Sikukuu njema

Steven was born and raised in Dar es Salaam, and moved to Germany for his studies. He graduated with a BSc. in Physics (Jacobs University Bremen), and then a MSc. in Engineering Physics (Technische Universität München). Steven is currently pursuing a PhD in Physics (growth of coatings/multilayers for next generation lithography reflective optics) in the Netherlands. He’s thinking about starting his own business in a few years; something high-tech related. At Vijana FM, Steven discusses issues critical to youths in Tanzania, music, sport and a host of other angles. He’s also helping Vijana FM with a Swahili translation project.

This post has 6 Comments

6
  1. Kuna kitabu alichowahi kukiandika baba wa Taifa JK.Nyerere kiitwacho ‘‘UONGOZI WETU NA HATIMA YA TANZANIA”. ni kitabu ambacho kimebeba maudhui mengi sana na yamkini unayajua au ulisha wahi kuyasikia katika baadhi ya hotuba zake,lakini pia kuna baadhi ya mengi tu waweze kuwa hujui kuwa kumbe yaliwahi kutokea kipindi cha zamani na sasa ni kama marudio tu,ila kwa sababu ya watu wengi kutojua na kwa sababu ya ukali na uwazi wa maneno alioutumia Nyerere katika kuandika hiki kitabu ,inasemekena kuwa hiki kitabu kilishapigwa marufuku kuuzwa nchini Tanzania kwa hiyo watu wengi hasa vijana waliokuwa bado wadogo inawezekana wasijue kilichokuwa kinaendelea hasa wakati wa uongozi wa Mh.Mwinyi.

    Kwa kifupi kuna mikasa mingi tu ila kuna miwili iliyolitikisa taifa kipindi hicho cha uongozi wa Rais Mwinyi nayo ni ule wa Zanzibar kujiunga na OIC na lile la wabunge wa Tanganyika kudai Taifa la Tanganyika yaani kuwe na Tanganyika,Zanzibar na Federation.

    Haya yalikuwa ni mambo mazito sana kwani yaliitikisa sana nchi na mpaka ikafikia Baba wa Taifa kuingilia Kati na kuanza kuongoza serikalii baada ya uongozi wa Mwinyi kuwa legelege na jeshi kutishia kuongoza Taifa kwa nguvu. Pia tukumbuke kilikuwa ni kipindi hikihiki ambao kulikuwa na maandalizi ya kuanza mfumo wa vyama vingi ambapo kulikuwa na haja ya kuanza mfumo wa kupokezana uongozi ambapo kulihitaji hekima na utashi wa hali ya juu lasivyo taifa lingeingia kwenye machafuko.

    Swala la Zanzibar kujiunga na OIC lilipingwa na bunge kwani lilikuwa ni kinyume na Katiba ya MUUNGANO ambayo inasema serikari haina dini yeyote, Kamati kuu ya CCM,Halimashauri kuu na bunge la Muungano lakini kwa sababu walivyoziita wenyewe eti ‘‘nyeti” waliruhusu Zanzibar kujiunga na OIC tena kwa siri,lakini siri haikuchukua mda mrefu na kila kitu kilikuwa wazi, baada ya kuona hivyo basi wabunge 55 walisaini majina yao kuomba kurudishwa Taifa la Tanganyika na walipoulizwa na baba wa taifa walisema kuwa wamechoshwa na uzanzibar .Hawa wabunge walijua hali halisi kuwa kuomba utanganyika maana yake mojakwa moja hakuna Tanzania walimaanisha kabisa kuwa basi walikuwa wamechoka na Mwinyi na walitaka achukue virago vyake .Maana ni hali halisi kama hili lingepita kama lilivyokuwa limekusudiwa ni wazi kuwa haohao wabunge wangem-impinchi (kumvua madaraka) .Raisi Cha ajabu Bunge lilipitisha azimio chini ya waziri mkuu Mh.John Malecela kipindi hicho,Waziri wa Sheria alikuwa ni Mh.Samwel Sitta, Katibu mkuu wa CCM Mh.Horrace Kolimba,Spika wa Bunge Msekwa ,Kiongozi wa group la WABUNGE 55 Mhe.Njelu Kasaka na Rais wa Zanzibar na makamu wa pili wa Tanzania alikuwa ni Dr.Salmor Amour.

    Katika kitabu hiki tunamwona Nyerere anasema sijawahi kulia kwa mambo ya CCM lakini siku hiyoalilia tena kwa machozi baada ya kukutana Dodoma kwenye Kamati kuu ya CCM wakati alikuwa akijua kabisa kuwa swala la wale wabunge kudai Tanganyika lilikuwa limeshakwisha,lakini cha ajabu alipofika pale kulikuwa kumeandaliwa lipoti ya uongo wa wazi iliyosomwa na Waziri wa sheria wakati huo Mh.Samweli Sita ikiwa imepambwa urembo kibao kumbe ni uongo mtupu ,alipowauliza wale wabunge hizi ilikuwa je hadi mkafikia huku walkajibu mzee bunge zima lilipitisha,alipomwuliza waziri mkuu(Samweli Malecela) akajibu wabunge walikuwa Mbogo. Na hii inaonesha wazi kuwa Raisi alishindwa kuzuia huu mjadala pamoja na mara ya kwanza kutoa hotuba kubwa bungeni akikemea Zanzibar kujiunga na OIC na kuamru ijiondoe, lakini kwa kuwa yeye ndio aliyeruhusu Zanzibar ijiunge na OIC (ingawa wabunge wengi walikuwa wakipinga) basi ilimuwia ugumu sana kupinga hiyo hoja ya gropu la wabunge 55 ,hivyo akakubali hali akijua kuwa yeye kama Rais alitakiwa ailinde Katiba ya Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania zaidi ya yeyote yule.Bahati nzuri Kamati kuu ya CCM ilikataa hiyo hoja na wakasema kuwa CCM inaamini na kushikilia misingi yake ya kuwa Tanganyika ziliungana na Tanzania kuwepo ,na bila Tanzania maana yake hakuna Tanganyika na kama tukiifufua Tanganyika maana yake ni kuua Tanzania.

    Baba wa Taifa ilibidi awe mkali sana alirudi Butiama akaandika mashairi marefu sana ambayo yote yalikuwa yakielezea hali halisi tangu hilo fukufuku la wabunge na alivyo washauri lakini walikuwa ni vichwa vigumu sana na kukaidi.

    Mara ya mwisho amejaribu kuongelea nini maana ya uwajibikaji kwa viongozi na akaelezea kwa urefu sana maana ya ku –resign (kuachia ngazi) akisema wazi kuwa hao viongozi(waziri mkuu,waziri wa sheria,katibu mkuu n.k) walipaswa kujihudhuru mara moja na kukaa pembeni na yeye mwenyewe alitumwa na Rais Mwinyi kuwaeleza kuhusu huo uwajibikaji lakini walikaidi ,Waziri mkuu alisema kuwa kama akijihudhuru na Rais kuteua Waziri mwingine mkuu wale wabunge 55 watapinga ,hivyo ni bora tu waendelea kuwa viongozi hapo utaona ni jinsi gani huu Malecela alivyokuwa anamchezea Raisi na kuwatumia wale wabunge 55.Ndio maana kama utakumbuka Baba waTaifa aliwachukia sana akina Malecela na na viongozi wengine mnaowajua hadi leo.

    Swala la uwajibikaji linaendele kuwa ni ndoto kwa Taifa letu hadi leo tumeshuhudia viongozi kama akina Lowasa ,Chenge,Rostam n.k…wanasitaafu uwaziri na kuendelea na ubunge na sasa tena bado wanaomba nafasi nyingine ya kurudi bungeni na kushuhudia Raisi wetu bila hata haya woga anawapigia kampeni na kuwasifia kuwa ni wachapa kazi.Jetutafika kweli?? nadhani bado tunasafari ndefu tena sana na yamkini wajukuu wetu ndo watakaofika huko wala sio kizazi chetu hiki.

    Kitu kilichonifurahisha zaidi katika hiki kitabu Nyerere alikuwa mu-wazi sana na hata ikafikia akaongelea kuhusu CCM kuwa hicho chama kwa sasa kina ‘‘kansa ya Uongozi ambapo isipotibiwa itakiua chama kizima” na akathubutu hata kusema anatamani kuona chama kingine cha upinzani kitakachoweza kukiondoa madarakani,ila akasema hadi sasa bado hajaona chama kingine na kwa hiyo pamoja na kansa ya uongozi wa CCM watu wataendelea kukichagua,au watu wanaweza wakachoka na kusema potelea mbali wakachagua chama chochote ilimradi tu watokane na kansa ya uongozi wa CCM.

    Wosia wa Baba wa Taifa.

    Ole wako Tanzania ;
    Tusipoisaidia!
    Niwezalo Nimefanya,
    kushauri na kuonya,

    Nimeonya Tahadhali,
    Nimetoa ushauri,
    Nimeshatoka kitini,
    Zaidi nifanye nini?

    Namlilia Jalia
    Atumlikie njia
    Tanzania ailinde
    waovu wasiivunje

    Nasi tumsaidie
    Yote tusiya mwachie
    Amina tena Amina
    Amina Tena na Tena.

  2. Ndugu Bihemo hiyo pdf hai-download, napata error messages, hata hiyo tovuti ya mallaba.org haifunguki, sasa sijui kama kuna uwezekano wa kunitumia hii pdf kupitia email address…

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Send this to a friend