Maswali matano na Neema A. Magimba

Neema A. Magimba ni wakili wa mahakama Kuu ya Tanzania na pia ni mwazilishi shiriki wa Sheria Kiganjani.

1. Kwa kifupi Sheria Kiganjani ni nini, na ipo kwa ajili ya watu gani?

Sheria Kiganjani ni mfumo unaomuwezesha mtumiaji kupata huduma za kisheria kupitia simu ya mkononi. Mfumo huu upo kwa lugha ya Kiswahili na unapatikana kupitia simu janja, simu za kawaida, na tovuti.

Sheria Kiganjani ni mfumo unaomuwezesha mtumiaji kupata huduma za kisheria kupitia simu ya mkononi.

Sheria Kiganjani inawalenga Watanzania wote wenye uhitaji wa huduma za kisheria haswa wale wa kipato cha chini na kati.

2. Mpaka sasa mmefikia watu wangapi na gharama za huduma zenu zipo vipi?

Mpaka sasa Sheria Kiganjani imefikia watu zaidi ya 25,000 Tanzania nzima. Gharama za huduma zetu ni kama ifuatavyo:

Kuongea au kuchati na wakili:

  • Mwezi: Tsh 5,000
  • Wiki: Tsh 2500
  • Siku: Tsh 1,000

Huduma za nyaraka hutegemea na aina ya nyaraka, na gharama ni kuanzia Tsh 5,000 mpaka Tsh 50,000.

3. Kwa watu wasio na smartphones na uwezo wa kupata Internet mnawafikia vipi?

Watu wasio na simu janja wanaweza kuwasiliana nasi kupitia number zetu za simu baada ya kufanya malipo, lakini watu hawa hunufaika na taarifa zote za muhimi kuhusiana na masuala ya sheria na ueleea wa sheria kupitia mfumo wetu wa Bulk SMS kila wiki.

Watu wasio na simu janja wanaweza kuwasiliana nasi kupitia number zetu za simu.

4. Unaiona wapi Sheria Kiganjani baada ya miaka mitano mbele?

Malengo yetu ni kuweza kufikia na kutoa huduma kwa watu 500,000 wa kipato cha kati na chini ndani ya miaka mitano.

5. Una nini la kuwaambia vijana juu ya fursa zilizopo kwenye upande wa digitali katika sekta ya Sheria kwa ujumla?

Sekta ya sheria kwa upande ya digitali bado ina fursa nyingi sana haswa kwa vijana wabunifu Tanzania. Njia za utoaji huduma za kisheria kwa unafuu na urahisi zipo nyingi, na nawasii vijana wote katika sekta hii kuzidisha ubunifu kwani fursa ipo kubwa sana.

Sekta ya sheria kwa upande ya digitali bado ina fursa nyingi sana haswa kwa vijana wabunifu Tanzania.

Popote ulipo unaweza kupata application Sheria Kiganjani au tembelea sheriakiganjani.co.tz kwa kuwasiliana na mawakili wetu na kwa msaada zaidi.

Previous ArticleNext Article
Leonce Godfrey has been in the field of Digital media and digital marketing with more than 3 years experience working in various capacities with highly reputable companies and organizations. He is writer, storyteller, content creator, photographer and journalist by professional. He simply amazing.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Send this to a friend