Maswali Matano na Josephine Mumwi

Josephine Mumwi ni mwanamitindo Mtanzania anayefanya vizuri katika anga za kimataifa kwasasa. Licha ya umri wake wa miaka 24 tu tayari amefanikiwa kusajiliwa na Agency kubwa ya The Circle Model Management ya mji wa Capetown nchini South Africa na nyngne Fabulous Models dot com iliyopo Johanesburg South Africa.

Vilevile ana Scouting Agency yake @house_of_vaazi (ikiwa kama kurudisha kwa jamii). Josephine ambaye hupenda kujiita “Barbie” kutokana na umbo lake dogo, ambalo ukimuangalia utaweza kuhisi ana miaka 16, alianza kufanya sanaa hii ya modeling mwaka 2016 wakati akiwa mwaka wa kwanza chuoni.

Kabla ya kujikita katika modeling, “Barbie” alikua film actress na miongoni mwa mashindani aliyofanya ni pamoja na TV series ya “TAUSI Likokola’s African Princess Model Search”, kitu ambacho kilimvutia zaidi katika tasnia ya fashion.

Josephine ni mmoja ya wanamitindo ambae ameweza kutumia mitandao ya kijamii vizuri sana katika tasnia yake, hivyo tulipata kujua mambo matano ambayo Josephine ameyajibu kuhusu matumizi ya mitandao ya kijamii kwake ilivyo.

1. Mitandao ya kijamii imekusaidia vipi katika ukuaji wako mpaka kuwa model wa kimataifa?

Mitandao ya kijamii hususa ni Instagram , Youtube, Facebook na Whatsapp naipa nafasi kubwa sana katika kunifikisha hapa nilipo sasa.

Nimeweza kujitambulisha kimataifa na kupata agency Africa Kusini kupitia mitandao ya kijamii baada ya kupenda kazi zangu nazofanya ambazo waliziona kupitia mitandao ya kijamii.

Pia nimeweza kupata kazi mbalimbali za mitindo na kutumia mitandao ya kijamii kama ofisi yangu ya kwanza.

Nimeweza kuajiri vijana wenzangu wakitanzania kupitia scouting agency yangu ya @house_of_vaazi na kuendelea kuwasiliana nao nikiwa South Africa na kuwapa kazi Tanzania.

Na kupitia mitandao yakijamii, nimefungua Youtube channel yangu mpya, inayo nisaidia kufundisha wanamitindo wadogo wa Africa Mashariki kwa lugha ya Kiswahili nikiwa nchini South Africa.

Mitandao ya kijamii imenipa nguvu ya kujitangaza na kufahamika na watu wengi duniani. Bila kusahau kipindi cha Lockdown nchini South Africa, ofisi zetu za mitindo ziliendelea kufanya kazi kupitia mitandao yakijamii.

2. Uliweza vipi kusimamia na kuendesha mwenyewe mitandao yako ya kijamii mpaka kufikia hapo?

Kama mwanzo nilivyo sema, mitandao ya kijamii imekuwa ofisi yangu ya kwanza. Mimi ni miongoni mwa watu ambao nahakikisha kuwa online muda wote, kwani natarajia jumbe za kazi kupitia mitandao ya kijamii.

Vilevile naendesha shughuli zangu zilizopo mbali na mimi kwa sasa (Tanzania) kupitia mitandao ya kijamii. Hivyo ni kama ofisi kwangu.

3. Ni changamoto gani kubwa uliyowahi kuipitia/bado unaipitia kama model katika safari yako ya kujitangaza kwenye mitandao ya kijamii?

Baadhi ya watu wanaelewa vibaya picha ninazo tuma katika mitandao ya kijamii kama mwanamitindo. Wanahisi napost ili kupelekea fikra zao katika mapenzi.

Kupata comment mbaya za matusi kutoka kwa watu wasiojulikana ni kawaida na ninachukulia kama changamoto nyingine tu kazini.

Changamoto nyingine ni watu kuingilia maisha yangu binafsi yasiyo wahusu, kutaka kujua zaidi ya ninavyo post mitandaoni au kutengeneza story zao fake kuhusu mimi.

4. Ni mafanikio gani makubwa umeyapata kupitia mitandao ya kijamii?

Nimeweza fikisha ujumbe wa kisanaa kwa jamii yangu kupitia mitandao ya kijami na pia nimeweza kutengeneza scouting agency yangu (@house_of_vaazi) nikishirikiana na ma stylist wakubwa Tanzania akiwemo Vaazi Stylist na Deo Stylist, inayo wawezesha wanamitindo wadogo wadogo kupata agency nje ya Tanzania na baadhi kufanya kazi mbalimbali za mitindo nchini Tanzania.

Vilevile nimeweza kupata deals mbalimbali za mitindo na matangazo kupitia mitandao yakijamii.

5. Kwa wanaotamani kufika hapo ulipo wewe, ni kitu gani unawaambia wasikifanye katika mitandao ya kijamii kama models wanaochipukia?

Wasikatishwe tamaa na mitazamo hasi ya jamii juu ya picha za mitindo wanazo zituma mitandaoni.

Wasipotoshwe na baadhi ya watu wanaoedit sana miili yao na kutuma picha mitandaoni, wajipende walivyo.

Na wasiishi kwa kuiga, hii ni kwasababu wanamitindo wengi wadogo hukata tamaa haraka kutokana na kutamani maisha ya watu fulani mitandaoni ambayo hakuna mtu mwenye uhakika kwamba hayo maisha yakifahari wanayoishi ni yakweli au ni picha tu zilizo fanyiwa photoshop.


Unaweza wasiliana na Josephine na kuangalia kazi zake kupitia Instagram page yake kwa jina @Josephine.mumwi na vilevile pitia YouTube channel yake JosephineMumwi.

Previous ArticleNext Article
Leonce Godfrey has been in the field of Digital media and digital marketing with more than 3 years experience working in various capacities with highly reputable companies and organizations. He is writer, storyteller, content creator, photographer and journalist by professional. He simply amazing.

This post has 3 Comments

3

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Send this to a friend