Mic MOJA tu?

Jana nilipata fursa ya kujikumbushia nyimbo za Hasheem. Sizungumzii Hasheem huyu — namuongelea Dogo! Wakati nasikiliza freestyle inayoenda kwa jina la ‘Naharibu’ rafiki yangu akanipa wazo la kichokozi… eti tumtafute Dogo, tumuombe arudi ulingoni, tumlipie gharama za studio ili atoea angalau album moja tu.

Tuyaache hayo.

Hivi umeshawahi kujiuliza hili swali: Ingekuwa vipi kama Bongo tungepewa mic moja tu? Yaani, baada ya kuangalia vipaji kadhaa/wasanii mbalimbali, unadhani yupi anastahili kupewa hicho kipaza sauti kimoja tu ili sauti yake iwafakie Vijana wote Tanzania?

Binafsi, napenda wasanii kibao na nawasikiliza wote, lakini kuna mmoja ambaye nadhani atastahili kupewa hiyo mic: N***a Jay, Jay wa Mitulinga, Mti Mkavu, Jay Tunakuzimia, Jay Nyangema, Heavy Weight MC, Prof. Jay…

Tangu Jay atoke na album ile nzito iliyoshiba mawe na vina tokea mwanzo hadi mwisho (Machozi, Jasho na Damu) sidhani kama ametuangusha. Na utakubaliana na mimi kuwa amekuwa kama sauti ya walalahoi.

Wakati muda wa kupiga kura ukikaribia na watu wakiumiza vichwa kura zao ziende kwa nani nadhani labda mambo yangekuwa rahisi mno kama Jay angekuwa mmoja wa wagombea!

Najua wengi mna mawazo tofauti ambayo ningependa kuyasikia. Nani apewe mic?

Previous ArticleNext Article
Steven was born and raised in Dar es Salaam, and moved to Germany for his studies. He graduated with a BSc. in Physics (Jacobs University Bremen), and then a MSc. in Engineering Physics (Technische Universität München). Steven is currently pursuing a PhD in Physics (growth of coatings/multilayers for next generation lithography reflective optics) in the Netherlands. He’s thinking about starting his own business in a few years; something high-tech related. At Vijana FM, Steven discusses issues critical to youths in Tanzania, music, sport and a host of other angles. He’s also helping Vijana FM with a Swahili translation project.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Send this to a friend