Maswali matano na Mussa Omary

Mussa Omary, ni kijana wa miaka 25 anayeishi Kimara, Matosa. Mussa ni mwanzilishi wa akaunti ya Instagram inayoitwa Nafeeltz, akaunti inayoongelea maswala ya hisia na maswala ya afya ya akili kwa uwazi.

Mussa alisoma DIT, kozi ya Mechanical Engineering mwaka 2016 na alisoma mwaka mmoja tu, hakufanikiwa kumaliza. Aliona kuwa Mechanical Engineering haikuwa kwaajili yake na hivyo akaacha chuo.

Baada ya hapo alienda kuishi Arusha na huko alijifuna graphics pamoja na website designing. Kwasasa yeye ni graphic na website designer na anafurahia mambo anayoyafanya kwenye maeneo haya huku akiendesha akaunti yake hiyo ya Instagram.

Tulipata nafasi ya kumuuliza Mussa maswali matano, na haya ndio machache aliyotushirikisha:

1. Tuambie zaidi kuhusu Nafeeltz. Wazo la kuanzisha lilikujaje?

Page ilianzishwa rasmi February 28, 2019 ni almost miaka 3 imeshapita sasa. 

Lakini kwanza kabisa nianze kusema binafsi niko na mapenzi ya kuandika nyimbo hususani za mapenzi lakini sijui kuimba na nilikua naogopa kujitangaza kwamba naandika nyimbo ni kwasababu nina aibu mnoo.

Licha ya hivyo niliwahi kuandika nyimbo kadhaa kisirisiri kisha nikampatia uncle wangu ambaye yeye yuko na talent ya kuimba lakini hajawekeza juhudi zake huko so hazikufika mbali.

Baada ya muda flani nikawa natafuta namna ya ku-share ujuzi wangu wa kuandika nyimbo huku sitaki kujulikana na hapo ndipo nilipopata wazo la kuanzisha page ya Instagram ambamo nitapost lyrics kadhaa za nyimbo nilizoandika katika mfumo wa quotes fupi fupi na hapo ndipo Nafeel ilipozaliwa kwa mara ya kwanza kabisa. 

Lakini baada ya miezi kadhaa ya kupost ndani ya page yangu watu kadhaa walijitokeza na kunifollow kutokana na mengi nilioandika yalikua yakiwagusa pia japo kila nilichoandika kilikua kinaelezea feelings zangu kweli hususani feelings za kuumizwa kimapenzi. 

Na hapo ndipo nilipo change perspective nzima kutoka kuandika na kupost lyrics za nyimbo na kuanza kupost feelings zangu pamoja na feelings za watu wangu wa karibu. 

Wengi wakawa wana relate na wakaanza kunifollow japo haikua kwa wingi so huu kwa ufupi ndio ulikua mwanzo wa page ya Nafeel.

Na kuhusu jina la “Nafeel” ni jina ambalo lilizaliwa kutokana na neno “Nahisi” nikireflect hisia zangu ambazo ndizo nilikua nazitumia kutengenezea misemo. So neno nafeel ni neno NA + FEEL (hisi) nimeongeza TZ (Tanzania) kureflect nilipo pamoja na kuwa accepted na Instagram kama username. 

2. Unadhani kuna umuhimu gani wa kuongelea hisia na tunayoyapitia kwa uwazi kama unavyoongelea kwenye jukwaa lako?

Unajua Eunice, kuna mengi ambayo tunakumbana nayo kila siku katika maisha hususani katika upande huu wa feelings. Na sometimes unapitia jambo ambalo linakugusa, linakuumiza kiasi kwamba hujihisi kama unathamani tena ya kuendelea kuishi na hali hii inatokana na kujihisi huna mtu ambaye anakuthamini au at least anaelewa kile ambacho unakipitia.

So page yangu ni mahala ambapo naweza kusema kuna wasaidia watu wa namna hii ambao wanahitaji mnoo kutokujihisi wako peke yao juu ya yale wanayo yapitia. 

3. Unahisi ishu ya afya ya akili kwa Tanzania inachukiliwaje?

Sijachunguza sana hicho kitu lakini afya ya akili ni moja ya vitu vinavyopewa uzito mdogo yaani vinavyopuuziwa mnoo kwa hapa Tanzania.

Inawezekana pengine ni kwasababu wengi hatuna elimu ya kujua faida na hasara za afya njema ya akili kwa binaadamu.

4. Unafikiri mitandao ya kijamii inawasaidiaje vijana kufunguka zaidi kama kwenye maeneo ya fursa na kwa kesi ya jukwaa lako kiafya ya akili?

Social media inampatia mtu yeyote power endapo ataamua kuitumia vizuri.

Kwa mfano mimi, am just a nobody, sio maarufu, sio hata yule mtu ambaye wengi walikua wananifahamu lakini kupitia power ya social media nimetengeneza kitu maarufu, kitu ambacho watu takribani 90,000 wanakifuatilia na hii ni fursa kubwa ya biashara endapo nitaamua kuwabadilisha watu kadhaa kati ya hawa 90,000 kuwa wateja na kujiingizia kipato licha ya kuwa nawasaidia pia

5. Unaonaje future ya jukwaa lako na mchango wake kwenye maisha ya watanzania?

Mission nilionayo kupitia page yangu ya Nafeel ni kuwasaidia watu wanaopitia nyakati ngumu (maumivu) kadri niwezavyo kwa kutumia teknolojia, na natamani kuendelea kufanya hivyo.


Check akaunti ya nafeeltz Instagram na wasiliana na Mussa kupitia akaunti yake binafsi hapa

Previous ArticleNext Article
Eunice is a multi-niche freelance writer with experience in writing health, lifestyle, finance, interviews, tech, travel, entrepreneurship, automotive, and mental health articles.

This post has 4 Comments

4

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Send this to a friend