Maswali Matano na Nipe Dili

Mussa ni mdau wa maendeleo hasa kwa vijana na wajasiriamali. Amekua akishiriki shughuli tofauti za kimaendeleo kupitia kazi zake rasmi na kujitolea.

Kwa sasa ni meneja miradi na kazi za kampuni iitwayo Unleashed Africa iliyopo Dar es Salaam. Amekua akijitolea kama meneja mradi wa Ujuzi kwa Vijana na Maendeleo uliopo chini Global Shapers Community Dar es Salaam Hub.

Mussa ni mchumi aliyebobea katika sera za uchumi na mipango, utafiti, content creation na monitoring and evaluation. Pia ni mshairi na msanii wa sanaa ya uchoraji kwa penseli, rangi na digitali na leo ametujuza mambo matano tusioyajua kuhusu NipeDili.

“Nipe Dili” ni nini?

Nipe Dili ni kipindi kinachotoa nafasi kwa vijana na wajasiriamali jamii wa kitanzania kukutana na wawekezaji ambapo huweza kupata uwekezaji kutokana na namna wanavyoweza kuzielezea biashara zao.

Vijana hawa hupitia mafunzo ya kibiashara kuweza kuzichanganua vizuri na kujua namna wanaweza kuzikuza kabla hawajapata nafasi ya kuzielezea mbele ya wawekezaji.

1. Wazo la kuanzisha Nipe Dili lilitoka wapi?

Wazo la Nipe Dili lilitokana na upungufu ulioonekana katika programu ya ujasiriamali inayoitwa Tujenge TZ Innovation Challenge. Upungufu huo ulikua ni kukosekana kwa uwekezaji kwa wajasiriamali waliopitia programu hiyo.

2. Yapi ni malengo na mkakati wa Nipe Dili kwa vijana?

Lengo la Nipe Dili ni kuwakutanisha vijana wajasiriamali jamii na fursa za uwekezaji kutoka kwa wawekezaji tofauti ndani ndani nje ya nchi.

Tunalenga kubadilisha mitazamo na namna mfumo mzima wa ujasiriamali unafanyika hapa Tanzania. Hii ni kwa wajasiriamali na wawekezaji kiujumla.

3. Mnaweza kuwafiki kwa njia gani watu mliokusudia kuwafikia?

Njia kubwa kabisa kwa sasa ni mitandao ya kijamii. Lakini pia tuna uhusiano na washirika kadhaa ambao wanahusika na shughuli za wajasiriamali na uwekezaji.

Washirika hawa hupendekeza wajasiramali wanaoonekana wanafaa kupata uwekezaji kupitia Nipe Dili, nasi huwapitisha kwenye mchujo na kupata wale wanaoonekana wana uwezekano mkubwa wa kupata uwekezaji.

4. Mnapitia changamoto gani kubwa inayowakwamisha kufikia malengo yenu?

Changamoto kubwa zaidi hizi: Wawekezaji (Angel Investors) ni wachache sana na watanzania wengi wenye uwezo huo bado hawajaelewa au hawana ufahamu juu ya aina hii ya uwekezaji na faida zake.

Wajasiriamali wengi hapa Tanzania hawana mipango madhubuti ya uendeshaji wa biashara zao. Hili linapelekea biashara nyingi kufa au kuishia katika hatua za mwanzo za biashara (startup). Biashara nyingi zilizotuma maombi ya kushiriki zilikua na hili tatizo.

5. Ni nini mnaweza shauri vijana na fursa iliyopo katika Nipedili kama platform kwa ajili yao?

Nipe Dili ni jukwaa wazi kwa kijana yeyote mwenye biashara au wazo la biashara lenye uhalisia na uhakika wa kutengeneza faida.

Kingine ni kuwa ubunifu pekee hauwezi kufanya biashara ifanikiwe. Ni lazima mjasiriamali ajifunze namna ya kuendesha na kukuza biashara yake ili asiingie kwenye mtego wa biashara dumavu.

Nipe dili kama jukwaa huru kwa vijana linaweza kuwajengea uwezo katika uelewa wa biashara na ushindani wake.


Unaweza kutembelea YouTube channel @NipeDili kujionea vipindi vyao vyote. Pia unaweza tembelea kurasa zao za kijamii Instagram @NipeDili na Twitter @NipeDili.

Previous ArticleNext Article
Leonce Godfrey has been in the field of Digital media and digital marketing with more than 3 years experience working in various capacities with highly reputable companies and organizations. He is writer, storyteller, content creator, photographer and journalist by professional. He simply amazing.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Send this to a friend