Taksi na Mashindano ya Olimpiki

Ujasiriamali huhitaji ubunifu, hasa katika dunia ya leo, ili kuweza kufanikiwa. Katika dunia ya leo yenye changamoto nyingi, ubunifu husaidia kutatua matatizo ya jamii kwa kufanya mabadiliko kidogo na kwa gharama nafuu. Dereva mmoja wa London anatuonesha jinsi gani yeye ameweza kutatua tatizo lake kwa kuongeza ubunifu kidogo kwenye biashara yake ya taksi.

Katika kipindi hiki cha michezo ya Olimpiki, jiji la London limefurika watu, hivyo barabara zimekumbwa na tatizo kubwa la foleni. Tatizo hili limeathiri biashara ya taksi, na madereva wengi wameanza kula hasara (watu wengi hupanda mabasi, treni au hata kutembea). David Weekes, kama  madereva wengine, ameathirika na tatizo hilo — lakini ametumia tatizo hilo kuanzisha biashara nyingine.

Kwa kuwa jiji la London limefurika watu sasa hivi, hoteli zenye nafasi zipo chache na ambazo zenye nafasi ni bei mbaya.

Ndugu Weekes akaona fursa; akaamua kufanya taksi yake kuwa kitanda, na kukipangisha kwa wageni.

Huu ni mfano mzuri jinsi ubunifu ulivyokuwa muhimu sana katika ujasiliamali. Tujifunze kutumia changamoto kama motisha, kuweza kusonga mbele. Je, una mfano kama huu kwa hapa Tanzania na Afrika kwa ujumla?

Previous ArticleNext Article
Bahati was born and raised in Tanzania, and then moved to California to pursue his college education. He graduated in 2008 with a Bachelor’s Degree in Political Science and a minor in Sociology. Bahati expects to be doing his Masters in African Studies in the near future. He is currently working on starting a t-shirt business and a possible publication of some of his writings. One thing that Bahati cannot live without is music, specifically Hip Hop & Bongoflava which he argues are both the voice of the youth today, and is excited to look into how Bongoflava can be a source of further entrepreneurship among the youth in Tanzania. Bahati believes that Bongoflava can help to reduce poverty in Tanzania, as can a more collective effort among key players.

This post has 1 Comment

1
  1. Ha! Entrepreneurship at its best. Might be some safety issues about having someone in bed while the car is moving, but hey, assuming no accidents, why not? Probably the most comfortable ride anyone could pay for in the whole city. Need to think of a way to do this in my Bajaj…

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Send this to a friend