Maswali matano na Alfan A. Kiyanga

Alfan Athuman Kiyanga ni mchezajia wa timu ya Taifa ya walemavu na klabu ya LSL. Pia anamiliki tuzo ya Mfungaji Bora ligi kuu Tanzania bara pamoja na michuano ya Afrika kwa watu wenye ulemavu.

1. Umeanza lini kucheza mpira wa miguu?

Nimeanza kucheza soka toka nikiwa darasa la 5 katika shule ya msingi Salvation Army. Nilikuwa na mapenzi na mpira toka utotoni kwangu, pia nilikuwa na ndoto siku moja niwe mchezaji mkubwa hapa Tanzania.

2. Kwanini ulichagua kucheza mpira wa miguu?

Nilichagua kucheza soka kwa sababu napenda kucheza mpira toka nikiwa shule na ndio kitu ambacho kilikuwa kinanivutia zaidi kwa wakati huo.

Kulikuwa na baadhi ya wachezaji wananivutia sana kipindi hicho nikiwa bado mdogo, hivyo nikajikuta na mimi napata msukumo wa kuingia kwenye kucheza mpira.

3. Ulipatwa na ulemavu ukiwa na umri gani? Vipi ulikuwa tayari unacheza mpira?

Nilipata ajali mwaka 1999 nikiwa na miaka saba, na ndio nilikuwa nimeshaanza kucheza mpira ila jambo hilo halikufanya niache kucheza mpira.

Niliendelea kucheza mpira, maana ni kitu ambacho nilikuwa nakipenda na sikuwa tayari hali niliyoipata iweze kusimamisha ndoto zangu.

4. Ulijisikiaje kuwa Mfungaji Bora wa michuano ya Afrika?

Nilijikisikia furaha sana kuwa Mfungaji Bora wa Africa kwani hata mimi mwenyewe sikutegemea kama nitakuwa mfungaji bora.

Mashindano yalikuwa magumu sana na isitoshe sisi Tanzania ndio mara ya kwanza kushiriki katika mashindano makubwa ya Africa kama yale.

5. Nini matarajio yako kwenye Kombe la Dunia na mipango yako ya hapo baadae?

Matarajio yangu kwenye Kombe la Dunia ni kuwa mfungaji bora wa Kombe la Dunia na pia bado napambana ili niweze kufikia ndoto yangu ya kucheza kwenye ligi kubwa duniani kama nchini Uturuki na Uingeleza.

Pia naomba kama kuna mtu anaweza kunitafutia timu ya kucheza kwenye ligi hizo niko tayari kufanya kazi nae kama wakala wangu.

“Pia naomba kama kuna mtu anaweza kunitafutia timu ya kucheza kwenye ligi hizo niko tayari kufanya kazi nae kama wakala wangu”.

Kwa mawasiliano na taarifa zaidi unaweza tembelea ukurasa wake wa Instagram kwa jina @alfanmajani10

Previous ArticleNext Article
Leonce Godfrey has been in the field of Digital media and digital marketing with more than 3 years experience working in various capacities with highly reputable companies and organizations. He is writer, storyteller, content creator, photographer and journalist by professional. He simply amazing.

This post has 1 Comment

1

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Send this to a friend