Maswali matano na Abel Shoo

Abel Stanley Shoo ni Muanzilishi na Mkurugenzi mtendaji wa Gengeni Delivery App.

  1. Gengeni Delivery App inajihusisha na nini na ulipata wapi wazo la kufungua kitu kama hiki?

Gengeni Delivery inajihusisha na uuzaji wa vitu mbalimbali kutoka sokoni na kuwafikishia watu wanaohitaji kununua kwajili ya matumizi yao binafsi.

Nilipata hili wazo baada yakutembelea soko la Boma wakati wa mvua nilikuta mazingira sio rafiki ya mimi kushuka kwenye gari na kwenda kupata huduma, niliona kuna haja ya kuwa na huduma kama hii ambayo itakuwa inakuletea huduma mbalimbali za sokoni mpaka nyumbani.

2. Gengeni Delivery App imeweza kuwafikia watu wangapi?

Kwa sasa ni kwa wakazi wa Dar tu ndio wanaweza kutumia huduma yetu. Takribani watu 2,000 wanatumia app yetu kupata huduma zetu. Na bado tuna mipango ya kupanua huduma zetu na ziweze kupatikana Tanzania nzima.

3. Mmejitofautisha vipi na application nyingine zinazotoa huduma kama zenu?

Kwanza, app yetu ni rafiki kutumia kwa mtu yeyote yule. Na tunauza bidhaa za vyakula tu. Pili, tunajitahidi kuwafikishia bidhaa zenye ubora wateja wetu.

4. Changamoto gani ambazo mnakutana nazo kama vijana mlioamua kuwekeza kwenye digitali Tanzania?

Ukosekanaji wa mazingira mazuri ya kiuendeshaji biashara hasa katika sera.

Digitali inabidi itambulike kama sekta rasmi ambayo inaweza kusaidia vijana na kupunguza msululu wa tozo na vibali katika uendeshaji wake.

5. Ikitokea mtu anataka kuwasaidia, ungependa msaidiwe kitu gani?

Tungependa kusaidiwa katika kuboresha huduma zetu na kuweza kuwafikia watu wengi zaidi ikiwezekana Tanzania nzima ili tuweze kutimiza malengo yetu.


Previous ArticleNext Article
Leonce Godfrey has been in the field of Digital media and digital marketing with more than 3 years experience working in various capacities with highly reputable companies and organizations. He is writer, storyteller, content creator, photographer and journalist by professional. He simply amazing.

This post has 3 Comments

3
  1. Je nini matarajio yako kuhusu gengeni baada ya miaka Mitano. Na unaonawapi ikifika na kusaidia watanzania kuweza kufanikiwa kupitia gengeni

  2. In the next five years our operations will cover half the country interms of serving Customers and also will help craate jobs in regions where will set up our farms. we are investing heavily in research so that we can have the exact data to help build the propoer infrastructure

  3. Hii application imemsaidia sana mama yangu na anaona kwamba inabidi akina mama wengine waweze kufahamu kuhusu application yenu unawezaje kulishughulikia hili?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Send this to a friend