Maswali matano na THL

Alex Patrick Achimpota, ni muhitimu wa shahada ya kwanza katika maendeleo ya fedha na uwekezaji chuo cha Mipango Dododa.

Kwasasa anajishughulisha na uwekajia wa mifumo ya kihasibu kwenye makampuni na biashara mbalimbali.
Kampuni anayoifanyia kazi inaitwa Twiga Hosting Limited (THL), ni mkufunzi katika mfumo wa kihasibu wa THL Accounting.

1. Ni nini maana ya THL na inajishughulisha na nini?

Thl ni kifupisho cha jina (Twiga Hosting Limited), ni kampuni inayojishughulisha na huduma mbalimbali ya kiteknolojia ikiwemo na mfumo wa kihasibu wa THL Accounting, ambao unabadilisha muenendo mzima wa kufanya na kuhifadhi taarifa mbalimbali za kihasibu kutoka kwenye makaratasi na kufanya kisasa zaidi na kuhifadhi taarifa kidigitali.

2. Kwanini unashauri mfanyabiashara atumie THL, ina faida gani kwao?

THL ni mfumo rahisi sana kuufanyia kazi, umetengenezwa kwa lengo la kumrahisishia mtumiaji urahisi wa kuhifadhi taarifa zake lakini bado zikiwa katika ufanisi mkubwa wa kihasibu, kama haitoshi gharama zake ni nafuu sana, jaribu kufikiri unalipa 80000 Tsh kwa mwaka mzima, hivyo kwa mfanyabiashara yeyote hii ni fursa adhimu.

3. THL imewezaje na inawafikiaje wafanyabiashara, hususani wadogo ambao wanaanza biashara?

Huu mfumo ni web based hivyo unapatikana online kwa kutumia kifaa chochote ambacho kinaweza ingia kwenye internet, hivyo kwa mfanya biashara wa daraja lolote ambae ana kiu ya kufanya mambo yake kisasa na mpangilio huu mfumo ni wa kuukimbilia na mpaka sasa kuna wafanya biashara zaidi ya elfu mbili wanaoutumia mfumo.

4. Ili uweze kutumia THL inahitaji gharama gani kwa upande wa hela na nguvu kazi?

Mfumo huu unaweza kutumika na mtu mmoja au zaidi ya mmoja, ambapo mmoja wao atakua kiongozi (admin) na ataweza kugawa majukumu kwa wengine kulingana na vitengo vyao, Mfano Mr A yeye atakua anafanya manunuzi, Mr B yeye atakua anafuatilia madeni na Mr C yeye atakua anafanya matumizi.

5. Una ushauri gani kwa wafanyabiashara kwenye matumizi ya digitali na platform nyingine kama THL kwenye kutoa huduma zao?

Mwisho kabisa napenda kuwashauri wafanyabiashara katika maeneo yote kama kiwe kiwanda au biashara ya kawaida ya kuuza na kununua au biashara ya kutoa huduma fulani kuutumia huu mfumo na kama watapata changamoto zozote msaada upo kwa masaa 24 na kwa watu wenye huduma kama THL napenda kuwashauri kufanya mifumo yao kuwa rahisi hasa kwa watumiaji sababu ndio walengwa wakuu.


Unaweza kupata taarifa zaidi za THL kwa kutembelea www.thlaccounting.com au kurasa yao ya instagram @thl_accounting. Au unaweza wasiliana na Alex kupitia +255 758 583272 au Instagram @alex_patrick.

Previous ArticleNext Article
Leonce Godfrey has been in the field of Digital media and digital marketing with more than 3 years experience working in various capacities with highly reputable companies and organizations. He is writer, storyteller, content creator, photographer and journalist by professional. He simply amazing.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Send this to a friend