa kwa muda. Huu uamuzi unatokana na ushauri niliopewa na baadhi ya wasomaji, ndugu, jamaa na marafiki kwa kuwa naangalia kama kuna uwezo wa kuzikusanya na kutoa kitabu hapo baadae (kama nikipata nafasi hiyo).

Kitabu (kitaitwa “Kelele za Ukimya – kutoka Uswazi“) kikikamilika nitawataarifu na nitapost baadhi ya hadithi hapa . Wakati huo huo naelewa kuwa wahusika wanaweza wakakataa kuchapisha kutokana na mambo ninayoongelea na sababu nyingine wa kadha. Lolote litakalotokea, utapata fursa ya kuzisoma — iwe kutoka kwenye kitabu, hapa Vijana FM, forums n.k.

Nawatakia siku na kazi njema!

__

SN.

Previous ArticleNext Article
Steven was born and raised in Dar es Salaam, and moved to Germany for his studies. He graduated with a BSc. in Physics (Jacobs University Bremen), and then a MSc. in Engineering Physics (Technische Universität München). Steven is currently pursuing a PhD in Physics (growth of coatings/multilayers for next generation lithography reflective optics) in the Netherlands. He’s thinking about starting his own business in a few years; something high-tech related. At Vijana FM, Steven discusses issues critical to youths in Tanzania, music, sport and a host of other angles. He’s also helping Vijana FM with a Swahili translation project.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Send this to a friend