Mnanda

Sikiliza maneno yanayoimbwa kwa makini:

Ngoma ya mchiriku au mnanda ni mojawapo ya vitambulisho vikubwa vya utamaduni wa Wazaramo au watu wanaotoka pwani, kwa ujumla (kuna makabila mengi madogo madogo ukiacha Wazaramo). Bahati mbaya, umekuwa ukihusishwa na kitu tunachokiita “uswahili.”

Ingawa hivi karibuni kuna nyimbo ambazo zimepewa nafasi kwenye vituo vya redio na runinga, kwa mtazamo wangu nadhani kama kungekuwa na watu ambao wangeufanyia kazi huu muziki ipasavyo, labda ungepunguza idadi ya vijana wazururaji.

Nisiwachoshe; kuna filamu nyingine hapa ya Jagwa wakitumbuiza kwenye lile tamasha maarufu la Sauti za Busara (2009).

Kama tamaduni nyingine nyingi tu za Kiafrika, sio kila kitu ni kizuri machoni mwa  watu kutoka kwenye tamaduni nyingine tofauti. Ninafahamu mambo mengi sana yanayotokea ngomani ambayo ingekuwa vema yakisitishwa. Lakini kuudumaza mnanda —  kabisa?

Ningependa kusikia maoni yenu kuhusu mashairi ya kijana:

Nikifikiria dunia, mwenzenu najijutia

Nawahi kukufuru Mungu mie, kwanini nimezaliwa?

Lakini sawa, Mola ndio alivyotupangia

Na jambo akipanga Mola, vigumu kulipangua

Kinachoniuma roho; nikimtazama mwanangu Pili, anavyonitegemea

Huwa najiulizaga sana, kitu gani nitamgaia mwana?

Au nitapofariki, mwanangu? Urithi gani nitamuachia?

Najua atapata tabu mama, hapa katika dunia

Jamani…. Liwalo na liwe, hayo yameshatokea

Hakuna la kufanya, kuweza kuikoa

Liwalo na liwe, hayo yameshatokea…

Previous ArticleNext Article
Steven was born and raised in Dar es Salaam, and moved to Germany for his studies. He graduated with a BSc. in Physics (Jacobs University Bremen), and then a MSc. in Engineering Physics (Technische Universität München). Steven is currently pursuing a PhD in Physics (growth of coatings/multilayers for next generation lithography reflective optics) in the Netherlands. He’s thinking about starting his own business in a few years; something high-tech related. At Vijana FM, Steven discusses issues critical to youths in Tanzania, music, sport and a host of other angles. He’s also helping Vijana FM with a Swahili translation project.

This post has 6 Comments

6
  1. Salala, umemwona mtoto huyo anamwiga mzima kubenua kiuno? Yai lai toba.

    Ama kwa nini mziki huu haupewi kipaumbele, nadhani ni kutona na kuwa nyingi ya tungo zake huwa zinawahusu zaidi watu wakubwa, hivyo nyingi ya nyimbo hizi haziwezi kusikilizwa na watu wa rika zote, yaani, kama ilivyo kwenye filamu, basi mchiriku nao unachukuliwa kama”X” katika muziki. Lakini si zote zipo hivyo.

    Ila ukinipiga swali pia mbona hata ile aina mpya ya Taarab aka Mipasho nayo inatumia maneno yanayofanana na “X” sitakupa jibu bayana, pengine ni kwa vile Mipasho na baadhi ya nyimbo za mahadhi ya Mashairi hutumia zaidi tamathali za semi kuliko Mchiriku ambao hutumia lugha isiyo na kificho.

    Nakubali kukosolewa kwa wanaofahamu zaidi. Wacha niketi nisubiri.

  2. Subi, si nd’o mnanda unavyochezwa (shurti kubenua kiuno), au? Kusema ukweli, nadhani sio mfano mzuri mbele ya watoto wadogo…

    Lakini nadhani wengi tunakumbuka hata Remmy Ongala naye alikuwa ana nyimbo zake tata sana (“Mambo kwa soksi”; ilikuwa mwiko kuucheza, lakini kuna baadhi ya madereva wa dala dala walikuwa vichwa ngumu. Sasa, kasheshe uko kwenye dala dala na mzazi wako! Inabidi utafute mjadala wa kuzugia… Ila wahuni wengine walikuwa wanacheka. Mi’ ilinikuta hiyo na sitakuja kusahau. Mambo yale kuaibishana… Unajisikia kama wewe ndio umeimba ule wimbo. Kinachobakia ni kujifanya huelewi tu na kufunga domo).

    Binafsi nadhani ile kasumba ya “uswahili” ndio inayochangia kudumaza mchiriku kwa kiasi fulani. Kuna nyimbo nyingine nzuri tu zinazoongelea mambo muhimu…

    Napenda kusema kwamba sitetei mambo yanayoendelea kwenye ngoma za mchiriku/mnanda usiku Uswazi.

  3. ukweli ninavyoona mimi kwanza ni stereo type kwa wanaoukejeli mchiriku halafu wanasikilisha hiphop na bongo flava…tofauti si kubwa zaidi .mchiriku ni ngoma ya mtaani..kwa tuliokulia uswahilini kama wanavyosema watu..hii ni sehemu ya utamaduni wetu..swaziland wanatembea uchi..kila mtu anahaki ya kuuelewa na kuutangaza utamaduni wake si kazi yetu kutafakazi wa nani mbya

  4. …Kwa haraka haraka ninaweza kusema kuwa mchiriku umechukua nafasi ya hip hop halisi kwa kuwa unazungumzia hali halisi ya mtu wa kawaida na struggles anazopitia kila siku ya maishani mwake. Huu wimbo umenigusa mno…ni hali halisi ya watanzania wengi…

  5. Habari, naomba mwenye moja kati ya nyimbo hizi. 1: Nasimama katikati AMADI kumuelezea,
    Kwa huu mkakati pengine atatulia, analeta varangati pombe….Amad amadiii punguza pombe utakwenda jela pasipo kutegemea.

    2: Mkeo ukimuachaaa, uache kumfuatafuata,
    Sizai umeniachaaa, kwa mwenzio nimezaaa.

    3. Wanangu leo nimewaiteniii, wananguuu
    Mimi baba yenu nimekula chumvi nyingi wananguuuu,

    4 Nimetokea tu kumpendaaa dada shani,
    Kwa umbile na anavyo kwenda dada shanii

    Juma mpogo a.k.a kifaa kuna hizi:-
    1: Niwewe shemeji yangu nikupendae, na kwa jinaaa unaitwa meeemi mwenye sura nzuri, nayakupendeza……
    2:Tealibu mbonde katoka Jaribu, Daresalaam ndio kwanza anafika…..
    3 Badala yakazi ngumu ya kutafuta pesax2 kitendo gani chakupokewa na boos…..
    4 kitu mapenzi kilianza zamani, tokea enzi za mababu zetuuuu….na hata hao mapenzi waliyakuta, tokea zama za Adam na Hawa……

    MWINA (Miami beach orginal)
    1 Huyoooo hatulii majumbaniiii, huyoooo ameshakuwa kuvulugeeee….
    2 Mwina nimeshika tama, baado nimejiinamia, Hili bado halijaachwa lingine linatokeaaa, tegeta beach wanaliaaa, sikinde kaaga duniaaa
    3: Mtumwa nina kueleza ubadilishe tabiaaa, wewe unaitwa baba ndugu yangu nakwambia, kazihutaki kufanya bwanaaa, virungu unatutia……
    4:Mkwe wangu vumiliaaaa ,ombi ulilolitoaaa, siyo nimekuzarauuuuu, bado nalifikiriaaaa
    5 : Mimi ninahangaika ninatafuta maishaaa, siwezi kukata tamaaa safari yangu sijafikiaa, watu nawaeleza bhuanaa, kazi kutesa kwa zamu ,sivizuri nakushauri uangaike pande zote zaduniaaaa…..

    BABA J (haukucha family)
    1 .Polee ndugu kanaliiii, kwa msiba ulio kufikaaa, kanali usilie sanaaa, hiyo kazi ya Rabuuukaaaa. Kwani kazi ya Mungu huwa haina makosa, kaumba dunia kaweka kila tabaka, kuna makaburi mapori na majangwa, mabwawa na mito maji yalochanganyika……😂😂😂
    2 :Salima nilikuambia, tulia nyumbani lakini hukunisikia sijui unataka niniix2 uzuri wa mwanamke…….
    3: Mama ebu fikiriaaaa mwanao ulio mzaaaa, umepata tabu kuleaaaaa mpaka sasa amekuwaa……
    4: Nauliza naulizaaaa walimwengu nifahamisheniiiii, mimi baba jeiiiii hapa dunianiiii sijui nifanye niniiii
    Hebu tuunde group la WHATSUP tujikumbushe ladha hizi. Naamini walioko Dar mnaweza kuwa msaada mkubwa kwetu ili mziki huu tuweze kuurithisha kwa kizazi na kizazi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Send this to a friend