Buriani Mpiganaji na Shujaa Regia Mtema

“Nilimfahamu marehemu Regia kama kijana mwanaharakati na mpambanaji asiyechoka kupigania kile anachokiamini. Kipindi hiki harakati nyingi alizokuwa akizifanya, alizifanya kupitia harakati za kudai haki za msingi za vijana wa Tanzania, hususan haki za makundi maalumu wakiwamo watu wenye ulemavu, watoto, wanawake na vijana kwa ujumla.”