Maswali matano na Neema Loth

Neema Loth ni ni afisa habari na mahusiano kwa umma, pia ni mwazilishi wa Digital Detox Tanzania.

1. Nini ni maana ya “Digital Detox?”.

‘Digital Detox’ ni neno la kiingereza ambalo mimi na team yangu tumelitohoa kwa kiswahili na kupata ‘kutoa sumu kidijitali’.

Huu ni mchakato ama muda ambao mtumiaji wa vifaa vya kidijitali anapunguza matumizi ama anaacha kwa kipindi fulani matumizi hayo ili kujumuika na mazingira halisia na watu halisia. Na hii ni kwa ajili ya kupunguza sonona, presha mtu anayoipata kutoka kwenye ulimwengu wa kidijitali au mitandao ya kijamii, na athari nyingine ambazo zinaweza kutokea kutokana na kujikita sana kwenye ulimwengu wa kidijitali.

Huu ni mchakato […] ambao mtumiaji wa vifaa vya kidijitali anapunguza matumizi […] hayo ili kujumuika na mazingira halisia na watu halisia.

2. Walengwa wa hii Digital Detox zaidi ni akina nani? Na ni vipi mnaweza kuwasaidia watu wenye uraibu wa mitandao ya kijamii?

Walengwa wetu wakuu wako katika makundi matatu:

  1. Vijana
  2. Watoto
  3. Watu wazima ama wazazi

Tunaweza kuwasaidia watu wenye uraibu wa mitandao ya kijamii kupitia huduma zetu ambazo ni kwa kutoa mafunzo (training), consultancy (sana sana kwa watu wa ofisini na makampuni), Digital Detox Retreats / tours, na Digital Detox therapies ambayo itamlazimu mtu kuonana moja kwa moja na mwanasaikolojia na kupata msaada.

3. Je, gharama za huduma zenu zipo vipi? Na mnaweza kuwafikia vipi watu ambao wanahitaji huduma zenu?

Gharama zetu ni nafuu sana, kwa sababu walengwa wetu wengi ni wananchi wa kawaida kabisa kwa sasa na ni shauku yetu tuweze kuwafikia wote wenye uhitaji na huduma zetu.

Sisi tunadeal na watu walioathirika kidijitali, kwa hiyo namna nzuri ya awali kabisa ni kuwafikia kupitia njia za kidijitali.

Kwa hiyo tunawafuata huko huko kwenye mitandao ya kijamii tukiwapa maarifa na kuwasha taa vichwani mwao kwamba hili ni tatizo na sisi tupo kuleta jawabu la tatizo hilo.

4. Kwa uzoefu wako, madhara ya uraibu wa matumizi ya mtandao utakuwa vipi baada ya miaka mitano ijayo kwa vijana?

Kama ilivyo kwa ugonjwa mwingine, usipotibiwa unakua vibaya zaidi.

Hata kwenye ulimwengu huu wa kidijitali, madhara yatakua mabaya sana kwa miaka mitano ijayo kwa vijana kama hatua za ufumbuzi wa suala hili hazitachukuliwa kuanzia sasa.

5. Una nini la kushauri lifanyike ili kuepuka uraibu wa mitandao ya kijamii?

Sisi kama LOG IN DETOX tutaendelea kutoa elimu hii pasi na kuchoka, lakini pia tunaomba sekta nyingine na serikali zituunge mkono katika hili, kwa pamoja tutatengeneza vizazi bora zaidi kama tukianza leo kulishughulikia hili kwa pamoja.

Unaweza tembelea mitandao yao ya kijamii, Instagram @digitoxe na Twitter @digitoxe

Previous ArticleNext Article
Leonce Godfrey has been in the field of Digital media and digital marketing with more than 3 years experience working in various capacities with highly reputable companies and organizations. He is writer, storyteller, content creator, photographer and journalist by professional. He simply amazing.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Send this to a friend