Intersexions

Video hii fupi inaonesha maisha ya watu tofauti na jinsi yanavyoingiliana kwa namna moja au nyingine. Kila mtu ana hadithi yake ya kipekee, na kila mtu amefika alipofika kwa namna tofauti, lakini wote wapo njia panda. Njia panda maishani mwao sio tu zimetokana na maamuzi waliofanya wao binafsi, bali kutokana na maamuzi yaliyofanywa na watu wengine. Hii ni kama kuendesha huku umelewa. Kwenye ajali unaweza ukapona wewe, lakini akaja kufa mtu mwingine ambaye alikataa kunywa usiku ule, ili kujihakikishia usalama wake na wengine barabarani.

Wahusika wawili wa mwanzo wananikumbusha ule mjadala wa maharusi ni lazima kupima ukimwi kabla ya harusi, la sivyo hawatafungishwa ndoa. Sasa, mzunguko wa maisha unaooneshwa ndani ya video hii utakuacha ukitafakari…

Previous ArticleNext Article
Bahati was born and raised in Tanzania, and then moved to California to pursue his college education. He graduated in 2008 with a Bachelor’s Degree in Political Science and a minor in Sociology. Bahati expects to be doing his Masters in African Studies in the near future. He is currently working on starting a t-shirt business and a possible publication of some of his writings. One thing that Bahati cannot live without is music, specifically Hip Hop & Bongoflava which he argues are both the voice of the youth today, and is excited to look into how Bongoflava can be a source of further entrepreneurship among the youth in Tanzania. Bahati believes that Bongoflava can help to reduce poverty in Tanzania, as can a more collective effort among key players.

This post has 12 Comments

12
  1. The severity of this issue is well presented in this clip. I believe that the way a film is shot and edited can really impact how the message is received.

    Thanks for posting this, it was engaging and educational.

  2. @Hyperkei, hahaha…kumbe na wewe umeshasikia hayo maneno mtaani. Myth nyingine bwana, sijui watu wanataka kujipa moyo kuwa wanaweza kuendelea na ngono zembe, ili mradi tu sio na wanawake weusi.

    Lakini wengine wanaweza kusema, mentality ya namna hii inaonyesha ni jinsi tunavyojiona sisi wenyewe waafrika, alafu ndio sisi hao hao tunalalamikia dunia ya kwanza wanapotuzungumzia vibaya, na kutudhalilisha kwenye media zao..

  3. @Bahati

    Ebanaweee…..mi’ nlijua Ukimwi ni kama Malaria, gonjwa la tropiki ati.

    Hivi kwa nini hatuoni

    1. movie sinema ya Mzungu mwenye Ukimwi tokea Ukimwi uzagae Afrika?. (niliona filamu moja tu ambayo Mzungu Suzi anakuwa naUkimwi. Nafikiri ilikuwa 1989 hivi na ndio mara yangu ya kwanza kusikia kuhusu Ukimwi)

    Hatuoni 
    2. Kwenye soap operas za South Africa kwa mfano Isidingo, nchi yenye mchanganyiko wa watu, wanaopata Ukimwi mbona ni weusi tu?

    Hatuoni
    3. Matangazo kwenye cable channels kuhusu kuwepo kwa Ukimwi?

    Hatuoni
    4. Matangazo ya tv/mabango yanayoonyesha kuwa watu wasiokuwa weusi wanao Ukimwi/VVU? 

    Kama Ukimwi ulianza nchi za Magharibi mbona kwao sasa ‘hakuna’ kulinganisha nchi za kusini mwa jangwa la Sahara? Hatua gani zilichukuliwa?

  4. Hyperkei maswali mazuri..

    1. landa ningeanza na kukuambia utafute filamu inaitwa Philadelphia, ya Tom Hanks na Denzel Washington..it will be worth your time trust me, kama hujaiona bado.

    2. Pamoja ukimwi ulianza magharibu, ukweli ni kwamba, umetapakaa zaidi kwenye hizi nchi zinazoendelea, na mimi sidhani rangi ya ngozi inakitu chochote kuhusiana na hilo, zaidi ya umasikini ukiwa majo ya chanzo kikuu.

    3. Nadhani soaps kama Isidingo wanaonyesha watu weusi tu ndio wenye ukimwi, labda wanataka watu weusi waweze ku-relate na wahusika, kwani ni tatizo linalowakabili wao zaidi. Hapo am just assuming. Lakini assumption hiyo inakuaja baada ya mimi kuangalia movie kuhusu Genocide ya Rwanda, inayoitwa Shooting Dogs, excellent movie, WAY BETTER than that other movie, hotel rwanda.
    My point here is this, mpiga picha mmoja wa kike yeye alikuwa anapiga tu picha miili ya watu waliochinjwa, wa rika zote, bila kujisikia vibaya. Baadae mwenzake akamuuliza, mbona haonyeshi hisia zozote, yule mama akasema, alivyokwenda kupiga picha Bosnia kipindi kile cha mauaji yao, alilia. Sababu, kwani alivyoona wale wafu ambao walikuwa wazungu kama yeye, aliweza kuona yule mfu angeweza kuwa mama yake, lakini Rwanda, ni watu weusi, na sio kuwa ni mbaguzi, hapana, lakini hawezi ku-relate kihivyo.

    Sasa nadhani watu wakiona watu ambao wanawafanania wao, inawagusa zaidi. Ukionyeshwa mhindi anayekufa na ukimwi, hujioni wewe, bali unaona mtu mwingine, so its kinda hard to relate. Tutake tusitake, we’re visual people.

  5. 1. Michezo ya West ikionyesha Ukimwi mara nyingi ina relate na watu ambao ni homosexuals kama kwenye hiyo Philadelphia.
    So kwa akili za watu wengine wanawake wa West walio heterosexual hawana VVU.

    2. Unasema umaskini unachangia kwenye watu kupata Ukimwi, hebu tufafanulie kidogo hapo. Mie ningeamini ukosefu wa maadili, na ukaidi ndio uliotufikisha hapo tulipo zaidi ya huo umasikini.

    3. Kama tumeamua kutangaza biashara ya utalii hivi tunavyotangaza sasa, lazima watu wafahamishwe kuwa hata Mzungu anaweza kuwa na Ukimwi japokuwa wanaoweza kuathirika kutoka kwa Watalii ni watu wachache. (hata ikiwa ni mtu mmoja aliye kwenye risk,serikali inapaswa kumlinda. Pia huyo mmoja akiambukizwa bila kujijua anauwezo wa kuambukiza wengine na wengine, na chain ikawa kubwa kama tulivyoonyeshwa hapo kwenye film)

  6. Hilo ni kweli, lakini sasa ndio unabidi uangalie hiyo filamu ilitengenezwa kipindi gani?, alafu uangalie ukimwi kipindi hicho ulipoanza kufaamika, waadhirika wengi walikuwa homosexuals, ndio maana ukaitwa ugonjwa wa mashoga, na hata baadhi yao kufikiria wao ndio chanzo..

    Pili, ukiangalia kwenye jamii ya watu weusi (wamarekani weusi) asilimia kubwa iliyoadhirika ni wanawake. Wanaume ambao wameadhirika, hutashangaa ukikuta ni wale ambao wanaitwa down low brothers, in short..they are homosexuals..so it all makes sense.

    Kwenye suala la utalii, ninakubaliana na wewe kabisa, Serikali inajukumu la kuelimisha watu kuhusu hilo. Lakini unadhani wahalijui hilo, unadhani hizi Serikali halijui kuwa kuna pedophiles wanaokuja kuharibu watoto, linajulikana hilo. One, hao pedophiles wanapenda nchi masikini, kwani tunataka sana hao watalii, hivyo sheria zetu zimelegezwa, na hata hivyo, tuko willing ku-turn a blind eye so we can make a buck, in the name of foreign currency.

    Mfano wa pili wa suala la umasikini ni hili la Serikali kuwa na uwezo wa kuwa na programs za kufundisha watu. Hakuna hizo programs kiasi hicho, hizo shule zenyewe mpaka leo ni kasheshe, ndio hilo la kuanzisha programs za kufundisha watu..i doubt that.

    Juzi kulikuwa na habari ya wamasai wana kuosha condoms zao na kuazimana. Hili halikunishtua, kwani kuna mkoa fulani Tanzania, watu walikuwa wanatumia ile mifuko milaini ya blue ya plastiki. Hapo kuna mawaili, ni either hakuna condom za kutosha, au watu hawana uwezo wa kununua hivyo kujikinga. Kama mtu anaishi under a dollar a day, your condom is not a priority. Lakini najua kuna hili la condom za bure, jiulize sasa, inawezekana zipo, lakini watu wakishapewa, wanazifanyia mradi, tunarudi tena kwenya umasikini, na hali ngumu ya maisha, hivyo kila kitu kwetu ni dili. Mifano ipo mingi tu…

    Hili la ukosefu wa maadili linanifurahishaga sana, kwani nikama tunakimbia responsibility zetu na kulaumu watu wengine. Lakini sikatai moja kwa moja kuwa, ufa kwenye maadili unachangia sana, lakini maadili hayo hayo katika baadhi ya mila zetu zinachangia.

    Kwa mfano, ukeketwaji, sijui kama mangariba hutumia nyembe moja kwa msichana mmoja na kutupa, au hiyo moja kwa wasichana wote.

    Lipo hili la kuridhi mke wa nduguyo, kwakuwa ni mila basi tena hakuna mjadala, hakuna kuuliza kwani kaka alikufa na nini, au kukataa kwa kuhofia. Lipo hilo la kuwa na wake wengi, polygamy….mtu akiwa ameoa wanawake ishirini, kirusi kikaingia, basi kila mtu anagawiwa share yake kwenye mzunguko, haponi mtu hapo.

    Je hili la kutahiri wanaume. Kuna tafiti ambazo zinaonyesha, mwanaume akipitia jando, inapunguza uwezekano wa kuambukizwa virusi vywa ukimwi. Lakini pamoja na hilo, zile mila ambazo jambo mwiko (wajaluo kwa mfano), hakuna atakayepitishiwa nyembe, kwasababu mila imesema hivyo, na sisemi kuwa watu wajaluo wote hawajatahiriwa, hapana…

    Wanawake, moja kati ya kundi masikini katika jamii zetu. Kupata kazi, hongo ya ngono, ukimkatalia bosi, unafukuzwa kazi au hupewi ile promotion. Ukiwa kwenye kundi lile la wengi ambao hawakwenda shule, kwasababu mila zetu zinasema kumsomesha msichana ni kupoteza muda. Sasa hapo sasa, mwanamke anakuwa tegemezi kwa mume wake. Hana maamuzi, na mwanaume ndio huyo ni kulala na vibinti, na ma-bar maid..lakini mke utakimbilia wapi, huna kipato chako, na ataanza wapi kumsihi mme wake avae condom au hata waende kupima, hilo ni a BIG NO NO..

    Feminist/ feminism na hili la Independent woman is a Western thing, na wapo watakaosema linavunja miko ya maadili yetu. Lakini that is a western thing, na wale independent career women wako free kujiamulia, since they have their own income, so they wont be pushed around. Mtu kitu, ukiwa masikini you lose your right to speak, ndio maana wanasema, you cant be a begger and a chooser….

  7. Mbali ya yote hayo bado ninaamini kuwa kuna tatizo la kimaadili linaochangia asilimia kubwa ya maambukizi pia hasa ukizingatia kuwa katika kundi la waathirika, wenye uwezo wa kifedha na elimu wamo wengi.

    Chukua tatizo la nyumba ndogo kwa mfano. Watu wanafika kuzaa huko nyumba ndogo (ambayo hujui inatunzwa na wangapi) ikimaanisha hakuna matumizi ya protection. 

    Watu wanaokwapua tu mabar maid wakiwa wamelewa chakari hawawezi kutumia protection. Kundi hili wamo watu wa aina zote pia.

    Watu wanaotumia protection siku mbili za mwanzo, baada ya hapo wakaacha kwa kusema weshamuamini partner kabla ya kwenda kupima. Akiachana nae akipata mwengine, routine ni ile ile pia.

    Na hata hiyo rushwa ya ngono ni ukosefu wa maadili kwa jamii nzima. 
    Mwanamme aliye kwenye nafasi asingeomba rushwa hiyo asingepewa, na wanawake wasingekuwa wakitoa hatimae wasingeombwa. 
    Hii tabia ya jamii kufumbia macho suala hili ndio nayo inazaa mabalaa mengine.

    Wanafunzi wa kike kutunzwa na watu wazima. Sio kama anashida atakosa kula, lakini anakuwa nae ili kupata pesa za kutumia kwenye mambo yasiyokuwa lazima. Huku pembeni akiwa na jamaa wa kwenda nae mitoko. 
    Wapo wenye kujishuku kama sio kujijua kuwa ni waathirika lakini wakaendeleza ngono bila protection. 
    Niukosefu wa morals tu na sheria iko kimya kwenye hilo. 

  8. @Anon..mchango mzuri, lakini swali langu ni nini kifanyike kurudisha hayo maadili sasa. Manake kila siku tunazungumza kuhusu mmomonyolo wa maadili, lakini ni nini kifanyike ili tuweze kurudi kwenye mstari?

    Hao wanaotumia condom siku mbili za mwanzo, alafu wanaacha, je unadhani ni ujinga wa makusudi, au ni ukosefu wa elimu sahihi kuhusu hili suala la kinga na ukimwi.

    Hao wanafunzi ambao wanatunzwa na watu wazima, nini tatizo?….hudhani ni umasikini?, fikiria, kama huna fedha kwenda shule ni mgogoro, kama umetoka kwenye maisha duni. Alafu, angalia kwanini kuna shule ambazo maudhurio ya wanafunzi ni hafifu, utakuta kuwa, suala la njaa liko juu ya moja ya sababu.

    Kuna shule ambazo wanatoa chakula kwa wanafunzi, to boost attendance. Najua hili linagusia zaidi shule za awali, lakini nimetaka tu uone picha ni jinsi gani mambo madogo ambayo tunaweza kutoyafikiria ndiyo ambayo yanayoleta matatizo makubwa…

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Send this to a friend