Solo Thang arudi na Ung’eng’e!

Juhudi za wasanii wetu kujaribu kuvuka mipaka zinatia moyo na nadhani zimeanza kuzaa matunda. Njia mojawapo ni kutumia lugha ambayo watu wengi nje ya Tanzania wanaielewa. Hii ina faida na hasara zake — inategemea unaangalia hili suala kwa jicho lipi!

Msanii mwingine ambaye anajulikana na wengi kuwa ana msimamo mkali, Ulamaa amerudi na wimbo mpya unaoitwa ‘All I need’:

Kama ulivyoona, kuanzia mwanzo hadi mwisho ni ung’eng’e tu au lugha ya Malkia, kama mchangiaji mmoja anavyoiita. Binafsi, nadhani jiwe limetulia. Lakini kama mmoja wa washabiki wa Solo Thang, kuna sehemu ya moyo wangu ambayo imetibuliwa.

Solo ana uwezo mkubwa SANA wa kufinyanga na kucheza na maneno ya lugha yetu ya Kiswahili. Kunuka Kunukia, Si Ulinikataa, Sukari na Pilipili, Hili Balaa, Homa ya Dunia…Vina Utata! Natumaini atarudi na nyimbo kama nilizozitaja huku akipiga danadana maneno ya Kiswahili kama Messi.

Hebu jikumbushie njia aliyopitia Msafiri (bofya)! Sikiliza ‘Sikati Tamaa’, ‘Travellaah’ na ‘Usinichokoze’…

Previous ArticleNext Article
Steven was born and raised in Dar es Salaam, and moved to Germany for his studies. He graduated with a BSc. in Physics (Jacobs University Bremen), and then a MSc. in Engineering Physics (Technische Universität München). Steven is currently pursuing a PhD in Physics (growth of coatings/multilayers for next generation lithography reflective optics) in the Netherlands. He’s thinking about starting his own business in a few years; something high-tech related. At Vijana FM, Steven discusses issues critical to youths in Tanzania, music, sport and a host of other angles. He’s also helping Vijana FM with a Swahili translation project.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Send this to a friend