Mambo matano muhimu kufanya kabla hujamaliza chuo

Elimu ya Tanzania ina lengo la kuleta maendeleo katika jamii yetu. Ili jamii iendelee kuna umuhimu mkubwa wa kutumia elimu katika nyanja mbali mbali ili kuongeza ubunifu na ufanisi wa kukabiri mambo mbali mbali ambayo yataleta tija katika jamii.

Wanachuo wanafanya makosa makubwa wanapokuwa chuoni kwani hawajiandalii maisha ambayo watakutana nayo huku mtaani baada ya kumaliza chuo. Leo ninakuletea mambo matano muhimu ambayo mwanachuo anatakiwa kufanya kabla hajamaliza chuo

1. Kutengeneza mtaji watu hususani wa taaluma yako

Moja ya vitu muhimu amabavyo mwanachuo anapaswa kuzingatia wakati bado yupo chuoni ni kutengeneza mtaji watu. Kivipi?

Wanachuo wengi baada ya kumaliza ndio huanza kutafuta watu ili wafundishwe au waunganishiwe sehemu yenye fursa. Ikumbukwe muda huo hao watu wanakuwa hawajui uwezo wa huyu mwanachuo.

Mtaji wa watu unatengenezwa ukiwa chuoni kwa kufanya kazi kwa kujitolea au internship kwa taasisi zinazotoa fursa hiyo. Huko ndio utakutana na watu na uwezo wako utaonekana. Kazi na bidii yako itajitangaza na kukutanisha na watu wengi ambao badae wanaweza kuwa msaada mkubwa kwako.

Kila sehemu unayopita kikazi hakikisha uwezo wako unaonekana. Pia hakikisha unabadilishana namba ya mawasilino na watu muhimu kila ukipata nafasi ya kufanya hivyo. Hujui ni lini au muda gani ambapo wewe utawahitaji watu hao kwa msaada au kujifunza. Na hata wao wakipata fursa au nafasi ya kukuhitaji, iwe rahisi kukupata. Huo ndio mtaji wa watu.

2. Kujijengea ujuzi na maarifa mbalimbali kuhusiana na taaluma yako

Kujijengea ujuzi na maarifa mbali mbali kuhusiana na kazi yako. Mwanachuo anapokuwa chuoni inapaswa atengeneze ujuzi mkubwa na maarifa mbali mbali kutokana na kazi husika ambayo anasomea. Ujuzi na maarifa utamjenga kwenye kazi yake afanye kwa ufanisi wa hali ya juu.

Kwenye kila taaluma kuna ule ujuzi na maarifa ya ziada ambayo yanampa thamani mtu.

3. Kujua jinsi ya kuandika CV, email za kazi na platform nyingine za ajira na fursa

Kujua jinsi ya kuandika CV, email za kazi na maarifa juu ya usahili wa kazi.

Ili kuomba kazi mtu yeyote lazima aandike CV yake katika kampuni au shirika fulani. Pia email ni njia ambayo hutumika kuombea kazi katika kampuni au shirika hivyo mwanachuo inabidi awe mjuzi nzuri wa kuandika CV ambayo inavutia pia awe mahiri katika kuandika email tofauti tofauti kama vile awe mjuzi katika kuandika email za kikazi.

Mwanachuo awe mahiri katika mambo hayo kabla hajamliza chuo ili kuwa mtaalamu zaidi katika kazi yake aliyosomea


4. Kushiriki katika warsha, makongamano na semina mbalimbali za kuongeza maarifa

Kushiriki katika matamasha, makongamano pamoja na semina mbali mbali.

Mwanachuo inabidi hauzulie katika matamasha, makongamano pamoja na semina mbali mbali hii itamfanya mwanachuo kuongea maarifa pamoja na ujuzi katika kazi mbali mbali ambayo anasomea.

Semina pamoja na makongamano ujumuisha mawazo mbali mbali ya watu wa rika tofauti hivyo muunganiko wa mawazo ya watu tofauti huweza kuleta mawazo chanya katika ubungo wa binadamu, hivyo kabla mwanachuo hajamaliza chuo inabidi hauzulie makongamano,matamasha pamoja na semina mbali mbali ili kuelimika zaidi.


5. Jitolee sehemu ili kujifunza zaidi

Kujitolea sehemu ili kujifunza zaidi. Ili kuongeza ujuzi lazima ujifunze kupitia sehemu mbali mbali hivyo mwanachuo inabidi aongeze ujuzi wake kupitia kujitolea.

Mwanachuo anaweza kujitolea sehemu inayohusiana na kazi yake ambayo anasomea chuoni kupitia njia hiyo itamuwezesha kuongeza maarifa pamoja na ujuzi wa kazi yake.

Pia kujitolea huwezesha kuongezeka kwa kujiamini pamoja na kuwa mahiri wa kazi husika, hivyo mwanachuo kabla hajamaliza chuo inabidi ajitolee ili aweze kuwa mahiri na mjuzi wa kazi husika.


Makala zingine na Leonce:

Previous ArticleNext Article
Leonce Godfrey has been in the field of Digital media and digital marketing with more than 3 years experience working in various capacities with highly reputable companies and organizations. He is writer, storyteller, content creator, photographer and journalist by professional. He simply amazing.

This post has 3 Comments

3

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Send this to a friend