Maswali matano na Ezytrade Africa

EzyTrade Africa ni platform ambayo unaweza kufanya manunuzi ya bidhaa mbalimbali ukiwa nyumbani na simu yako. Pia Ezytrade inawapa uwezo wafanyabiashara wa bidhaa mbalimbali kuweka bidhaa zao mtandaoni hasa kwenye platform ya Ezytrade ambayo itamkutanisha wateja mbalimbali wanaotaka na kuulizia bidhaa hizo.

Unaweza kujiunga kwa kutembelea www.ezytrade.africa.

  1. Wazo la kuanzisha lilitoka wapi na kwanini iliitwa Ezytrade?

Sisi waanzilishi wa Ezytrade ni mkusanyiko wa vizazi ambao kati yetu tumezaliwa vijijini na wengine wamezaliwa kwenye majiji kama Dar es Salaam. Na tumesoma masuala mbalimbali ya maendeleao ya kibiashara na masuala ya TEHAMA. Kwa muunganiko wetu tuliona kuna umuhimu wa kufanya kitu ukizingatia ukweli kwamba maendeleo ya biashara zetu barani Africa ni duni.

Hivyo tuliamua kutengeza kitu ambacho kitakuwa kichocheo cha kuziba nafasi iliyopo kati ya raslimali watu, rasilimali vitu na fursa zilizopo mbele yetu.

Kwa maendeleo ya TEHAMA yanavyokuwa kwa kasi, tuliona kuna umuhimu wa kuhamia kufanya manunuzi ya vitu mtandaoni.

Basi tuliamua kuja na “digital trade ecosystem” ambayo itarahisisha ufanyaji wa biashara na kuipa jina “Ezytrade” ikiwa na maana kuwa biashara imefanywa kuwa rahisi.

2. Mna mkakati gani wa kuweza kuwavutia watu wengi zaidi ambao watafanya manunuzi katika platform yenu?

Mali bila daftari upotea bila habari, digital trading platforms zinaweka ukaribu sana kati ya muuzaji na mteja. Kwa mfano historia ya manunuzi, upendeleo wake, maoni ya kila mteja n.k.

Kwa ufupi kila muuzaji anakuwa ameunganishwa na mteja wake moja kwa moja.

Ukaribu huu tulioutengeneza kati ya muuzaji na mteja wake tunaona utaimarisha biashara za wateja wetu, ukaribu huu utaongeza na wateja na hivyo kuongeza mauzo. Kazi yetu ni kuonyesha wateja wetu kuwa duka-mtandao lako maana yake ni unapeleka duka lako lilioko Kariakoo kwenye kila sehemu mteja wako yupo na pale wanapoweza kutumia simu zao.

Kama muuzaji ana simu na mnunuzi ana simu kwanini wasiunganishwe?

3. Mapokezi yamekuwa vipi ikiwa hii ni kitu kipya kwa Watanzania wengi?

Tunashukuru wadau wote wa digital trading platforms zetu wametupokea kwa imani kubwa sana.

Kila anayeuza bidhaa au kutoa huduma sasa anajua kuwa wanunuzi wengi sasa wanapenda kupata maelezo mazuri ya bidhaa au huduma na kusikia wateja waliotangulia kutumia hizo bidhaa au huduma wanasemaje.

Wajasiriamali wengi wametambua hilo tayari kazi yetu ni kuwapa muongozo nzuri na kuwatengenezea mazingira ya kuuza na kutoa huduma kwa njia za mtandao.

4. Mnapitia changamoto gani kubwa inayowakwamisha kufikia malengo yenu?

Changamoto hazikosi.

Baada ya kumaliza kujenga mfumo sasa ni kazi ya kuingiza taarifa za bidhaa. Wajasiliamali hawajaandaa taarifa nzuri kuhusu bidhaa zao. Maelezo waliyonayo kila ukiyaangalia unaona wanauza kidogo na bidhaa zao ni bora.

Tunahitaji vijana wasomi hasa kwenye vitengo vya masoko na matangazo, copywriting ambao wanaweza kuchukua jukumu la kutangaza bidhaa zetu. Pia mrejesho tunaoupata kila tunapotuma sample za mazao yetu ya kilimo kama spices, nuts, oil seeds, n.k. ni mrejesho mzuri sana lakini bado hajuwa na uwezo nzuri wa kutunza kumbukumbu hususani maoni ya wetu juu ya huduma zetu.

5. Ni nini mnaweza shauri vijana na fursa iliyopo katika platform ya EzyTrade?

Hili ni swali muhimu sana.

Digital Trading Platform zetu zime-design-iwa juu ya nguzo kadhaa; mojawapo ni vijana. Platforms zetu zote zinatumia mawakala. Kwa hiyo vijana wanaweza kuwa Activators, Digital Sales Agents, Order Fulfillment Agents, Brand Ambassadors, Advocates and Influencers, kwenye uendeshaji wa Fulfilment and Collection Centres, Webshops Attendants, Digital Marketing na maeneo mengi kadri ya utashi, utayari na matamanio ya mtu.

Huko mbele kila kitu kitakuwa kuhusu mtandao, ni suala la kuelewa uko wapi kwenye ramani ya utandawazi na mtandao na nini unaweza kuchangia ili kusukuma gurudumu.

Sisi kazi yetu ni kufundisha na kusimamia kila anayetaka kujiunga kwenye uchumi wa mtandao. Tuna imani sana na vijana wa bara hili.


Unaweza kujiunga na Ezytrade africa kwa kutembelea www.ezytrade.africa na ukafanya manunuzi mbalimbali mtandaoni au kujiunga kama mtoa huduma kwa kuhamishia duka lako mtandaoni.

Pia unaweza kutembelea kurasa zao za kijamii Facebook @Ezytrade Africa na Instagram @Ezytrade Africa.

Previous ArticleNext Article
Leonce Godfrey has been in the field of Digital media and digital marketing with more than 3 years experience working in various capacities with highly reputable companies and organizations. He is writer, storyteller, content creator, photographer and journalist by professional. He simply amazing.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Send this to a friend