Watoto wanaweza kujifunza bila mwalimu?

Wakati tukitafuta suluhisho bora kuhusu tatizo la elimu nchini, baadhi ya washikadau wanafanya majaribio ya kisasa kusaidia ufundishaji bora wa wanafunzi. Sugata Mitra na wenzake wanataka kufahamu je, bila uwepo wa mwalimu wanafunzi wanaweza kujifundisha wenyewe kwa kutumia kompyuta? Endelea kwa kutazama video hii ili ujionee maajabu kuhusu yepi yanawezekana.

Tumepata mwanga kuwa wanafunzi wadogo wanaweza kujifundisha wenyewe, na hasa katika makundi madogomadogo. Ni mambo gani yamekugusa ulipoangalia video hii? Binafsi ninapoangalia vitu kama hivi ninamuwaza mwanafunzi wa kule Kalamazwite, Rukwa au pale Mwembe-makumbi, Unguja na kutamani siku moja naye apate nafasi ya kuunganishwa katika gridi ya utandawazi kwa njia kama hii, ili baadaye naye aweze kuwa na usawa wa kiushindani akilinganishwa na wengine popote duniani. Je, tunaweza kutumia njia kama hii ya kompyuta ili kusaidia kupunguza tatizo la uhaba wa walimu? Tujiulize maswali gani kabla ya kudandia project kama ya one-laptop-per-child (OLPC)?

Picha kwa hisani ya www.jamiiforums.com
Previous ArticleNext Article
Joji was born and grew up in Dar es Salaam, Tanzania. He graduated with a B.Sc in Biochemistry in Germany, and is now pursuing a Masters degree in Microbiology & Immunology at the Swiss Federal Institute of Technology (ETH) in Zurich, Switzerland . Joji is particularly interested in matters related to global health, and basic science research that tackles public health challenges. He is engaged in mentoring Tanzanian students in higher education issues, most notably at the Kibaha High School. In this capacity, Joji blogs with Vijana FM about scientific research and development, and how youth can gain greater access to higher learning.

This post has 9 Comments

9
  1. ah nahisi mambo haya hayahitaji kukurupuka kaka. wenzetu washafanya utafiti wa kutosha; unajua hata tatizo letu katika teknolojia ni kwamba tunakopi na kupaste tu. hatujali kama yatufaa au dhumuni la kwanza la kutengenezwa teknoli hiyo yaendanana na ya kwetu, au kwa vile imefaa ughaibuni na kwetu itafaa tu. mi nachokka sana na hii system ya kutopambanua mambo kwa kina na kuaamua kukopi tu… ila mtoto wa kilindi kilwa huko mpaka haya yamkute, wenzetu watakuwa wanasoma kutumia invisible laptop.

  2. ek, unaongelea nani hasa kwenye suala la kukopi na kupaste tu? Mtu aliyeona wenzetu wanafanya nini na kutuletea makala (tujaribu kujifunza) au “sisi” (serikali ya Tanzania) ndio inayokopi na kupaste?

    Aisee, bora hata hiyo Serikali yetu ingekuwa inakopi halafu tunakuja kurekebisha makosa tu, badala ya kutofanya kitu chochote kabisa!

    Labda mengine kutoka ughaibuni hayafai kwetu kama unavyosema, basi fanya utafiti na utuletee ripoti kabla ya kurusha mawe. Na wakati ukifanya utafiti kumbuka baada ya miaka 10 – 20, wadogo zetu kutoka Lindi hawatakuwa wanashindana na Watanzania wenzao tu…

    Sasa, swali la msingi ni hili: tubaki tukisubiri Serikali yetu ifanye utafiti na kuamua nini hasa kifanyike kuokoa jahazi (kuamua teknolojia au mifumo ipi inafaa kukuza vipaji vya wanafunzi), au kuangalia mifumo gani inafanya vizuri na kujaribu kuitumia kwenye jamii yetu Tanzania?

  3. EK, utafiti huu umefanywa India, katika sehemu zenye umasikini unaofanana na ule uliopo Tanzania. Walijaribu pia Afrika ya Kusini na kuona pia wanafunzi wanaweza kujifundisha masomo mbalimbali wenyewe bila uwepo wa mwalimu.

    Kwahiyo la maana litakuwa kufikiria kama utafiti huu unaweza kutumika Tanzania, kwani walimu wengi hawapendi kwenda kufundisha vijijini. Miaka 20 ijayo kazi nyingi zitahitaji uelewa wa masuala ya IT na teknolojia, watoto wakitayarishwa mapema itawasaidia kuwa washindani kimataifa hapo baadaye.

    Rais wa TZ majuzi alitoa ahadi kuwa kila mwanafunzi baada ya miaka mitano atakuwa na laptop. Sasa hapa tunaweza kujadili na kumkabili kwa kumuuliza pesa za laptop moja kwa kila mwanafunzi zitatoka wapi? Je, tutatumia zile laptop za dola 100 za project One-Laptop-Per-Child? Kwanini tusiangalie basi uwezekano wa laptop 1 kwa wanafunzi 5 na kuendelea – kwa sababu watafiti kama Prof. Mitra wanasema wanafunzi wanafanya vyema zaidi wakijifunza kompyuta kwa makundi.

    Na sio lazima ku’copy na ku’paste. Tuwahusishe basi na wataalamu wetu kutafuta njia mbadala za kuwapa mwangaza wa kiteknolojia wanafunzi wetu wa msingi. Njia iliyo nafuu, na yenye ufanisi.

    Hatuwezi kuruka ngazi za maendeleo, tatizo la walimu walio bora linabidi litatuliwe haraka, na hili liwe la kipaumbele. Ila tusidhani wenzetu watatusubiri.

  4. Naamini inawezekana kabisa na huyu jamaa ameshafanya majaribio ya ajabu. La muhimu ni kutengeneza mfumo wa kuweza kufanya hivyo … kwa kweli shirika la TAMASHA linafikiria sana suala hilo na lingependa kuwasiliana na wakereketwa wa elimu ambao wanajua kwamba huu mfumo tulio nao hauwezi kufanya kazi tena. Ni sawa na kupiga rangi gari mkweche. Umkweche utabaki palepale, tunahitaji mawazo mbadala

  5. Labda “kujifunza” ni neno sahihi kama unavyopendekeza, Joe. Lakini nadhani mwandishi alikuwa anajaribu kusema “teach oneself/themselves” na sio “learn”; ambayo ndio dhana kubwa ya makala hii. Pia, kumbuka mtu anaweza akafundishwa lakini akashindwa kujifunza chochote.

    Sasa, kama Kiswahili hakina mzizi wa neno lenye maana sawa na “teach oneself” basi inakuwa ngumu kuwasilisha ujumbe sahihi. Kiswahili kigumu jamani — mimi mpaka leo bado natafuta neno sahihi la Kiswahili lenye maana sawa na “privacy.”

  6. Kujifunza ni kuwa na madiliko yaliyo chanya au hasi kutokana na fundisho ulopata kwa madhuni flani,au kupata kufahamu jambo,kitu au swala fulani kwa kushiriki ktk jambo au kwa kufikiri. Mwanafunzi anaweza kujifunza mwenyewe katk level flan hasa ktk utoto ambapo matendo yake humpelekea kujifunza kwa kuona kinachofanywa na wenzake au madhala yanayoweza mtokea ktk michezo yake. Lakini kuna maarifa ambayo mwanafunzi hawezi kujifunza pasi mwalim. Mathalan maarifa yatokanayo na histori, principles au sheria, mwalim ananafasi kubwa hasa ktk kum ‘scafford’ anapo shindwa. Nafasi ya mwalim haiwez kupuuzwa hasa ktk kumback up mwanafunzi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Send this to a friend