Siasa na Vikaragosi…

Leo hii nimekumbana na habari hii inayohusu kipindi hiki kinachoitwa Za Newz cha Afrika ya Kusini. Kipindi hiki kinafanana na Ze comedy cha Tanzania, sema wao wanatumia vikaragosi na wamezamia zaidi kwenye ulingo wa siasa.

Kipindi kama hiki cha Za newz kina nafasi kubwa sana kwenye jamii zetu, hasa katika kuelimisha wanajamii maswala ya kisiasa. Tanzania tukiwa bado na mwamko mdogo katika siasa, vipindi kama hivi vinaweza kuongeza changamoto na mwamko wa kisiasa, hasa miongoni mwa sisi vijana. CCM wamenza kufanya hivyo kwa kutumia wasanii wa bongoflava, mfano ni katika kampeni yao ya mimi nimechangia, naomba na wewe uchangie pia.

Vyombo vya habari bado vinakazi kubwa kuhakikisha wananchi wanajihusisha na maswala ya kisiasa. Kupiga kura ni namna moja tu ya kujihusisha na siasa, lakini je tunazifahamu itikadi za wagombea vizuri. Lazima tujue katiba ya vyama tunavyotaka kuvipigia kura. Sasa kipindi kama Za Newz kinajitahidi kusogeza jamii karibu na maswala ya kisiasa kwa kutumia njia ya kukejeli na kuchekesha. Mimi ninadhani hiyo ni njia nzuri ya kuvuta jamii hasa vijana, na kuwapa habari juu ya maswala mbalimbali ya kisiasa.

Uchaguzi mkuu wa raisi na wabunge ndio huo unakuja, lakini je, sisi kama wapiga kura tumejiandaa vyakutosha, au tunaenda tu kupigia kura wale wagombea wenye sura zenye mvuto na matabasamu mazuri?

Previous ArticleNext Article
Bahati was born and raised in Tanzania, and then moved to California to pursue his college education. He graduated in 2008 with a Bachelor’s Degree in Political Science and a minor in Sociology. Bahati expects to be doing his Masters in African Studies in the near future. He is currently working on starting a t-shirt business and a possible publication of some of his writings. One thing that Bahati cannot live without is music, specifically Hip Hop & Bongoflava which he argues are both the voice of the youth today, and is excited to look into how Bongoflava can be a source of further entrepreneurship among the youth in Tanzania. Bahati believes that Bongoflava can help to reduce poverty in Tanzania, as can a more collective effort among key players.

This post has 4 Comments

4
  1. Swali ni hili: Viongozi wetu watakubali vitu kama hivi vifanywe mbele ya macho yao? Anayewapatia ni Kipanya; ingawa katuni zake huwekwa kapuni mara nyingine.

    Pia, Gado ameanza kufanyia kazi haya mambo ya vikaragosi.

    Ukiacha hayo, kuna 'tetesi' kuwa Nakaaya anajipanga kugombea ubunge kupitia CHADEMA.

  2. mmhh Nakaaya anagombania ubunge..kuumbe, now its all making sense..haha..tetesi zinasema anagombea jimbo gani?…

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Send this to a friend