Mbu na harufu ya pombe

Habari si njema kwa ‘wanywaji’ bongo. Utafiti umeonyesha kuwa, mbu wanaosababisha malaria wanavutiwa mno na harufu ya aliyekunywa bia. Mbu kama wadudu wengine wengi wana uwezo mkubwa wa kuhisia harufu mbalimbali – insect repellant nyingi zinatumia sifa hii ili kufukuza mbu. Katika utafiti huu uliofanyika huko Burkina Faso, watu 43 pamoja na mbu takribani 2500 walitumika ili kuweza kudadisi athari zozote kwa mbu zitokanazo na unjwaji wa bia.

Watafiti hawa wanaeleza kuwa metabolism ya bia mwilini inabadilisha kemikali fulani za harufu zitokazo ngozini na hivyo harufu itokayo baada ya kunywa bia yaweza kuwa inawavutia mbu hawa. Pia wanadokeza kuwa, baada ya bia kunywewa kinga mwilini hupungua, kwahiyo mbu kwa namna fulani wameweza kujenga uwezo wa kuhisia upungufu huu na hivyo kupendelea zaidi harufu ya waliokunywa pombe. Utafiti zaidi wahitajika ili kufahamu ni signatures gani za harufu zinazobadilika ambazo zinavutia mbu hawa. Itabidi tuanze kupiga ‘tungi’ ndani ya neti.

Previous ArticleNext Article
Joji was born and grew up in Dar es Salaam, Tanzania. He graduated with a B.Sc in Biochemistry in Germany, and is now pursuing a Masters degree in Microbiology & Immunology at the Swiss Federal Institute of Technology (ETH) in Zurich, Switzerland . Joji is particularly interested in matters related to global health, and basic science research that tackles public health challenges. He is engaged in mentoring Tanzanian students in higher education issues, most notably at the Kibaha High School. In this capacity, Joji blogs with Vijana FM about scientific research and development, and how youth can gain greater access to higher learning.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Send this to a friend