Watoto wa Taliban

Kuna propaganda nyingi kuhusu watu wanaojitoa muhanga na kujilipua, hasa kutoka kwenye vyombo vya habari vya nchi za Magharibi. Lakini umeshawahi kujiuliza: Hivi, wanajaribu kutafuta chanzo? Au wamekaa tu kwenye makochi nyumbani na “kujifunza” yanayotokea Pakistani, Afghanistani, Iraki au Israeli kwa kusikiliza habari za saa mbili usiku?

Unaweza ukadhani – labda – baada ya kukusanya ujuzi na maarifa tutaanza kwa kutafuta vyanzo vya matukio ya watu wanaojitoa muhanga badala ya kusambaza propaganda za fitna. Unafikiri tukijifunza asili au vyanzo vya matukio kama haya ulimwengu utaweza kukabili haya mambo?

Sharmeen Obaid-Chinoy kutoka Pakistani amelivalia njuga hili suala; na ifuatayo ni filamu ambayo Sharmeen anazungumzia jinsi Taliban wanavyowashawishi watoto na vijana wadogo kujitoa muhanga:

Napenda kuonya kwamba sio lazima ukubaliane na kila kitu unachoona au kusikia kwenye hizi filamu. Lakini ni vema ukijua nini kinachoendelea kwenye upande wa pili wa thumni. Wakati mwingine labda tunadhani haya mambo hayatuhusu — lakini mimi na wewe tunajua na tumeona (kwenye vyombo vya habari) Watanzania wenzetu ambao wanajihusisha na hivi vitendo.

Previous ArticleNext Article
Steven was born and raised in Dar es Salaam, and moved to Germany for his studies. He graduated with a BSc. in Physics (Jacobs University Bremen), and then a MSc. in Engineering Physics (Technische Universität München). Steven is currently pursuing a PhD in Physics (growth of coatings/multilayers for next generation lithography reflective optics) in the Netherlands. He’s thinking about starting his own business in a few years; something high-tech related. At Vijana FM, Steven discusses issues critical to youths in Tanzania, music, sport and a host of other angles. He’s also helping Vijana FM with a Swahili translation project.

This post has 1 Comment

1

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Send this to a friend