Mabalozi wa jamii

Baada ya kusoma makala ya Kim Ghattas kuhusiana na wake za marais wa Afrika, nimejikuta nikikubaliana na yeye kwa kiasi kikubwa. Kwanza mara nyingi tukijadili masuala ya uongozi na jamii, wengi wetu humtupia macho rais wa nchi na wasaidizi wake pekee. Tabia hii ni ya kawaida na iliyozoeleka, kwani bado tunaishi katika jamii ambazo zimetawaliwa na mifumo dume.

Lakini pamoja na mifumo dume hii inayoendelea kunyanyasa wanawake, hasa walio masikini, wachache wao wenye nguvu, wanaonesha kupata shida ya kujifahamu wenyewe; umuhimu wao na nafasi yao katika jamii. Hapa ninazungumzia wake za marais wa Afrika. Hivyo nikafikiria kama kuna umuhimu tukiwa tunazungumzia kufundisha viongozi, tukafikiria kufundisha wake za marais pia.

Mama Obama

Mimi ninaamini kuna haja hiyo, kwani wake za marais wana nafasi muhimu sana katika jamii. Wao ni mama na sisi wananchi ni watoto wao — wao wanaweza kuchukuliwa kama mabalozi wa jamii. Hivyo basi, wake za marais wana jukumu la kuwa nuru (role models) ambayo itatazamwa na kufuatwa na wanawake wenzao. Ujasiri na ujumuikaji wao na wanajamii katika shughuli za kijamii, unaweza kujenga imani na pia kuchochea wanawake wengi kusonga mbele kimaendeleo katika jamii. Kwani leo hii si ajabu kuona wanawake wengi weusi wa Marekani wakimwangalia Michelle Obama, na kutaka kuwa wenye maendeleo kama yeye.

Mifano ya wake za marais walio mstari wa mbele kutumikia jamii zao ni mingi. Mmoja wao ni Malkia Rania wa Jordan. Ukifuatilia kazi za kijamii za Malkia Rania, utaona kabisa ana upendo wa dhati na miradi na mipango yake ya jamii. Hapa ndipo tunapokuja kwenye suala la umuhimu wa kufanya kitu unachokipenda na kukifanya kwa nguvu zako zote.

Malkia Rania ameamua kuvalia njuga suala la elimu.

Tanzania kwa upande mwingine kuna tabia ambayo nadhani sasa imekuwa ni mfumo fulani hivi — kila mke wa rais mpya kuanzisha asasi yake. Kwa mfano asasi ya Mh. Salma Kikwete, inaitwa Wama, inashughulika na masula mbalimbali ya jamii yanayowahusu zaidi wanawake na watoto. Asasi hiyo, kama asasi ya mama Mkapa EOTF zote zinalenga kumkomboa mwanamke.

Mama Kikwete na Mama Mkapa.

Hili ni jambo jema, lakini wasiwasi wangu ni huu. Je, wake wengi wa marais wa Afrika huanzisha asasi hizi kwa kuwa tu ni wake za marais? Hivyo kujisikia ni lazima wawe na kitu cha kujishughulisha nacho? Au wao hujihusisha na mipango fulani ya jamii kwa kuwa ni kitu ambacho kinawagusa moyoni kwa dhati?

Ukitaka kupima, tuangalie asasi za wake za marais wa Afrika, na zinapofikia pindi waume zao wanapomaliza muda wao, kama bado zinabaki kuwa na nguvu au zinafifia pasipo kujulikana. Hapo ndipo utajua nani alikuwa na mapenzi ya dhati na nani alikuwa anafanya mradi!

Mfano, ukimwangalia Malkia Rania wa Jordan, yeye amejikita zaidi kwenye elimu, kwani hilo ndilo jambo moja kubwa linalomgusa yeye binafsi. Hapo hapo, tukimdadisi Bi. Hillary Clinton, wakati wa kipindi cha urais wa Bill Clinton yeye alipigania kufa na kupona wananchi wa Marekani wapate huduma ya afya bila kujali uwezo wao wa kifedha.

Sasa kabla sijahitimisha na makala ya Kim Ghattas, ombi langu kwa wake za marais ni kama ifuatavyo: Umuhimu wa kuwa na msukumo na motisha katika mipango ya jamii wanayojishughulisha nayo ni kitu cha msingi sana. Suala hili linaweza kufanikiwa zaidi kama wakijua masuala yanayowagusa, na hata wakitambua vipaji vyao; kuwa mabalozi wa dhati dhidi ya vitu vinavyowakereketa, na sio kupigania vitu ambavyo vinawapendezesha machoni mwa watu pekee. Mimi binafsi ninaamini wake za marais wanaweza kutumia jukwaa walilo nalo kuleta mabadiliko makubwa katika jamii kama wakiwa na mwongozo mzuri na mapenzi ya dhati, na kama watatumia jukwaa hilo vizuri.

Makala ya Bi Ghattas inaendelea kwa kusema:

“[African first ladies] are mothers of their country, they refer to them as Mama so and so,” said Gery Ryan, a senior social scientist at Rand and one of the organizers of the program.

“They’re probably the only woman in the country who can pick up the phone and talk to anyone, the only other person apart from the president or prime minister who can get on TV and people will listen,” Mr Ryan said.

Endelea kusoma…

Previous ArticleNext Article
Bahati was born and raised in Tanzania, and then moved to California to pursue his college education. He graduated in 2008 with a Bachelor’s Degree in Political Science and a minor in Sociology. Bahati expects to be doing his Masters in African Studies in the near future. He is currently working on starting a t-shirt business and a possible publication of some of his writings. One thing that Bahati cannot live without is music, specifically Hip Hop & Bongoflava which he argues are both the voice of the youth today, and is excited to look into how Bongoflava can be a source of further entrepreneurship among the youth in Tanzania. Bahati believes that Bongoflava can help to reduce poverty in Tanzania, as can a more collective effort among key players.

This post has 1 Comment

1
  1. EOTF sijui ilikufa wapi. Enzi zile kila siku kwenye taarifa za habari, utasikia EOTF this, EOTF that. Kuna umuhimu gani wa kila anayekuja kuanzisha taasisi yake? Kwanini kutounganisha resources kwenye mpango mmoja?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Send this to a friend