Utaenda ‘jeshini’?

Wengi wetu tumesikia simulizi za kusisimua kutoka kwa wazazi wetu pindi walipokuwa jeshini (National Service). Nyingi zinahusu shida, uvumilivu, ufanisi na uzalendo. Ingawa kuna waliochukia maisha magumu waliyoyapata walipokuwa jeshini, wengi wao wanakumbuka kipindi hicho kwa tabasamu. Binafsi mama yangu anasikitika kuwa vijana wa leo hatupitii kimbembe kama alichopitia yeye baada ya form six kwa mwaka mmoja pale JKT Ruvu.

Mpango wa National Service ulianzishwa na Mwl. Nyerere katikati ya miaka ya 60 kwa nia ya kujenga taifa lenye watu wazalendo, jasiri, werevu na wakakamavu. Mchakato huu ulikuwa wa lazima kwa wanafunzi wote wanaomaliza shule ya sekondari kwenda katika kambi za jeshi na kupitia mafunzo mbalimbali ya kijeshi na kielimu kwa mwaka mmoja. Mpango huu ulifutwa mwaka 1992, na hivyo kufanywa wa hiari.

Nchini Tanzania, kuna mjadala umejitokeza kuhusu kurudishwa kwa mpango wa National Service kwa vijana wa sasa. Je, itakuwa vibaya tukirudisha mchakato huu kwa wanaomaliza sekondari kutumikia taifa kabla ya kujiunga na chuo au sekta binafsi? Simaanishi tuwe na national service ya kijeshi, la hasha, bali tuanzishe mpango kwa ajili ya wahitimu wa sekondari utakaoweza kuwapeleka vijana wetu vijijini kufundisha masomo kama hisabati, na lugha kwa kipindi cha miezi 6-12. Au hata kuwatumia vijana hawa katika hospitali zetu – kwenye awareness campaigns za ukimwi/malaria vijijini, au kuwatumia kwenye vituo vya kilimo, vituo vya wazee/walemavu/watoto yatima na hata kwenye mabenki. Ilimradi tu mchakato huu usiwe wa kitumwa, au mateso bali uliojaa elimu mbadala wa vitendo ili kujenga taifa imara.

Previous ArticleNext Article
Joji was born and grew up in Dar es Salaam, Tanzania. He graduated with a B.Sc in Biochemistry in Germany, and is now pursuing a Masters degree in Microbiology & Immunology at the Swiss Federal Institute of Technology (ETH) in Zurich, Switzerland . Joji is particularly interested in matters related to global health, and basic science research that tackles public health challenges. He is engaged in mentoring Tanzanian students in higher education issues, most notably at the Kibaha High School. In this capacity, Joji blogs with Vijana FM about scientific research and development, and how youth can gain greater access to higher learning.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Send this to a friend