Mbongi wa makamu mkuu wa UDSM

‘Uhuru una maana gani kwangu? Mtazamo wa vijana’

Katika vyombo vya habari, mijadala mbalimbali na hata maongezi ya kawaida, wananchi wanahisi na wanasema kwamba mshikamano wa kitaifa na wa kijamii umepungua sana katika nchi yetu, haswa katika miaka ya hivi karibuni. Ni dhahiri kwamba hisia hizo sio za kubuni bali ni dalili za hali halisi. Au ni hisia tu? Ishara moja wapo ya mipasuko hii ni malumbano ambayo tumeanza kushuhudia kila siku katika magazeti yetu na hoja na misimamo mbalimbali ya kisiasia na wanasiasa. Au hayo sio malumbano bali ni mijadala tu ambayo ni muhimu iwepo katika mfumo wa kidemokrasia?

Tumeshuhudia malumbano kuhusu wa Tanganyika na Zanzibar. Hii ni dalili mojawapo ya mpasuko wa ki-nchi na wa kitaifa. Je, ni kweli, kwa sababu matatizo ya muungano ni ya muda mrefu tu? Tumesoma na kusikia malumbano ya kidini na pia tumeshuhudia baadhi ya wasomi, wanahabari na wanasiasa wakijenga hoja zao kwa kuegemea dini. Au hii ni sehemu ya uhuru wa kimawazo tu kwa hivyo haina ubaya wowote? Au, kwa vyovyote vile, si jambo geni kwa sababu huko nyuma mawazo kama haya yalikuwepo bali hayakuzungumziwa kwa uwazi? Tumekuta baadhi ya wanasiasa wakitumia ukanda kuwashawishi wananchi. Na pia tumesikia wengine wakitumia tofauti za ubaguzi wa rangi kama kisingizio cha kujitafutia mashabiki. Ukweli ni kwamba ule mshikimano wa kitaifa na kijamii ambao tulizoea katika miongo miwili ya baada ya uhuru umedidimia kwa kiasi kikubwa. Au hoja hizi ni za watu wachache ambao ni wafuasi tu wa mfumo wa uhodhi (monopoly) wa kisiasa na kimawazo?

Lengo la Mbongi huu ni kujadili masuala haya kwa uwazi, ufasaha na kwa undani ili kubainisha vyanzo na chimbuko la mipasuko hii. Kama ilivyo kawaida katika mijadala, sio washiriki wote wakubaliane. Ndio maana ya kujadili. Jukumu la Mchokozi Mkuu (chief interlocutor) ni kuibua masuala mbalimbali ili kuchochea mijadala.

Je, ni kweli kwamba jamii yetu ina mipasuko au hizo ni hisia tu za watu wachache? Kwani kuna ubaya gani watu kujitambulisha kwa misingi ya dini zao, makabila yao au ukanda wao? Na kama kuna ubaya, ubaya hasa uko wapi? Katika medani ya siasa au ya kijamii? Miongoni mwa wananchi wenyewe au wanasiasia na viongozi? Nini ni chimbuko la mifarakano hii na nani awajibike? Wapi tutafute chimbuko na vyanzo vya mipasuko? Katika mfumo wa kisiasa, kijamii au kiuchumi? Je, mipasuko hii ina uhusiano wowote na mfumo wa uchumi, hususan, mgawanyiko wa kitabaka katika mfumo wa uzalishaji? Na je kuna uhusiano wowote kati ya tunachoshuhudia katika jamii yetu na uhusiano wetu na mataifa ya nje au jinsi tulivyoingiliana na mfumo wa utandawazi?

Nini kifanyike ili tuweze kuepukana na madhara ya mipasuko hii? Tuanzie wapi? Mfumo wa elimu, utamaduni au mfumo wa kisiasa? Na nani mwenye jukumu la kuchochoea utafutaji wa dira mpya itakayoleta mshikamano? Je, panaweza kuwepo mshikamano wa kitaifa bila kujali mgawanyiko wa kitabaka? Mgawanyiko kati ya matajiri wachache na mafukura wengi?

Nini wajibu wa wasomi na wanazuoni katika hali kama hii?

Nyote mnaalikwa

Lini: Oktoba 14, 2010

Wapi: Ukumbi wa Nkrumah, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM)

Waandaaji: Kigoda cha Taaluma cha Mwalimu Nyerere

Muda: Saa 3.00 asubuhi – saa 9.00 mchana

Ratiba kamili inapatikana hapa (bofya)

Kuhusu Kigoda cha Taaluma cha Mwalimu Nyerere, bofya hapa

Previous ArticleNext Article
Joji was born and grew up in Dar es Salaam, Tanzania. He graduated with a B.Sc in Biochemistry in Germany, and is now pursuing a Masters degree in Microbiology & Immunology at the Swiss Federal Institute of Technology (ETH) in Zurich, Switzerland . Joji is particularly interested in matters related to global health, and basic science research that tackles public health challenges. He is engaged in mentoring Tanzanian students in higher education issues, most notably at the Kibaha High School. In this capacity, Joji blogs with Vijana FM about scientific research and development, and how youth can gain greater access to higher learning.

This post has 1 Comment

1
  1. Kwa kweli yote hayo ni kweli tupu, kwanza Tz imekuwa na mitazamo mingi lakini mtazamo wa kidini na kubaguana ndo imechukua nafasi, mf. mtoto wa kigogo hata kama hakupata alama za juu anapata chuo na ufadhili 100% lakini wa-mlala hoi anaachwa akiangaika na maksi zake za juu, kwa kweli Tz imekuwa haina usawa ktk nyanja zote, pia ni uonevu mwingi na dhuluma ndio imewajaa na chuki binafsi pia, mf. mtu anaambiwa sio raia na anaonekana hafai kwa wakati huo ktk uongozi ghafla baada ya kuona walichokitaka kimekua, wanasema tena bila aibu “amethibitishwa ni raia, yaani huo ni uonevu mtupu na hakuna uhuru wala hekima yoyote, mf. unaweza kusema jambo fulani ukanyamazishwa au kufukuzwa kama si kusimamishwa katika nafasi uliyokuwa nayo. Pia umasikini ndio usiseme, watoto wetu wanaendelea kukalia vumbi wakiwa wameshikilia madaftari wakimsikiliza mwalimu akifundisha darasani, yaani inatia uchungu sana. Da! nashindwa kuendelea, Mubarikiwe kwa hoja yenye nguvu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Send this to a friend