Utamaduni wa kusoma vitabu

Na Sakura

Kumekuwa na mijadala mirefu inayohusiana na utamaduni wa kujisomea vitabu. Wakati nchi za Magharibi zikikabiliana na kushuka kwa kiwango cha usomaji, kutokana na ushindani ulioletwa na teknolojia mpya (runinga, Facebook, Youtube n.k.), nchi za Afrika — hasa kusini mwa jangwa la Sahara — zinasemekana kuwa hazijawahi hata kuwa na utamaduni huo.

Kwa mujibu wa Baraza la Maendeleo ya Vitabu Tanzania (BAMVITA), idadi ya washiriki imekuwa ikiongezeka kwenye maonesho yake ya kila mwaka ya Wiki ya Vitabu, japokuwa mauzo ya vitabu kwenye maonesho hayo bado hayaridhishi.

Si ajabu kwa Watanzania kutokuwa na utamaduni wa kujisomea vitabu kwa vile vitabu ni gharama na uchumi hauwaruhusu. Uwepo wa maktaba moja tu kwenye jiji kubwa kama Dar es Salaam au Arusha na uhaba wa maduka ya vitabu ni changamoto za aina yake. Hivyo hata kwa wale wanaojua faida za kujisomea hulazimika kuishia kwenye magazeti.

Lakini, sasa Mungu bariki. Kwa wale wenye fursa ya kutumia teknolojia za kisasa wanaweza kuondokana na udhia huo na kujisomea kwa tani yao; bure. Project Gutenberg na Kobo kwa mfano zinafanya kazi hata kwenye simu za mkononi. Kwa hiyo, ile nusu saa isiyopangiwa bajeti ya matumizi kwa siku inaweza kutumika kufungua japo kurasa chache.

Hivi, kwanini tunahitaji utamaduni huu?

J. K. Nyerere ana haya ya kusema (1967):

… Books are a very important way to knowledge and to self-improvement; from them we can learn new ideas; new techniques of working and new methods. We can learn about the development of men in all its different aspects; we can broaden our understanding of other peoples and even of ourselves. All the experiences of mankind, all his discoveries and his inventions can be learned about through reading.

Ni kweli kuwa utamaduni huu wa kujisomea unajengeka vizuri zaidi iwapo utaanzia utotoni, lakini pia wanaoanza kupenda vitabu ukubwani si wachache. Kuna suala lingine linakuja, kati ya takriban vitabu milioni 130 (kwa mujibu wa Google) vilivyoko, kipi cha kusoma?

Wataalamu wanasema ni bora kupata mapendekezo kutoka kwa watu wengine kwanza kabla ya kujitosa kutafuta kitabu kama si msomaji wa kila siku.

Mimi leo napendekeza kitabu hiki hasa kwa wanawake: The Help

Kathryn Stocket: The Help

Kitabu hiki kinachoonesha mazingira ya mwanzoni mwa miaka ya 1960 katika mji mmoja huko Mississippi, Marekani, kinazungumzia zaidi uhusiano baina ya wafanyakazi weusi wa majumbani (mayaya) kwenye familia za watu weupe.

Licha ya kufanya kazi muhimu ya kulea watoto wa waajiri wao, wafanyakazi hao waliendelea kubaguliwa, na pia kunyimwa haki zao za msingi, kama kiwango sahihi cha mshahara pamoja na heshima wanayostahiki kama binadamu.

Sehemu kubwa ya kitabu hicho ipo katika mfumo wa makala za tajiriba za makazini mwao (tell-all-narratives); kitabu wanachoandika kwa kificho kwa msaada wa mwanadada kijana mweupe wakijua kuwa kitabadili maisha yao.

Licha ya kuwa hadithi hii imetungwa kuakisi maisha na hali ya ubaguzi wa rangi nchini Marekani, kitabu hiki kimenikumbusha hali ya wafanyakazi wengi wa ndani Tanzania.

Kweli hawabaguliwi kwa rangi yao lakini hawana muda maalumu wa kazi na mshahara wao ni mdogo mno. Kuna wanaozuiliwa kukaa meza moja na wenye nyumba, na wapo wanaonyanyaswa na kudhalilishwa kwa namna moja au nyingine.

Sitashangaa ikiwa mimi, wewe, yule kule, tulihusika au tunaendelea kushiriki katika huu udhalilishaji bila hata kujitambua.

Umeshawahi kujiuliza mfanyakazi wa ndani anafikiria nini?

Makala nyingine:

Previous ArticleNext Article
Steven was born and raised in Dar es Salaam, and moved to Germany for his studies. He graduated with a BSc. in Physics (Jacobs University Bremen), and then a MSc. in Engineering Physics (Technische Universität München). Steven is currently pursuing a PhD in Physics (growth of coatings/multilayers for next generation lithography reflective optics) in the Netherlands. He’s thinking about starting his own business in a few years; something high-tech related. At Vijana FM, Steven discusses issues critical to youths in Tanzania, music, sport and a host of other angles. He’s also helping Vijana FM with a Swahili translation project.

This post has 3 Comments

3
  1. kweli kabisa. Tena leo nikasikiliza mazungumzo kati ya mfanyakazi ya ndani na mlinzi wa nje. Kwa jinsi yule wa ndani alivyokuwa anamfokea yule wa nje, nikamkumbuka sana Malcolm X kuhusu ‘house nigger’ na ‘field nigger’

  2. Hapa naungana mkono kabisa na mwandishi wa makala hii, napenda vijana wa leo tuwe na mtazamo chanya na kizazi kijacho kwa kuwakuza watoto wetu katika mifumo wa kupenda kusoma vitabu mbali mbali na kuongeza natumuzi ya computer.

    Nafikiri tuliathiriwa sana na mfumo wa mababu na mababa zetu wa kuwasilisha taarifa kwa njia ya mdomo na hadithi. Lakini sasa umefikia wakati na inatupasa kuandika na kusoma

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Send this to a friend