Maswali Matano na Chausiku Foundation

Chausiku Foundation ni taasisi iliyoweza kugundua mashine aina ya “ATM” ambayo inauwezo wa kutoa pedi kwa ajili ya matumizi ya watoto wakike wakiwa shuleni.

Bungire Hussein (kulia) ni mwanzilishi shiriki na msimamizi miradi katika taasisi ya Chausiku Foundation.

Mpaka sasa wameweza kutengeneza mashine moja ambayo imefungwa katika Shule ya Sekondari ya Mama Salma Kikwete, huku wanafunzi zaidi ya 100 wakinufaika na huduma hii.

Tulipata wasaa wa kuwatembelea na kujifunza mambo kadhaa kutoka kwao.

1. Wazo la kutengeneza Chausiku mlilipata wapi na kwanini mliamua kuita ugunduzi wenu Chausiku?

Wazo la mashine ya Chausiku lilianzia chuoni ambapo moja ya kigezo cha kumaliza mwaka wa nne ni pamoja na kutengeneza project yenye kutatua matatizo yanayozunguka jamii yetu. Kutokana na ilo wazo lilitoka kwa mwana kikundi mmoja na kuamua kutengeneza mashine ambayo itasaidia kutatua tatizo la ukosefu wa pedi mashuleni. Kikundi kilitembelea shule kadhaa kwa ajili ya kupata taarifa ya awali namna gani mashine hio itawasaidia na kupata data kamili.

Mashine hio ndipo ikatengenezwa na kupitia maboresho mbalimbali kadri siku zinavyoenda iliendelea kuwa bora.

Jina la Chausiku lilianzia chuoni ambapo tulitaka jina ambalo litawakilisha asili, kwa maana ya Tanzania (Africa) na kiswahili pia. Hivyo Chausiku lilipendekezwa na baadae kupata umaarufu mkubwa chuoni hivyo likabaki kuwa kama lilivyo.

2. Changamoto gani mliipata na ipi ambayo bado mnaipitia katika ugunduzi wenu?

Changamoto kubwa ya ugunduzi huu ni pesa (funds) ya kuendesha mradi uwafikie na wengine wengi. Sisi kama waanzilishi tunatamani sana uvumbuzi huu uwafikie maelfu na maelfu ya wanafunzi Tanzania.

Hilo ndio lengo kuu iliotupelekea kufungua NGO, ili tuweze kushirikiana na wadau wengine wengi kutatuta changamoto ya mtoto wa kike shuleni. Kwa hivyo wadau kama watu binafsi, makumpuni, mashirika yasio ya kiserikali na mengineyo ndio walengwa hasa wa kutushika mkono katika kufanikisha project hii.

Sisi kama wanakikundi kwa michago yetu ya ndani tuliweza kuwaonesha watu kitu gani tunacho na kitafanyaje kazi na ndicho tulichokifanya katika shule ya mama Salma Kikwete. Hivyo basi mahitaji ni mengi na shule ni nyingi sana. Tunahitaji support kutoka kwa wadau.

Wote wanakaribishwa.

3. Ni nini mipango na malengo yenu juu ya ugunduzi wenu katika kusaidia watoto wa kike?

Mpango wetu ni kuwafikia wanafunzi wengi zaidi ndani ya Tanzania. Kwa mwaka 2021 tumejiwekea malengo ya kufikisha mashine katika shule 100. Hio ndo target yetu.

4. Kama akitokea mtu akiomba kuwasaidia, mngependa musaidiwe nini?

Msaada pekee ni ambao ungetusaidia sisi kukamilisha lengo letu ni gharama za kuweza kupata mashine zingine. Cost kubwa kwetu ipo kwenye kutengeneza mashine. Pia yeyote ambae anacho za kutusaidia pia hatuwezi mzuia maana lengo letu ni kumsaidia mtoto wa kike ili aweze kupata hitaji la pedi akiwa shuleni.

5. Mnaiona wapi Chausiku baada ya miaka mitano ijayo?

Baada ya miaka mitano tunamuona Chausiku akiwa katika kila shule na sehemu mbalimbali za mkusanyiko wa watu akisaidia wanawake kukabiliana na dharura ya hedhi wanapokua katika shughuli zao.


Fuatilia Chausiku foundation Instagram na Twitter.

Previous ArticleNext Article
Leonce Godfrey has been in the field of Digital media and digital marketing with more than 3 years experience working in various capacities with highly reputable companies and organizations. He is writer, storyteller, content creator, photographer and journalist by professional. He simply amazing.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Send this to a friend