Njia 5 za kupata wateja kwa urahisi na haraka Upwork

Hivi karibuni niliamua kujiunga na Upwork, baada ya kuona watu wengi wakiisifia Upwork kama sehemu nzuri ya kupata kazi za mtandaoni.

Ukweli ni kuwa wengi wanaisifia na wengi pia wanaiponda, inategemea na yapi unayapitia ukiwa kwenye jukwaa hili. Kwa wengi imekuwa ni sehemu nzuri lakini pia ni sehemu ya ushindani sana kwa sababu watu wenye ujuzi mbalimbali wako wengi hasa kutoka sehemu mbalimbali za dunia. Katika makala hii naenda kukushirikisha njia kadhaa ambazo nimejifunza na kuona kuwa zinanisaidia kupata kazi kwa urahisi na haraka kupitia jukwaa hili hata kama ushindani ni mkubwa.

Njia hizo ni:

Kuangalia ushindani wa kazi kwa idadi ya watu waliotuma proposal

Ni rahisi sana kupata kazi kama ukiwa wa kwanza kwanza kutuma maombi, mwanzoni wakati najiunga nilikuwa kila saa naangalia Upwork ili niwe wa kwanza kwanza kuomba kazi. Ni ngumu sana kupata kazi kama ndio umejiunga wengine huchukua muda mrefu kidogo kabla ya kupata, ila mimi nilipata wiki hiyo hiyo ya kwanza niliyojiunga.

Tuma maombi kwa kazi ambazo zimeombwa na watu 5-10, ni rahisi kupata hapo kliko zile zilizoombwa na watu 20-50, hapo soko lina wengi sana, nafasi ya wewe kuonekana wa pekee inakuwa imepungua. Kwahiyo jitahidi uwe wa kwanza kwanza kutuma maombi na utume ukiona idadi ile ya 5-10

Mshawishi mteja kwa kujionyesha kuwa unaweza kufanya aliyoyataja

Jitahidi kusoma maandishi ya mteja kwa ufanisi na unapotuma maombi, jitahidi kugusia yale aliyoyaeleza. Jiuze vizuri, uza ujuzi wako wa yale aliyoyaeleza na jinsi gani unaweza kutatua matatizo yake. Fanya maombi kuwa mafupi ila hakikisha unamwonyesha ni jinsi gani wewe ndio chaguo zuri la kazi yake hiyo na sio wengine, mwambie kwanini akuchague wewe na jibu rahisi ni kuwa unaweza kufanya yale aliyoyataja na unaujuzi nayo kwa vile umeshawahi kuyafanya.

Usipende kutuma maombi kwa kampuni ambazo malipo hayajawa verified

Nitapenda kusikia kwa wengine kuhusu hili kama walishawahi pata kazi kwa kampuni au mtu ambaye malipo yake hayajawa verified na Upwork, binafsi kwa wote niliowaomba ambao hawakuwa verified waliishia kufungiwa na Upwork kwa kutotimiza masharti na wengine kuwa ni utani tu hawakuwa serious kwamba wanatafuta freelancer.

Ukweli ni kuwa njia rahisi ya kumpima mtu unayetaka kumtumia maombi ya kazi Upwork ni kuangalia mrejesho aliopewa na wengine, kama wamesema ni mtu mbaya kufanya naye kazi au lah, unaweza angalia malipo, je ni mlipaji mzuri ukifanya naye kazi? Amelipaje wale aliowahi kufanya nao kazi? Na haya unaweza kuyaona kama malipo yake yako verified, ndio maana nashauri hili ili usije ukapoteza tu muda kuomba kwa mtu ambaye haujui ufanyaji kazi wake ukoje.

Omba kazi ambazo zinakuvutia na unaona utafurahia kuifanya

Kuna kazi ukisoma tu maelezo unaona hii naitaka, yani hii lazima niipate, nitapenda kuifanya, omba hizo. Maombi ya ili mradi maombi na maombi ya kweli unaipenda kazi yako tofauti, jitahidi pia kuchagua kazi na utume maombi kwa zile ulizozipenda kweli.

Punguza gharama kidogo

Pale alipoweka bajeti yake, jitahidi kushuka kidogo. Wengi sio kwamba wanapenda kutumia hela kivile hata wewe huwa unenda kununa huduma au bidhaa sehemu yenye punguzo la bei. Ukipunguza kidogo unnamfanya mteja arukie kwako kwasababu duniani kote wote tunapenda kulipia gharama kidogo kwa chochote tunachonunua. Usipunguze sana mpaka unajikuta unfanya kazi nzito malipo kidogo ila jitahidi kwenye kila maombi kushusha bei, akiweka bajeti $300, wewe kwenye maombi weka $250.


Kwa kuongezea, hakikisha kwenye maombi yako unamalizia na swali. Hii ni nzuri kwasababu unampa mteja neno la kuanzia akija kuongea na wewe, anajibu tu swali lako nakuendelea na maelezo kuhusu kazi. Uliza swali linaloendana na kazi aliyotoa maana inaonesha kuwa umesoma na unatamani kuifahamu kwa undani. Na kama utapenda basi, tuma link ya kazi zako nyingine kama sample. Kwa kazi ambazo unahisi zinafanana na ulizowahi kufanya au ukionyesha zipo sehemu fulani ujuzi wako utajulikana zaidi basi hakikisha unaweka link yako. Muda mwingine maelezo ya kazi husema weka link, hii husaidia pia kwa mtu kuona kwamba una ujuzi na utaweza kazi yake.

Jitahidi pia kuangalia nchi anazotaka freelancers, ukishaona alama nyekundu unapoangalia maelezo ya kazi, usiiombe. Hiyo inamaana kuna vigezo hauna, unaweza kuomba ila mwajiri ataona kuwa hauna vigezo vyake hivyo kuipata kazi ni kwa neema.

Ni matumaini yangu kuwa dondoo hizi zitakusaidia kupata kazi kiurahisi na kwa haraka Upwork na kama bado haujajiunga bonyeza hapa kufanya hivyo.

Previous ArticleNext Article
Eunice is a multi-niche freelance writer with experience in writing health, lifestyle, finance, interviews, tech, travel, entrepreneurship, automotive, and mental health articles.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Send this to a friend