January

Sidhani watu wengi sana walikuwa wanamfahamu ‘Mgosi‘ January mwaka jana. Wengine walikuwa hata walikuwa hawajui kuwa Bumbuli kuna mashamba ya chai!  Ok, mi’ binafsi sijawahi kupanda ile milima ya Usambara kuona mashamba ya chai, lakini nimepita tu karibu kwenye safari zangu za Tanga na Upareni.

Safari ya kwenda Usambaani – kule milimani – ni kitendawili wakati wa mvua. Sina uhakika kama mambo yamebadilika sana; lakini wakati ule ilikuwa inakubidi ushuke Korogwe halafu uchukue mabasi madogo au hata pick-ups zinazoenda milimani. Shughuli ni pevu pale ambapo gari linaanza kuteleza kwenye tope. Mara nyingi kina baba hushuka na kuanza kusukuma gari. Lakini kuna siku (mvua ikizidi) inabidi safari iahirishwe au wanaoweza kutembea wanaendelea…

Ngoja niache soga…

Mi’ sio mwanachama wa chama chochote kile, lakini najitahidi kuwa makini kusikiliza na kuangalia mambo yanayotokea kwenye ulingo wa siasa. Kama mtu mwingine yule wa kawaida, kusema kweli nimechoshwa kuona tu picha za watu wakisema wamejiunga na chama fulani au wamejitosa kwenye kinyang’anyiro cha kugombea ubunge kwenye jimbo fulani.

Kwa maneno mengine, napenda kuona watu wanaotangaza nia zao wakitoa na sera zao — kikamilifu. Kutuonesha nini watakachokileta kwenye jimbo fulani. Hii bila shaka itatupa vielelezo vitakavyopimika, ili tuweze kuuliza maswali ya msingi. Akiteleza huko mbeleni, tutajua wapi alishindwa na yeye mwenyewe mhusika atajua wapi patahitaji mabadiliko. Zitto Kabwe ni mmoja wa wanasiasa wachache sana ambao wamejitahidi kwa hilo.

Ila kuna mtu mwingine kaingia mjini, au tuseme Bumbuli: January!

Nimemfuatilia toka atangaze nia yake. Kama watu wengine wengi nadhani labda wingu lililoletwa na jina lake la pili lilinifumba macho (kimoyomoyo nikawa nasema “yale yale!”). Lakini baada ya kusoma hotuba yake wakati anatangaza nia, na kuona kijana anajua hadi bei ya chai (Wastani wa bei ya majani mabichi ya chai kule Bumbuli ni shilingi 130 kwa kilo!), kusema ukweli, mawazo yakabadilika. Kilichonifurahisha ni kwamba ana mawazo tayari ya jinsi ya kutatua matatizo ya wakazi wa Bumbuli.

Wagombea wengine, je? Kutundika CV yako kwenye blog tu haitoshi. Vijana tumeanza kujifunza kuuliza maswali ya maana siku hizi.

Kwa kifupi, dogo yuko makini na nadhani atafika mbali (kama angekuwa anagombea Urais mwaka huu nadhani nisingeona aibu au kusita kuweka kura yangu hadharani). Ingawa Bumbuli ni sehemu ndogo tu, kipawa cha mtu hakifichwi na vichaka. Kaonesha kuwa anaweza kuwapanga watu, ana mawazo yanayoweza kuleta mabadiliko, kutatua matatizo n.k. Tunasubiri tuone matokeo baada ya miaka mitano; itakuwa rahisi kupima kwasababu nitakuwa nimeshakisoma kitabu chake “Jana, Leo na Kesho.”

Kwa kumalizia tu, inatia moyo, na naomba wale viongozi wa ngazi za juu waangalie na kujifunza machache kutoka kwa January. Kama January unaisoma hii makala, mshauri Rais afanye mdahalo basi na wagombea wengine wa kiti cha Urais.

Oh, nilikuwa nimesahau. Jina lake kamili ni January Makamba.

Kwaheri!

Previous ArticleNext Article
Steven was born and raised in Dar es Salaam, and moved to Germany for his studies. He graduated with a BSc. in Physics (Jacobs University Bremen), and then a MSc. in Engineering Physics (Technische Universität München). Steven is currently pursuing a PhD in Physics (growth of coatings/multilayers for next generation lithography reflective optics) in the Netherlands. He’s thinking about starting his own business in a few years; something high-tech related. At Vijana FM, Steven discusses issues critical to youths in Tanzania, music, sport and a host of other angles. He’s also helping Vijana FM with a Swahili translation project.

This post has 7 Comments

7
  1. Bunge linalofuata patakuwa hapatoshi. From January Makamba to Halima Mdee to mama Tibaijuka, I can’t wait.

  2. Kweli, bila shaka kutakuwa na midahalo ya maana. Najua wengi hupenda kuingiza “siasa za kujilinda”, lakini idadi ya watu wanaokuja na vielelezo thabiti inaongezeka taratibu. Binafsi, kama nilivyosema hapo juu, inatia moyo; ingawa kama tunavyojua safari ni ndefu.

    Kwahiyo wanaoweza kusaidia na wenye mawazo mbadala wajitokeze. Tuache siasa za vyama na tuzame kwenye siasa za maendeleo, kwasababu hicho ndicho tunachokitaji sasa hivi.

    Nina uhakika watu wawili watatu – wenye hulka ya uongozi – wakiona vitu kama hivi bila shaka wataitikia mwito.

  3. Huyu kijana anatuweka kwenye wakati mgumu watu ambao tumeshachoka CCM. Ni mategemo yangu kuwa hiki ndio mwanzo wa kizazi kipya cha CCM na huu ndio mwanzo wa mwisho wa kizazi kile cha CCM.

    Bunge lijalo nadhani tutamuangalia kwa karibu, na kuona uwezo wake na maendeleo atakayoleta.

    Lakini basi, mimi binafsi ninaomba tu asijisahau akabebwa na upepo wa marafiki wa huyo mwenye jina mwisho wa jina lake. Manake, siasa nayo inawenyewe, huwezi kuingia tu ukataka upigane vikumbo na mamwinyi uliowakuta. Lakini kama akiwa makini, nadhani atafanikiwa kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kufika mbali zaidi ya ubunge, na hata kuanza kuchochea mabadiliko ya kweli ndani ya chama.

    In short, naomba tu asije ishia kuwa kibaraka wa makabaila wa siasa ya Bongo…

  4. Tutafakari: Hivi ukiangalia kambi ya upinzani, unadhani wanaweza kuwa na “organization” ambayo itaweza kuongoza nchi? Tokea mfumo wa vyama vingi upitishwe 1992, hawajafanya la maana ambalo limeamsha wananchi wa Tanzania. Migogoro tu na imebakia watu kuhama kutoka chama kimoja kwenda kingine.

    Tukae na kusubiri; labda wapinzani wataamka? Kujiunga na kuleta upinzani wa kweli dhidi ya CCM? Au demokrasia ya kweli Tanzania itakuja tu pale CCM itakapogawanyika?

    Binafsi, najaribu kuangalia mambo kwa jicho la tatu na naona mambo yakibadilika, ilihali kwa mwendo wa kinyonga. Lakini watu wenye hulka ya uongozi wanajitokeza polepole.. Slaa, Mdee, Zitto, Makamba, Tibaijuka. Watu kama hawa wakiweka siasa za vyama pembeni na kujali maslahi ya Taifa, nadhani safari ya kwenda tunapotaka itaanza.

  5. I’m tired of seeing his face. Cant wait for the campaign to be over so atulie alale Bungeni while getting his monthly allowances…

    Politics in Tanzania are corrupted coz no matter what they try to portray in the media it’s all fake. WE ARE NOT A DEMOCRATIC country. Its a one party country same political party rules every other election.

    We already know who is going to win. So why vote if it doesn’t matter? Its like a monarchy.. The government is run by family members.. Passing down authority to their children. Where does this leave our children? People in power take advantage of that. I’m tired of reading and hearing the same names. Makamba…Kikwete and the like.

    People who need representation aren’t represented? Where did this Makamba kid come from?? If we want to see change we need to change the leaders. It’s sad to know that some people still believe Nyerere is the president. There needs to be another party that will offer opportunities. Many people run through CCM coz they are guaranteed positions. How would ShyRose us? People need to be free to speak up since as we all know when you do, you end up disappearing or dying… We need a movement.

  6. I can’t faulty him, the people of Bumbuli have spoken, who are we to oppose it, whether he had enough money to burn from his backers or through his shear persuasive power it doesn’t matter, they boy has won.

    That was the easy part, the hard part now is to represent the Bumbuli people, they need, water, electricity, health, welfare, education and basic infrastructure, will January deliver?

    Let’s hope so, I don’t give a toss whether his family were influential in the elections, we needed new blood, you can’t teach old dogs new tricks, it’s our time, if my fellow walalahoi would like to have a go, no sweat, but let’s give him our support, lets chip in our points and remind him not to get that common “Tz Mp’s disease”!

    Oh yes, once they get into that bunge, they tend to forget all the promises and the people who elected them!
    Let’s hope not!

  7. Since ni mCCM sitegemei makubwa mazuri kwake maana kuwa ndani ya CCM ni lazima ukubaliane na uchafu wao, kwa mazingira hayo January hataleta mabadiliko gani ndani ya chama chafu. Nape alikuwa nuru mpya ndani ya CCM lakini wapi wenye chama walimkemea kwa nguvu kubwa hadi kukosa nafasi aliyostahili ya ubunge kiasi cha kumleta mama asiye na hoja Hawa Ng’umbi.

    Nje ya CCM watu ni waadilifu lakini wakijiunga na chama hiki huchafuka mara moja, kwani mifumo yake inaruhusu ufisadi. CCM mara nyingi inatumia rasilimali za umma kwa maslahi ya chama chao. Lakini haijawahi kutokea mwana-CCM katetea raslimali yetu zaidi chama chao kwanza.

    Katika hali halisi January ataongeza idadi ya wabunge waunga hoja kwa asilimilia 100. Msiwe na imani sana na huyu kijana. Binafsi nilifurahi sana alipotoa kitabu kuhusu hali ya jimbo lake lakini nikimfikiria baba yake, napata wasiwasi. Makamba ni kiongozi dhaifu sana. Je, mtoto anaweza kuwa tofauti na baba yake kwa kiasi kikubwa?

    Tunamsubiri Bungeni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Send this to a friend