Kiingereza cha ugoko darasani

“Kwa wale ambao wanajua jiko la mkaa, ni nini kazi ya kale kakopo unakoweka juu ya mkaa saa ya kuwasha?” Siku moja tukiwa form two ticha wa physics alituuliza, tukabaki tukicheka. Kicheko chetu sana-sana kilisababishwa na utani na kejeli iliyokuwa imefichwa kwenye hilo swali. Mwalimu alikuwa akigusia kuwa baadhi yetu tulikuwa washamba kiasi kwamba hata jiko la mkaa hatujui likoje. Vichekesho vilipoisha, wanafunzi tukaanza kujaribu kutoa maelezo, mengine ya kisayansi na mengine tunayajua wenyewe, kujaribu kupambanua sababu ya kukoleza mkaa kwa kutumia kale kakopo.

Baada ya maelezo ya mtu wa tisa au kumi hivi, mwalimu aliamua kusitisha kuchukua maoni akidai kuwa punde si punde tutaishia kusema kuwa ni uchawi au mazingaombwe. Baada ya hapo aliendelea kutupa maelezo ya kifizikia zaidi, kwamba kale kakopo kanasaidia kutengeneza mkondo wa hewa unaopita kutoka chini ya jiko, kunakokuwa na majivu, kuelekea juu kupitia kwenye kale kakopo. Mkondo huu unapoongezeka nguvu basi jiko linakuwa kama linajipulizia lenyewe. Tukapigwa pindi kwa mchanganyiko wa Kiswahili na Kingereza. Mpaka leo nakumbuka vizuri sana lile somo.

Walimu wangu wengine waliokuwa waking’ang’ania kufundisha kwa Kiingereza peke yake, walikuwa wanapata shida kuelezea vizuri mambo mbalimbali. Kiingereza kilikuwa kama kizuizi cha namna flani kwao japo walikuwa wakijitahidi kukisisitiza. Nikilinganisha ufundishaji wao na wa ticha wa fizikia niliyetoa mfano yake hapo juu, kulikuwa kuna tofauti kubwa sana ya ubunifu katika kutuhusisha wanafunzi wakati wa vipindi. Basi hii ikichanganywa na woga wa kujieleza tuliokuwa nao wanafunzi kutokana na mahusiano yetu na walimu, ambayo yalikuwa kama ya panya na paka, vipindi vya “Inglishi onli” vilikuwa havipandi kabisa yani. Hata HakiElimu waliwahi kulizungumzia suala la lugha ya darasani katika tangazo lao la HakiElimu Lugha.

Kwa Kiswahili?

Hata vitabu tulivyosoma vilikuwa vimeandikwa kwa ajili ya mazingira ambayo ni tofauti sana na tuliyokuwa tumezoa sisi. Labda nitoe mfano kidogo ili nieleweke. Nakumbuka nikiwa nasoma mambo ya impulse, momentum na collisions katika kitabu kimoja cha fizikia (sijui ni Abbot ile…), nilikumbana na mfano uliokuwa unazungumzia mchezo wa pool. Sasa mimi wakati huo nilikuwa sijawahi kusikia pool ni nini. Matokeo yake niliishia kupoteza muda mwingi kujaribu kufikiri pool ni kitu gani na nikaishia kuwa frustrated. Sasa hivi najiuliza, je, kungekuwa na kitabu chenye mfano unaotumia gololi, manati, mipira ya mifuko ya nylon n.k., experience yangu ya kusoma fizikia ingekuwa tofauti? Hebu na wewe jaribu kufikiri ni mifano mingapi au ni concepts ngapi umepitia ambazo mwanzoni hukuzielewa kutokana tu na kutojua mazingira ya uelezwaji wake?

Najua na ninakubali kuwa kuna sababu nyingi za kufundisha kwa Kiingereza na kuhakikisha kuwa wanafunzi tuna uwezo wa kuelewa na kujieleza kwa Kiingereza katika ulimwengu wa sasa. Hata hivyo ninathubutu kusema kuwa ubunifu, kitu ambacho ni chemichemi ya utatuzi wa matatizo mengi yanayotuzunguka, unaweza kuathiriwa na msukumo wa kufundisha kwa lugha ambayo ni tatizo la msingi katika mfumo wetu wa elimu. Lugha na mazingira ya utoaji wa elimu vinaweza kuwa chachu ya kuongeza upeo wetu wanafunzi katika kuelewa mambo, kutuhamasisha kuwa wabunifu na wafumbuzi wa matatizo yetu. Pia kupitia lugha na mazingira ya utoaji wa elimu, tunaweza kuwa katika hatari ya kushindwa kuwa wafumbuzi wa matatizo yetu.

Najua pia kuwa changamoto nyingine kubwa, hasa kwa sayansi, ni upatikanaji wa resources kama vile vitabu ambavyo vimeandikwa kwa Kiswahili na vilivyokusudiwa kwa mazingira ya walengwa. Natamani siku moja nisome mambo ya relativity ya Einstein, Higg’s Boson, String Theory au Abstract Algebra kwa Kiswahili. Tena natamani zaidi siku moja nisome nadharia za fizikia, kemia n.k. ambazo zimebuniwa na Waswahili kwa Kiswahili.Unajua nini, natoa changamoto hapahapa, mtu yeyote anayeweza kutafsiri nadharia yeyote ile ya fizikia, kemia au baiolojia kwa Kiswahili na kuielezea, tafadhali afanye hivyo kwenye comments. Hata ukichanganya lugha pia poa!

Previous ArticleNext Article
Wondering when the inside of an egg becomes a chicken, Steven broke an egg everyday for 7 days, out of his mother’s chicken project at the age of 5 before he got into a lot of trouble. It’s from such childhood curiosity that Steven’s interest in science and technology are founded. He went from breaking eggs to recently graduating with a BSc. Engineering Sciences (Electrical Engineering and Computer Science) in 2010 and is now doing research at the Harvard School of Public Health. Steven also manages Operations for Lebone Solutions Inc, and wants to build technology-focused schools in Tanzania one day and provide kids with an environment that inspires them create, innovate and invent to better their communities.

This post has 12 Comments

12
  1. Sidhani kama tatizo hasa ni lugha, nafikiri tatizo zaidi ni ukosefu wa ubunifu wakati wa kuelezea theory mbali mbali tu.

    Nakumbuka nikiwa form 2 tulikuwa na mwalimu wa baolojia Mmarekani. Kiswahili chake kilikuwa cha kubabaisha, hakieleweki kabisa. Wakati wa kufundisha alikuwa akitumia kiingereza tu lakini alikuwa akijitahidi kutoa mifano inayooneakana (visual examples).

    Kuna siku alikuwa anafundisha kuhusu Ukimwi, akafika kufundisha kuhusu kutumia condom. Enzi hizo kwa jamii iliyonizunguka ilikuwa hata neno condom kusemwa na watu wazima ni taboo seuze kuiona yenyewe kwa watoto wa miaka 13-14!

    Hakujipa tabu Mzungu wa watu, alikuja na mchi mdogo wa kutwangia, akasema haya tutatumia nyenzo hii. Licha ya kuonyesha namna ya kutumia, wanafunzi kadhaa wakapata ‘fursa’ ya kwenda kujifunza kwa vitendo matumizi sahihi ya condom (bila ya shaka wote wanaume, watoto wa kike walikuwa katika hali ya bumbuwazi kwa muda wote huo). Japo kuwa ilikuwa the most embarrassing lesson I have had to date, nafikiri hata ikifika miaka 50 baadae, kati ya wanafunzi tuliokuwa pale hakuna anaeweza kusahau ilmu ile.

    Naweza kusema huyu alikuwa hodari wa kufundisha kwa kutumia vitendo na kutokana na hiyo basi lugha haikuwa kikwazo kwake au wanafunzi.

  2. Mkuu hiki kisa kwenye aya ya kwanza kimenifurahisha!

    Ninadhani hapa upana wa lugha yetu ndio tatizo. Ingawa tutaweza kuelezea nadharia zinazotokana na uvumbuzi wa kitanzania au hali ya kwetu na kutokana na misamiati yetu wenyewe, hali ya kukokotoa misamiati mipya kuelezea nadharia ngeni au ‘abstract’ inakuwa taabu kidogo.

    Ila, kuna baadhi ya watu wanafanya masahihisho katika kurasa za wikipedia na kuziweka kwa kiswahili. Kuna wengine pia wanatafsiri maongezi ya TED (http://goo.gl/eqeI3).

    Jifurahishe na kurasa ifuatayo:
    http://goo.gl/hMli5

  3. Unaonaje tukiacha kutafsiri kutoka kiingereza kwenda kiswahili? Lengo ni kuacha society ijitengenezee lugha taratibu bila kuumba maneno yasiyo na ladha wala uhalisi wa vitu, vifaa au hisia fulani fulani…Inakuwa vigumu mno pale watu wa BAKITA wanapotengeneza maneno wakitegemea kila mtu atalifuatilia. Imechukua miaka mingi sana kwa neno kikokotozi kuanza kutumika na angalau asilimia 5 watu wazungumzao Kiswahili pale Tanzania sembuse watu watzungumzao kiswahili duniani? Cha maana tupige hatua kuendeleza sayansi na teknolojia na hapo tutaona jamii zetu zikikumbatia uwepo wa kiswahili kama lugha itumikayo kwenye karne hizi za maendeleo ya kisayansi…

  4. Naam. Utafsiri wa maneno mengine ya Kiingereza – hasa za kisayansi – ni mgumu sana. Angalia dhana ya ‘hewa mkaa’, ambayo kwa wale wasiokosa somo wanajua Kiingereza chake ni ‘carbon dioxide’. Ambayo ni sawa kama umeenda shule, lakini kwa wale waliokosa somo wanaelewa nini kwa kusikia ‘hewa mkaa’. Yaani, ni moshi wa mkaa? Au ni hewa yaliojaa na moshi? Au ndio nini? Bila shaka, kwa mtu ambaye hakuenda shule, ‘hewa mkaa’ haileti maana yoyote. Lugha ya kisayansi inabaki kwa sisi wachache tuliopata fursa ya elimu.

    By the way, nampa big-up mwandishi wa hiyo stori. Kwangu mimi, waandishi wa vyombo vya habari kwa lugha ya Kiswahili ninaowaheshimu ni pamoja na Mihangwa, Mabala, na Mjengwa. Lakini hiyo post yako imenivutia saaaana kaka kwa utumiaji wako wa lugha. Kwa maneno mengine, uandishi wako umetulia ile mbaya. Keep it up!

  5. Unanikumbusha miaka kama saba iliyopita nilikuwa na mazungumzo na Profesa wa Hisabati na Fizikia hapo Chuo Kikuu cha Columbia kuhusu kutafsiri kitabu chake “The Elegant Universe: Superstrings, hidden dimensions, and the quest for the ultimate theory” kwenda kiswahili, profesa Greene aliniambia yuko radhi na tayari kitabu chake kilishatafsiriwa katika lugha nyingi tu na kuuzwa vizuri.

    Washauri fulani wakaniambia kwetu watu wenye utashi wa kujua hayo mambo hawahitaji kutafsiriwa kiswahili, na wasiojua kiingereza hawana utashi wa kujua hayo, au angalau si wengi kiasi cha kuhalalisha kazi ya utafsiri na uchapaji wa kitabu hiki katika kiswahili. Nikaachana na hiyo habari. Lakini kuna umuhimu wa kufanya kazi kama hizi. Hata kama ni kwa ajili ya kukuza msamiati wa kiswahili tu uendane na mambo mapya yanayogunduliwa katika sayansi.

  6. Nakubaliana na VN moja kwa moja

    hatuwezi kutegemea lugha iwe na maneno ya kisayansi ikiwa jamii yenyewe haiishi wala kuzungukwa na sayansi.

    Lugha siku zote inakwenda sambamba na utamaduni wa jamii. Tukichukulia utamaduni wa ‘sayansi ya kiza’ kwa mfano, unakuta kiswahili kimesheheni misamiati ya kuweza kuzungumzia suala hili.

    kapigwa kipapai, karogwa, kaendewa kwa fundi, kafukiziwa, kwa kutaja kwa uchache tu, yote yanazungumzia kitu kimoja ikiashiria kuwa jamii ina uelewa wa kutosha wa suala hilo kwa watu wa rika lote.

    nafikiri ni vyema kuiwacha lugha ikajibadili kwa vile itakavyo wenyewe bila ya kuishurutisha, badala yake tukazanie kwa walimu kufundisha kivitendo zaidi na pia kukikuza kiswahili kinachotumika sasa.

  7. Wadau inapendeza sana kuona mawazo yenu hapo juu yakiboresha fikra na mitazamo mbalimbali juu ya hili suala.

    Binafsi nimejengwa sana na mtizamo wa kusisitiza matumizi ya vitendo katika ufundishaji. Kwa hakika hili ndio haswa litapima na kuleta changamoto kwa walimu hususani jinsi ya kutumia rasilimali walizonazo katika ubunifu wa hali ya juu mno. Hata kama rasilimali hizo ni kidogo. Mfano, jaribio maarufu la form one ambalo wengi tunalikumbuka kama pendulum bob kutoka enzi zile za O level linaweza kufanyika hata kwa kutumia jiwe lililotundikwa mtini kwa kutumia kamba ya katani. Japo kutakuwa na mapungufu ya precision na accuracy ya jaribio lenyewe, lakini errors ni jambo la kawaida kabisa kwenye jaribio lolote la kisayansi. Tena ni muhimu sana wanafunzi wafundishwe hivyo kwa wazi kabisa tangu awali. Kwa meneno mengine, walimu, hasa wa sayansi, wana changamoto ya kutumia ubunifu wao na kugeuza mazingira waliyonayo kuwa maabara ya kuwawezesha wanafunzi kuelewa concepts.

    Jambo lingine ambalo labda sikulieleza vizuri kwenye post hapo juu ni lugha ya kufundishia. Labda ningesisitiza delivery zaidi ya kusema lugha tu, maana hata vitendo ni aina ya lugha. Nilichokuwa nataka kusema hasa ni kwamba katika kueleza concepts mbalimbali darasani walimu wasilazimishe kutumia lugha (au delivery ukipenda) ambayo haimsaidii mwanafunzi kuelewa. Kwa mfano, tuseme unafundisha fizikia kwenye shule ya kata, ambayo wanafunzi wengi walioko darasani ni wale ambao hawakupata maksi za juu darasa la saba na hivyo msingi wao wa lugha ya kiingereza sio mzuri. Je, utajilazimisha kueleza concept kwa kiingereza peke yake?

    Ni kweli huwezi kutafsiri msamiati wote wa sayansi kuwa wa kiswahili maana utakumbana na tatizo kubwa zaidi la kuwamezesha watoto wa watu maneno yatakayozidi kuwachanganya. Nafikiri ili waelewe, mwalimu inabidi atumie mchanganyiko wa kiswahili na kiingereza katika kufundisha; zaidi sana matumizi ya vitendo. Wanafunzi wakielewa, regardless of lugha iliyotumika kuwaelewesha, inawapunguzia frustration ya lugha ambayo ni kizuizi cha uelewa kwao na badala yake kujenga curiosity ya kutaka kujua zaidi mazingira yao. Katika experience yangu, mtu ukishakuwa curious na kupenda kitu, hata lugha haiwezi kukuzuia tena kujifunza zaidi.

  8. Safi mno SL.
    Kwa kweli nakubaliana nawe, kujua kukitwanga kiingereza sio ishara ya elimu kupanda.Mifano tunayo ya nchi zilizoendelea ambazo hazizungumzi kiingereza au lugha ya kigeni ya watawala wao wa zamani. Inawezekana kuwa tunaona uvivu kutafsiri vitabu vya masomo kwa lugha yetu, muhimu kuliko yote nakumbuka wasomi na baba wa taifa walishawahi kulizungumzia hili swala. Sie tulichoishia ndio kuanzisha na kuendeleza academy schools, “kudolarizi bidhaa zetu” na kuendelea kuwa limbukeni wa bidhaa na mambo ya nchi za nje. Itabidi tu tuamke, tena kwa sana maana tupo nyuma kweli kweli!

  9. For real people? Mnaniambia tusubiri mpaka tuwe na large hadron super collider ndiyo tutafute Kiswahili chake ? Mpaka tuweze kuiona Higgs boson wenyewe ndiyo tuipatie jina la Kiswahili? Labda tuendelee kuangalia hizo nyungo zinapaje tu.

    Societies zote zilizoendelea hazikuendelea kwa kujifungia, zimeendelea kwa kujifungua. Mansa Aboubakar alifika Amerika kabla ya Columbus, lakini kwa sababu Mali ili frown upon a Mansa leaving his people to explore foreign lands, hata kwenye historia yao hawamsemi, watu wanamjua Mansa Musa tu. Wachina walianza kuendelea kisayansi kabla ya wazungu, in 1434 they even sailed all the way to Italy and ignited the Renaissance, they even came to East Africa and took giraffes back to their imperial courts, but how did the west come to advance more than the Chinese ? Because the west was open for business, and ready to learn from other cultures, including enriching it’s culture from cultures around the world.

    This isolationist thinking is as dangerous now as it was back in the days. The same isolationist thinking that stagnated Chinese innovation, – in their case out of a patriotic pride that believed China was the center of the world and civilization, and therefore the Chinese did not need to learn from the rest of the world, rather the rest of the world needed to learn from China- is still just as dangerous today.

    Even in Chemistry, we are familiar with the concept of a catalyst, surely by the sheer truism of the second law of thermodynamics, with increasing disorder and entropy, we will be forced to adapt to a more complex world, and either perish in ignorance or more likely adapt, but if we can speed the whole process by a catalyst of glancing at what others are doing, where is the harm in that ?

    We must not find it irreconcilable that a society can learn from another and at the same time strive to chart it’s own course. The fact that we are so backwards in scientific endeavors should not make us isolationist in a quixotic craze at reinventing the wheel, while we already have the blueprints to a nuclear technology. If we can excite our youngsters minds, who knows that the next batch of singularitarians will not come from Dar ?

  10. @Kiranga

    Sio tunasubiri mpaka tuwe na LHC ndo tutafute neno lake, lakini kutunga au kutafuta neno lake la kiswahili kwa sasa, kisha iweje? Hata tukipata hilo neno, kitachotokea ni kuliweka kwenye kamusi tu lakini litashindwa kusambaa kwa watumizi wa lugha.

    Hatukatai kuwa ni lazima tukubali jamii yetu ifunguke kwa influences za nje ili tupate kuendelea, lakini kupiga hatua zinazoacha pengo kubwa baina ya lugha na jamii pia haileti mantiki. Lugha iliyojaa misamiati ambayo haitumiwi na jamii, ni sawa na kusema ni lugha mfu. Ipo lakini haimsaidii mtumiaji wa lugha wala haiakisi hali halisi ya jamii.

    Tunapo fundisha sayansi iliyojaa kina Newton na Faraday ni moja ya viashiria kuwa tumefungua jamii yetu kwa ajili ya elimu na athari nyengine za nje na sio kuwa tumejifunga.

    Suala linakuja, ilmu hii ya kigeni tunaifikisha vipi kwa walengwa? Tutumie misamiati migeni tuliyoitengeneza mahsusi kwa ajili ya kufikisha elimu hii au tutumie lugha ya kigeni inayotokana na chanzo cha elimu hiyo ya kigeni? Au tuchanganye lugha wakati wa kutoa ufafanuzi zaidi pamoja na kutumia mifano itokanayo na mazingira yaliyotuzunguka?

    Ikiwa tutasema hawa wanafunzi kujifunza misamiati mipya ya sayansi kwa kiswahili ni sawa na kujifunza kwa kiingereza kwa sababu zote ni ‘lugha’ ngeni kwao, basi tutakuwa sahihi kusema misamiati mipya itungwe na ianze kutumika kwa wanafunzi wa shule za sekondari ya chini, kidogo kidogo ianze kuzoeleka kwenye jamii.

    Hapa tena tunakutana na tatizo jengine. Tunaweza kutunga/kutafsiri misamiati yote ya sayansi kwa mkupuo kuanzia M-theory hadi Fuzzy Clustering bila ya kupoteza maana na uhalisia wa sayansi yenyewe au itatubidi tuanze na sayansi ya chini kwanza ya akina Archimedes inayohusiana na objects in fluids peke yake?Na pale mwanafunzi akipata interest ya kujisomea mwenyewe wakati vitabu vyote mbali na vile vya shuleni vimeandikwa kwa kiingereza itakuwaje?

    Nafikiri urahisi zaidi uko katika kuongeza muamko unaohusiana na sayansi na teknolojia kwanza kabla ya kutunga misamiti na sio kinyume chake.

  11. kwa kusema kweli lazima tudhihirishe mitazamo inayotumika katika lugha ya kiswahili kwa vile lugha ya kiswahili imeanza kukuwa au kupanuka.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Send this to a friend