Kunani Memphis na Hasheem Thabeet?

Leo nataka kujadili hili la minong’ono juu ya Hasheem Thabeet kuhamishwa kwenda timu nyingine. Kwa baadhi yetu ambao tunafuatilia ligi ya kikapu ya marekani (NBA), tunajua kuwa msimu huu si lele mama, na timu nyingi wanafanya mabadiliko kujiimarisha.

Mbona hatuoni "mikuno" na "matawi" tuliyokuwa tunategemea?

Lakini tukiacha yote hayo, mcheza kwao hutunzwa. Hivyo nimeona niliangalie hili la Hasheem Thabeet, pamoja ya kuwa mimi sio shabiki wa Memphis Grizzlies.

Miezi kadhaa Hasheem alipopelekwa D-League baadhi yenu mlipatwa na hofu kidogo. Mimi binafsi habari hiyo haikunishtua, kwani wachezaji wapya (rookies) hupelekwa huko mara kwa mara ili waboreshe mambo kadhaa katika mchezo wao. Lakini wasiwasi wangu na Hasheem umeanza hivi sasa; pamoja kuwa ni mdogo, lakini umeanza rasmi.

Baada ya kutathmini msimu huu unapoelekea na jinsi timu zilivyojizatiti kutokana na ushindani kuwa mkubwa, kuna uwezekano mkubwa sana wa wachezaji ambao viwango vyao kimchezo havijaongezeka kutupwa nje au kukaa benchi. Hapa ndipo wasiwasi wangu na Hasheem unakuja, na makala hii inaakisi vizuri wasiwasi wangu juu ya Hasheem na mchezo wake.

Mimi binafsi sitapenda kuona furaha yetu na Hasheem (ya kuwa NBA) inakatika ghafla kama mwanga wa kikoroboi, kwani mwanga huo umeshafifia kutokana na Hasheem kupata muda mchache wa kucheza. Hali hii ikiendelea, najua nafasi ya Hasheem itaanza kuwa matatani, kwa sababu najua msimu ujao kutakuwa na wachezaji wapya kutoka vyuoni wenye usongo wa kuingia NBA.

Hapo hapo, Grizzlies nao wataanza kutafuta “center” wa kutegemewa kumsaidia Marc Gasol, kwani wachezaji huumia mara kwa mara, kama yaliyomtokea “center” wa Rockets, Yao Ming mpaka hii leo. Hii ndio maana timu nyingi hupenda kuwa na mchezaji mwingine wa kutegemewa nyuma ya namba moja katika kila nafasi. Lakini kwa hivi sasa, kama Gasol akiumia, nina mashaka kama Hasheem atakuwa chaguo la kwanza kuziba pengo.

Kiwango: Hasheem anaweza kuziba pengo la Gasol atakapoumia?

Ninasema hivyo kwasababu endapo Grizzlies wataingia kwenye ngwe ya mtoano (playoffs), shughuli itakuwa ni kufa na kupona tu! Kwani Hasheem na Gasol, watabidi wakabiliane na akina  Shaquille O’neal na Perkins wa Celtics, Howard wa Orlando Magic n.k. — hawa wote ni vyuma vya reli.

Lakini pamoja na yote haya, ningependa sana kusikia upande wa Hasheem kwenye hili suala zima, na hasa mambo kadhaa yaliyoandikwa kwenye makala niliyoitaja hapo juu. Hasa kupata mtanzamo wake juu ya maendeleo yake kimchezo na nafasi yake katika ushindani mkubwa uliopo hivi sasa.

Previous ArticleNext Article
Bahati was born and raised in Tanzania, and then moved to California to pursue his college education. He graduated in 2008 with a Bachelor’s Degree in Political Science and a minor in Sociology. Bahati expects to be doing his Masters in African Studies in the near future. He is currently working on starting a t-shirt business and a possible publication of some of his writings. One thing that Bahati cannot live without is music, specifically Hip Hop & Bongoflava which he argues are both the voice of the youth today, and is excited to look into how Bongoflava can be a source of further entrepreneurship among the youth in Tanzania. Bahati believes that Bongoflava can help to reduce poverty in Tanzania, as can a more collective effort among key players.

This post has 7 Comments

7
  1. Mimi nina wasiwasi, lakini ninamatumaini makubwa sana na dogo Hasheem. Nadhani anaweza ku-improve wakati wowote pale atakapopata muda wa kucheza, hata kama inamaanisha trade, kwani sasa hivi wanampa muda mchache sana kutokana na kukata tamaa nae na maendeleo yake madogo. Ukifuatilia vizuri uchambuzi wa wataalamu wa NBA…NBAtv, Sports Center, etc, unaweza kukubaliana na mimi. Wanasema kwamba kila mtu alijua kwamba jamaa atakuwa long term project(3-5years, or so), yaani hamna mtu aliyetegeme kwamba jamaa angeweza ku-impact game mara moja. Ila ugomvi unakuja kwamba Memphis walichukua risk kumchukua namba namba mbili katika draft-na inasemekana kwamba kocha wake alikuwa hamtaki, ila alilazimishwa na maneger au owner, kitu kama icho, kwa hiyo kuna malumbano fulani kuhusu huyu Hasheem, ila pia kidogo na yeye hasheem anachangia kwani badala ya kuwa-prove wrong watu wanaomtilia mashaka, yeye ndio anawapa kichwa kidogo kutokana na uzembe kidogo. Hata pia ndio maana alipelekwa d-league na kocha kama adahbu fulani ya uzembe udaku ulivyodai.

    Ila kwa kifupi jamaa atakuwa fresh tu baada ya miaka miwili mitatu hivi, pia akikaza msuli lakini. Hata foward wao wa Memphis mfano anaitwa Zack Randolph naye alikuwa nyanya kwa muda mrefu, kwenda timu mpaka timu kwa miaka kama tisa kumi sasa, ndio amekuwa babu kubwa wakutegemewa. Jamaa atakuwa okay, msiwe na wasiwasi wapenzi. Ila pia itabidi ajitahidi sana mazoezi hasa kipindi cha summer. Ila kweli akiridhika kama sasa hivi bila juhudi, kweli vijana wanaotoka vyou na usongo wa NBA watamfanya atafute timu China, au Europe. Ila kila laheri Hasheem. Jitahidi bwana.
    Happy Holidays everyone!!!

  2. Amani, umenena..na unachosema ni kweli, sema sasa kwa mchezaji wa nje alafu akitokea mchezaji mwingine ambaye ana usongo zaidi na atachukua fedha kidogo, hapo ndio kasheshe.

    Ligi imekuwa mshike mshike msimu huu. Pia unachosema kuhusu bidii ni kweli, manake ukiamwangalia Shannon Brown wa Lakers, msimu uliopita na msimu huu ni mchezaji tofauti, mambo ya kushinda gym summer nzima. Dwight Howard na yeye alikuwa akifanya mazoezi na Hakeem ku-improve game yake.

    Mimi nina hope kuwa mabadiliko yataanza kuonekana. Kwani suala la kuongezewa minutes, huja pale unapofanya mambo ndani ya dakika chache zile zile unazopewa, kwani ukisubiri uongezewe muda ndio ufanye mambo, utajikuta hata hizo dakika chache ni dakika za kuotea mara moja moja.

    Hapo hapo umegusia pointi nzuri, labda Hasheem atakuja ku-improve ndani ya hii miaka miwili mitatu ijayo, na labda anahitaji kuhamia timu nyingine ambayo itakuwa na matumaini naye mapya kuliko picha ninayopata hivi sasa kati yake na Grizzlies.

    Kwani ukimwangalia Turkoglu alivyohamia Toronto alafu Suns, alikuwa sio yule wa Magic. Ni kama alififia lakini sasa hivi nina furahi kusikia kuwa amerudi Magic kwani tunakumbuka moto wake alivyokuwa huko, inawezekana chemistry yake na system ya coach wa Magic inapikika kisawa sawa…

    anyways tusubiri tuone

  3. Dah, si mchezo. Just last week nilikuwa naangalia documentary ya Hakeem “The Dream” Olajuwon….shiiiiiiiii….and story yake na Hasheem sio tofauti sana. Ila Olajuwon was more talented I would say.

    Mimi tatizo naona ni Hasheem alikimbilia NBA mapema sana. 1 more year in Uconn would have helped. Manake kama Bahati ulivyosema, NBA ni ngangari mbaya siku hizi. Makocha hawana muda wa nurture talents. Wanataka ready made products. Na hasheem is far from that.

    Halafu kuwa drafted 2nd hurts it alot. All eyes on him. Angekuwa 20th or so. Watu wasingemfutilia kabisa. So angeendelea ku improve pole pole.

    Anyway, mimi naona they should trade him to lower teams ili apate playing mins. Ila na yeye aingie gym full time, kufa na kupona. Aongeze msuli, na post moves. Anaonekana yuko very rigid. So kazi anayo ukimfananisha na elite centers.

    ili ni lazima aongeze mazoezi, na awe traded to lower teams ili in 2 years awe amepata exposure ya kutosha. manake naogopa akiendelea hivi Memphis hawataongeza contract. Na timu nyingine hazitamtaka. Then thats it. 3/4 yrs career in the NBA. So lazima aongeze bidii.

  4. Bata nadhani huo utakuwa ushauri mzuri kwa kaka Hasheem. 1 more year in Uconn ni kweli ingesaidia, tatizo ziku hizi karibu kila sport, ukifika tu miaka ishirini na tano, unaanza kuangaliwa kama mzee, manake watu wanaanza pro miaka 17, well nba wameongeza kidogo, lakini ndio hivyo tena.

    Tatizo jingine sasa hivi ni kuwa, zile timu ambazo zipo chini zinaclear cap space ili ku-acquire heavy weights, kaa umefuatilia timu kama New Jersey Nets in the past few seasons wamekuwa wanatimua watu ili wawe na space ya kuwa na star, walimkosa Lebron, lakini sasa wanamwinda Carmelo, hivyo hata kwenye timu zinazojijenga, wao wanaclear space for heavy weights, sio ku-nurture talent kama ulivyosema, lakini doesnt mean there is no hope.

    Mimi sijui vizuri organization ya Memphis iko vipi, ndio maana tungempaha Hasheem ingetusaidia. Ninasema hivyo kwakuwa, Bynum wa Lakers alipochukuliwa kila mtu alimshangaa GM. Na yeye alikuwa yupo yupo tu, watu wakaanza kushangaa GM wa Lakers anaweza kufanya blunders kihivyo. Lakini kutoka na organization/ franchise ilivyo, Bynum akapewa special coach afanye naye mazoezi ya kuimprove game yake, and that was the all time great Kareem Abdul-Jabaar.

    Sasa sijui kama kuna uwezekano kama huo kwa Memphis kumpatia Hasheem kocha wa kiufundi ku-nurture his talent, but again, wanaweza kuwa wameshafanya hivyo, au labda Hasheem mwenyewe atafute kocha ambae atafanya nae kazi, kama Hakeem

  5. D-league itamsaidia sana kwa maoni yangu..sio dhambi wala aibu hata kidogo kucheza d-league…asisahau,umri nao unaenda,mathalani NBA…hao wakina Bynum ndo kwanza wana miaka 20..Hasheem akifika 25 na kama bado atakuwa anacheza kama achezavyo,mikataba itakuwa ya wasiwasi…

    Ni mchezaji mzuri,ila nikionacho ni ukosefu wa confidence tu ambayo akirudi d-league ataipata vizuri..

  6. D-League haimfai sana wala nini kwa kiwango chake(expectation), yaani second pick overall. Ndio maana aliweka historia ya kuwa the first highest pick kuwa sent huko d-league. Wachezaji wanaochukuliwa first round, mara nyingi sio raisi kwenda d-league, mara nyingi wanakuwa wakali sana, isipokuwa Hasheem tu na wachache wengine kama Darko Milicic, Kwame Brown, Yinka Dare, etc, ndio maana pick ya Hasheem iliitwa “risk” . Ila ninakubaliana na Bahati hapo juu, labda trade inaweza ikawa kitu kuzuri kwake akapata muda wa kucheza, Toronto walikuwa wanamuulizia mfano, na Huston wanajaribu kuomba exceptions ya Yao. Ila inabidia naye Hasheem ajiatahidi sana na hou muda mdogo anaopata kucheza. Inaonekana kama ameridhika fulani alikuwa amesemwa hata na wataalamu wa NBA, ukiachia wabongo, ingawa wabongo wamezidi negativity. Inabidi aamke mapema, uwezo anao. Ila kama wazee mnavyosema hapo juu, asipojitahidi anaweza akaishia 4 year career NBA.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Send this to a friend