Siku 90 Zinatosha Kukujengea Mazoea ya Ushindi

Watu wengi tunaishi kutokana na mazoea ambayo yamejenga tabia ambazo zinatufelisha katika mishe zetu nyingi. Kwa bahati mbaya tunashidwa jinsi ya kuyashinda haya mazoea na kutengeneza tabia ambazo zitatujengea misingi ya ushindi katika mishe zetu.

Kuna kitabu kimoja niliwahi kusoma, kwa bahati mbaya nimesahau jina la kitabu hadi na la mwandishi, ila sio mbaya maana ujumbe ambao niliupata kwenye hicho kitabu mpaka leo bado upo kichwani.

Katika hicho kitabu ambacho nimekisahau kuna ujumbe ambao nahisi kamwe sitausahau.

Mwandishi wa kile kitabu anasema ” Mazoea hujenga tabia na tabia inapokomaa akili inaacha kujihusisha na hayo mazoea uliyojijengea”, kama umejitengenezea mazoea mazuri basi una bahati, ila kama umejitengenezea mazoea mabaya na akili yako imekususa katika kudili na tabia zako hizo, basi una unahitaji msaada wa haraka.

Kama hujanielewa ipo hivi, kama una mazoea ya kuiba na mazoea hayo yakikomaa, yanakuwa tabia yako. Hapo ndipo taratibu akili itaanza kuacha kudili na tabia hiyo, kwahiyo ukifika sehemu na ukaona kitu kimekaa pekee, akili itajitenga na kujiweka pembeni na gafla utajikuta umeiba hicho kitu. Ukimaliza, akili yako itarudi na hapo ndipo majuto yakapoanza.

Kwa wale wavivu ambao tuna mazoea ya kusema tunaanza kesho kupiga mishe mishe kama kufungua biashara, na kesho ikifika tunaghairisha tunapanga siku nyingine. Mazoea yakikua yanazaa tabia ambayo akili itasimama kudili nayo na itakuacha upambane na hali yako, hapo ndio utahisi kama umerogwa kwa mipango yako isiyotimia, kumbe ni tabia yako tu ndio inakuchelewesha.

Kuna wengine tunajijua tuna uwezo wa kufaulu kabisa kama tukikomaa na kusoma kwa bidii, ila kutokana na mazoea yetu ya kulala na akili zetu zimetususa zinatuacha tuendelee kulala, mwisho wa siku tunafeli tena. Tukishafeli tunapanga tena na kupania kabisa kuwa mitihani ijayo itanikoma kwa msuli nitakopiga, ila kutokana mazoea yetu ya kulala mpaka mitihani ijayo inafika inatukuta bado tumelala. Hivyo ndivyo akili inavyotususa.

Nani ameshakata tamaa kwa tabia ambazo ameshindwa kuziacha? Nani ana amini anaweza kufanikiwa zaidi kama akiacha hizo tabia na kuwa serious kwa kile anachotaka kufanya au anachofanya?

Wengi wetu tumeyafanya mazoea yetu kuwa tabia, na kwa bahati mbaya tabia hizo zimekomaa kichwani mwetu na akili yetu imesusa kabisa kutuambia kuwa tunakosea kwa tabia zetu za kipuuzi ambazo zinatufelisha.

Labda nikwambie kitu, akili inajengwa kutokana na mazoea yetu. Na mazoea yakikomaa huwa tabia, na tabia ikikomaa akili inasusa kupambana na tabia hizo hivyo inatuacha tucheze ngoma ambayo tumeizoea..

Ogopa sana akili yako ikikususa kwa mazoea mabaya unaoyafanya. Hapa ndio utashangaa kila unachofanya ufanikiwi, Hapa ndio utashangaa kila ukipanga mipango yako hujui hata inakufa vipi.

Kwa akili na upuuzi wangu naamini mazoea na tabia unayajenga wewe mwenyewe. Na inachukua wastani wa siku 90 au miezi mitatu kwa mtu kutengemeza tabia mpya.

Anza leo kujenga tabia mpya ambazo zitakufanya ufikie malengo, shindana na uvivu wako, shindana na mazoea yako, shindana na tabia yako.

Na baada ya miezi mitatu utakuwa na tabia mpya, utakuwa na mazoea mapya na utakuwa na akili mpya kutokana na mazoea uliyoanza kujijengea kuanzia leo.

Ukianza diet leo, matokeo utaanza kuyaona baada ya siku 90, Ukianza kuandika kitabu leo, utakuwa upo kurasa ya 300 baada ya siku 90. Ukianza kujifunza kitu leo, baada ya siku 90 utaweza kusimama mwenyewe.

Hivyo ukijijengea mazoea mapya ndani ya siku 90, basi hakika utakuwa na tabia mpya. Tabia yako haiwezi kubadilika ndani ya siku moja, anza kuibadili leo kwa kutengeneza mazoea mapya na uje unipe mrejesho baada ya siku 90.

Previous ArticleNext Article
Leonce Godfrey has been in the field of Digital media and digital marketing with more than 3 years experience working in various capacities with highly reputable companies and organizations. He is writer, storyteller, content creator, photographer and journalist by professional. He simply amazing.

This post has 1 Comment

1

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Send this to a friend