Maswali matano na Dear Coco

Jacqueline Shuma ni mwanahabari mwenye shahada ya Mawasiliano ya Umma (Bachelor of Arts in Mass Communication) aliyoipata pale St Augustine University of Tanzania. Pia ni kati ya watu wenye ushawishi mkubwa katika mtandao wa Twitter (Influencer). Amefanya kazi za utangazaji na kwasasa ni dubbing artist.

Tofauti na watu mashuhuri wengine katika mtandao huo, Jacqueline ameamua kutumia kurasa wake wa Twitter kuwasaidia na kuwapa vijana sehemu ya kuelezea matatizo yao na kupata ushauri mbalimbali kutoka kwa watu wazoefu na wataalam. Jacqueline hufikisha jumbe mbalimbali anazozipokea kutoka kwa vijana na watu mbalimbali wanaopitia hali ngumu na msongo wa mawazo na kuhitaji msaada wa kiushauri kutoka kwa wadao.

#DearCoco ndio hashtag inayotumika kubeba maudhui yote yanayobeba harakati za Jacqueline katika kusaidia vijana wenzake. Na haya ndio mambo matano usiyoyajua kuhusu Jacqueline na harakati zake za Dear Coco.

1. Wazo la #DearCoco lilitoka wapi na ni nini kilikusukuma mpaka ukaanzisha hashtag DearCoco?

Hapakua na wazo la #DearCoco kwamba nilijipanga nije na kitu kama hicho. Ilitokea tu siku nilihoji kitu Twitter nikaomba wanipe majibu DM. Walifunguka sana kwa uwazi. Ndio nikagundua watu wana mambo mengi ila ujasiri wa kuyasema ndo hawana.

Hivyo niliona kuna umuhimu wa kufungua jukwaa ambalo litaweza kuwakutanisha watu na kutoa yale ya moyoni na matatizo yanayowakabiri kutibu msongo wa mawazo na mambo yanayowasumbua. Na hivyo ndivyo harakati za #DearCoco zilivyoanza.

2. Ni watu wangapi umeweza kuwasaidia katika harakati za #DearCoco?.

Ni wengi sana wanaweza kufika zaidi ya 100. Kuna wengine hujifunza kupitia matatizo ya wengine wanayopitia hivyo namba inaweza ikawa kubwa zaidi hata kwa maelfu kwa kuzingatia kiasi cha watu wanaonifuafa mtandaoni. Nashukuru Mungu watu wameniamini na kwa usiri mkubwa kama vijana tumekuwa tunasaidiana na kushauriana kwenye mambo mbalimbali kadri vile navyopokea jumbe zao.

#DearCoco imekuwa sehemu salama kutoa dukuduku zao. Naamini nitaweza kuwafikia watu wengi zaidi ili tuweze kusaidiana katika matatizo tunayoyapitia kila siku katika maisha yetu.

3. Ni kitu gani umejifunza katika harakati zako za kusaidia watu mtandaoni?

Nimejifunza mengi ila sana sana uvumilivu. Kudili na jamii yataka uvumilivu sana. Tumetofautiana katika uelewa, elimu, kimawazo na kifikra. Inabidi umuelewe kila mtu na uheshimu misimamo yake.

4. Ni kitu gani kibaya kilichowahi kukukuta katika harakati zako za #DearCoco mpaka ukahisi kukata tamaa au kuacha unachokifanya?.

Kuna mtu alinitafuta akiwa ana msongo wa mawazo na anataka kujiua. Kwa bahati mbaya nilikuwa busy sikuona ujumbe wake kwa wakati. Akapost kusema ameamua kujiua na akatoa lawama kwamba alikuja hadi kwangu sikumsaidia. Nikapokea shutuma nyingi sana.

Nilipitia wakati mgumu, ila nashukuru nilielewa ni kuwa ni kati ya changamoto za kazi. Sio kila wakati kazi itaenda vizuri au vile umepenga. Kuna muda unaweza kupitia nyakati ngumu.

5. Una washauri nini vijana juu ya matumizi ya mitandao ya kijamii?

Wawe na staha. Imekua fasheni kuja mitandaoni kutukana na kukebehi watu ambao hata hawajakosea. Wajifunze kubishana kwa hoja na sio matusi. Wajifunze kujenga hoja.

Mitandaoni sio sehemu nzuri kukejeri na kukebehi watu. Kwa bahati mbaya huwezi jua huyo mtu anapitia nini kwa wakati huo. Tuwe wafariji na washauri maana watu wanapitia mengi huko chini. Tupeane amani ya moyo huwezi kujua unamsaidia mtu gani.


Unaweza kupitia na kufuatilia mijadara ya Dear Coco kwa kutafuta #DearCoco Twitter. Au kupitia account yake Twitter @YourFrenchFry na Instagram @itsdearcoco.

Previous ArticleNext Article
Leonce Godfrey has been in the field of Digital media and digital marketing with more than 3 years experience working in various capacities with highly reputable companies and organizations. He is writer, storyteller, content creator, photographer and journalist by professional. He simply amazing.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Send this to a friend